Kituo cha Mabasi cha Magufuli kimegeuka soko kwa sababu ya usimamizi mbaya

Kama wanaosimamia wameshindwa kazi wapewe usaidizi. Tatizo sio wafanyabiashara wadogowadogo
Hivi unawajua wafanyabiashara wadogowadogo au unawasikia? Msiwababeshe lawama wasimamizi.nendeni Nyie wenyewe mkawapangie maeneo ya kufanyia biashara muweke na masharti mnawatafutia lawama wenzenu.
 
Nani sasa awaguse wakati mwendazake aliamuru wasiguswe waacheni tu mapaka watakapo oona kero ndio watawatfutia sehwmu nyingine....
 
Kituo cha mabasi kinatakiwa kutumika kama kituo cha mabasi kulingana na mpango kazi uliowasilishwa na kutekelezwa. Wafanyabiashara ndogo ndogo hata kama waliwahi kutetewa na hayati JPM wapewe somo upya na wapangiwe sehemu rasmi za kufanya biashara,siyo stendi kuu ya mabasi.

Vinginevyo, waunganishe mitaji yao, waunde ushirika wa wafanyabiashara wapangishe vyumba vilivyokwisha jengwa pale ili kuwe na mahali rasmi pa kununua bidhaa kwa wasafiri wanaopenda kula kula kama mchwa. Kuwe na utaratibu, sheria zizingatiwe na walipe kodi. Hivi ni nani anailinda haki yangu ya kusafiri bila kubughudhiwa pale nisipotaka kununua chochote ninaposafiri?

Tuachane na hii tabia ya kujifanyia mambo kama kwamba hakuna sheria, mimi ninapopanga safari sihitaji kulazimishwa kusikiliza mziki wowote, kuangalia video au kulazimishwa kula au kunywa, watu watafute ridhiki ndio,...lakini wafuate utaratibu uliowekwa na waliopewa Mamlaka ya kusimamia wasiyumbishwe kama kwamba siyo watalaamu.
 
Unakubali kuwa kuna kutokuwajibika kwa viongozi katika suala la wamachinga kujaza barabara, hapo hapo unapinga wanaotoa hoja ya kurekebisha hiyo hali hawawapendi wamachinga sababu ya JPM🤣🤣.

Wewe ni vuguvugu, unakaa hapo katikati, si moto si baridi.

Unaamini kuwa si sawa walivyojazana kila sehemu na kuna viongozi hawawajibiki ila wakati huo huo unapinga kurekebisha hilo sababu sijui JPM imekuwaje kulingana na akili yako.

Kufuata utaratibu si kurekebisha hili la wao kujazana sehemu wasizotakiwa kuwepo? Au unasimamia lipi wewe?
 
Mtu akiuza nyanya zake barabarani wewe mpitaji unapungukiwa nini??
Akiuza nyanya bila kuzuia barabara nikiwa natembea kuelekea nyumbani au naendesha usafiri kupeleka mtu hospitali mfano hivi hakuna tatizo. Hapo ni sokoni, imagine sasa sehemu ambayo hakuna soko ila kuna hiyo hali na ww ni mtumiaji wa barabara hiyo.







 
Mtu akiuza nyanya zake barabarani wewe mpitaji unapungukiwa nini??
hebu jaribu kupita maeneo ya kariakoo halafu bahati mbaya ukanyage nyanya za mtu ambae amezitandaza barabarani uone watachokufanya. Halafu hapo utajua utapungukiwa nini.
Wamachinga kwa kuweka vitu barabarani wamejimilikisha barabara za halaiki na kujiona wapo sahihi. Hakuna mtu anaepinga uwepo wao maana wanasaidia katika kuuza bidhaa za muhimu, tatizo linakuja wanazingatia vipi mahitaji ya watumiaji wengine wa maeneo wanayoweka biashara zao.
 
Ni wazo zuri, lakini kuwaondoa si sahihi bali wawekewe utaribu mzuri ambao wao wataendelea kupata ridhiki zao bila kuwakwaza wapita njia.
 

Unapambana sana kuhamishia chuki za JPM kwa machingaz ila huwezi kufanikiwa

Una roho mbaya kiasi cha kutamani binadamu wenzio waondolewe wanakopatia riziki wafe njaa badala ya kujadili jinsi ya kuboresha utaratibu ili waendelee kufanya kazi kujipatia kipato

Kweli kila mtu ana ubongo ila matumizi ndio tofauti...... jitahidi kutumia ubongo wako kujenga zaidi ya kubomoa
 
Ww si mstaarabu sababu unatumia jina la JPM vibaya kuhalalisha hoja zako za uvuguvugu.

Kwani nikuulize, wamachinga kutolewa barabarani na wakawepo sehemu zao kuna uhusiano gani na chuki au mapenzi kwa JPM?

Sio wewe uliyekubali kuwa sehemu walipojazana wamachinga barabarani viongozi hawawajibiki?
 
Hawa wanatakiwa waondolewe na kupewa maeneo maalumu, machinga wamekuwa kero sana ktk miji mikubwa.
 
Kama wanaosimamia wameshindwa kazi wapewe usaidizi. Tatizo sio wafanyabiashara wadogowadogo.
Hakuna haja ya kuwagusa kama ina maana ya kuwaondoa
Ila ipo haja ya kutengeneza mfumo mzuri wa wao kuwepo kwa manufaa ya wote
Umeandika sanaaaaaaa kwanini hawa wamachinga wanakuumiza hivi?

Waache wenzio wapate rizki sababu nao wana mahitaji kama yako japo hawana kazi sawa na yako
Tuacheni tutafte rizki jamani
Mbona mnaleta nongwa???
@mama D utaacha lini unafiki?
 
Mataga hao hawajielewi mkuu?
 
Shida ya hao machinga ni kufunga njia hata kwa wapita njia kwa miguu na ukipita wanaporomosha matusi I wish I could be president in jiwes voice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…