Hata mimi nilitaka kuitaja zambia sababu ndio nchi walau tunaendana kiuchumi, Lungu katuzidi sana, stendi yake biashara zote ziko kwenye fremu kubwa na vifremu vidogo, hakuna bidhaa iliyomwagwa chini wala vimeza meza. Highway yao ya kutokea huku kwetu hakuna banda la turubai utaliona linapepea pembeni mwa barabara, na sehemu za biashara zote highway ziko mita kadhaa kutoka barabarani. Angalau ndicho nilichokiona kwa mwaka huo 2018 nilipokua hapo sijui kwa sasa.
Huku mambo yaliyofanyika kwa miaka mitano mfululizo sidhani kama kuna kiongozi atayekuja kuweza kupambana na machinga wanaopanga biashara zao hadi mabarabarani. Itabidi kutumia mabavu kuwaondoa which sio sahihi au kuwaomba sana na kuwanyeyekea wahame, kitu ambacho nacho hawatatii.