Kituo cha Mabasi cha Magufuli kimegeuka soko kwa sababu ya usimamizi mbaya

Mwendazake alisema WASIBUGHUZIWE..!! Only to gain political cheap popularity..!!!
 
Kwahiyo ulitaka hao waliopewa thamana ya kusimamia hio section wapingane na kaul ya mume wao jiwe?,jiwe alishasema wamachinga waachwe wafanye biashara wasiguswe
 
Hao waliopewa dhamana za mipango miji wanakula mishahara miaka nenda rudi na bado tu hawapati ufumbuzi wa kuwapanga Machinga na kina Mama wauza mboga.

Tatizo ninusimamizi
Na hili sio tatizo kwa machinga tuu! Hata garage bubu, bars lounges , vituo vya bodaboda......
 
Nilimsikia juzi Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo alisema kwamba wamejipanga kuwaondoa na kuwawekea utaratibu mzuri
 
Bora wawafukuze wamachinga wote , stendi ibaki kuwa stendi na siyo gulio. Aliyewaruhusu kuifanya stendi hiyo gulio ameishaondoka na harudi tena. Ni wakati sasa kufuata utaratibu na siyo utashi wa mtu mmoja
 
Hali hii ya wamachinga kupanga biashara popote penye nafasi niliiona huko huko Zambia mwaka 1995, Lusaka nzima ilijaa vibanda vya biashara kila mahali, kama kweli wamebadilika basi watendaji wetu waende wakajifunze mbinu zilizotumika hadi wakafanikiwa.
 
Hali hii yakupanga biashara barabarani imeharibu taswira ya jiji la Dsm, baya zaidi barabara kuu iendayo kusini Kilwa Road, maeneo ya Mbagala R3, machinga wametandaza biashara zao Hadi barabarani, askari barabarani wanawashuhudia hawawasemi kisa, eti wanalipa kodi
 
Nilipita pale wiki2 zilizopita nikaambiwa vyakula haviruhusiwi kuingizwa kituoni kwa sasa ila vinapatikana upande wa pili wa kituo
Pia niliambiwa ujenzi unaendelea... na ukikamilika kila kitu kitakua sawa
Uliambiwa kama nani au Taga
 
Waziri UMMY MWALIMU, Mkurugenzi wa Manispaa na viongozi wengine wana husika na suala hilo, ila kwa sasa wana subiri wananchi wainue MABANGO ndipo watatekeleza.
 
Exactly!
 
Hebu weka picha hapa nione vitunguu katikakati ya barabara
Hakuna haja ya kukuza mambo kiasi hiki
Uzuri nipo mkoani Kesho kama nikipita mtaa huo mpaka wameubatiza jina kipande cha kariakoo na ni mkoani ntakupigia picha. Nilishangaa sana, barabara ya lami imefungwa kabisa huwezi katiza. Kunauzwa nyanya, kuna wa mishkaki, popcorn, nguo yaani balaa...
 

Wakati unapita kupiga picha uombe na maelezo toka kwa wahusika kabisa

Changamoto zinapatiwa suluhu kwa kuzifanyia kazi na sio kwa kulalamika bila hata kuwa na maoni au mapendekezo

Maendeleo hayana vyama

Usisahau kuniletea zawadi huko mkoani utokakoπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„
 
Manispaa ya ubungo baada ya kupewa kituo hiki wameshindwa kukisimamia kabisa... Hadi Leo hawajui Hao wafanya biashara eneo Lao litakuwa lipi.. Kuna wakati walitaka Kuwa toa wakawashindwa.. Mpaka Sasa pia Hao wafanya biashara hawajaanza kulipia eneo.. Meneja pia Ni mzembe sana...Bila suma jkt hicho kituo kingekuwa hakitamaniki
 
Swala la machinga ni la muda amini nawaambia madhara yake tutaona
 
Mtu akiuza nyanya zake barabarani wewe mpitaji unapungukiwa nini??
napata hasara ya barabara kuminywa na kupelekea kuleta usumbufu na hata hatari kwa watumiaji wa barabara na hata baadhi ya barabara kufungwa kabisa.ieleweke kila kitu kina mahala pake mkuu kwani masoko yana nini wasiuzie sokoni watu wakawafuata huko au hata huko barabarani kukawekwa utaratibu mzuri kuliko kuwaachia tu kila mtu akaamua kujitandazia anapoona panamfaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kibaya zaidi kuna wafanyabishara wadogo wanaolipa kodi humo humo ndani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…