Kituo cha Mabasi Magufuli bei ya pango hadi Tsh. 1,200,000/= kwa siku

Kituo cha Mabasi Magufuli bei ya pango hadi Tsh. 1,200,000/= kwa siku

Mimi tokea tu Siku ile nikwazike na Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Kuwaruhusu Wamachinga wajitawale ndani humo nilijua kuna shida na hata sitaki kuyasikia yanayojiri huko kwani ni Upuuzi mtupu tu.
Bila machinga kukanyaga humo hizo kodi za pango zingekua fair?!
 
Mimi tokea tu Siku ile nikwazike na Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa Kuwaruhusu Wamachinga wajitawale ndani humo nilijua kuna shida na hata sitaki kuyasikia yanayojiri huko kwani ni Upuuzi mtupu tu.
Ha ha ha
 
Sasa kama mjasiriamali amepewa fremu ili auze maji na soda ndani ya kituo ghorofani kwa kodi (rent) ya Tsh. 36,028,200/= kwa mwezi sawa na Tsh. 1,201,000/= kwa siku uhalisia uko wapi! Machinga wanauza maji na soda hizo hizo ndani na nje ya kituo hicho hicho kwa rent ya kitambulisho chake cha Tsh, 20,000/= kwa mwaka sawa na Tsh. 55 kwa siku.

Attached ni mchanganuo wa bei ya pango kama ulivyoidhinishwa na DCC kabla haijavunjwa na Hayati Rais Magufuli mwezi February 2021 wakati wa uzinduzi.

Data hizo ni kutoka waraka ulioidhinishwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa DCC uliosomeka "“Majina ya walioshinda zabuni ya upangishaji maeneo ya biashara na utoaji huduma mbalimbali katika Kituo Kikuu cha Mabasi Mbezi Luis 2020”

Mipango mingi ya ajabu ya aina hii kupitia TAMISEMI imeshindwa kama vile: Bus stand ya Dodoma, Machinga Coplex ya pale Ilala, Mwal Nyerere Airport Terminal 3, machinjio ya Vingunguti nk.

Ummy Mwalimu take action please, hapo hakuna biashara.
Data hizo ni kutoka andiko G. Kombe.

View attachment 1756589
Naanza kuona kituo kikianza kuwa sehemu ya kusambazia unga mikoani na nje ya nchi , kwa biashara za halali huwezi kulipa kodi hizo
 
We ni mjinga kama unetetea hayo mamilioni
Investment ya 60B mnataka mlipe kodi ya laki na nusu kwa mwezi, unategemea huo mradi utarudisha lini hela?

Miaka michache ujayo wakishindwa kuendesha stend kwa uchafu na uchakavu bado mtarudi kuwasema wameshindwa, poor management sijui maneno gani
 
Wanataka watu washindwe ili wawaweke watu wao, yule mbunge aliyesifiwa atuambie amechukua hatua gani?
 
Ngoja tuendelee kupasha sisi tunakuja kuwatetea wanyonge huko au nasema uongo ndugu zangu?
GWAJIMA SLIDER_1.jpg
 
Wanataka watu washindwe ili wawaweke watu wao, yule mbunge aliyesifiwa atuambie amechukua hatua gani?
Huyo Mbunge hashikiki tena wala simu za wanajimbo hapokeagi tena akifikiri 2025 ni mbali sana.......
 
Back
Top Bottom