Kituo cha Mabasi Magufuli bei ya pango hadi Tsh. 1,200,000/= kwa siku

Ayo maji unauza peke ako, hivi unajua faida anayopata kwemye chupa moja ya maji?
 
Hawajui Biashara na hili ndio tatizo la serikali kutokukubali ukweli, hio stand wangetafuta mwekezaji na wao wachukue kodi, pesa iliyotumika ni nyingi, Kituo baada ya miezi sita hakitamaniki na pesa haitakaa irudi. Sekta binafsi ndio Engine na Jeshi la kiuchumi la nchi. Serikali ibaki na miradi mikubwa sana na Kuwa mwangalizi wa sekta binafsi sio kendesha Biashara Ndogo Ndogo
 
Investment ya 60B mnataka mlipe kodi ya laki na nusu kwa mwezi, unategemea huo mradi utarudisha lini hela?

Miaka michache ujayo wakishindwa kuendesha stend kwa uchafu na uchakavu bado mtarudi kuwasema wameshindwa, poor management sijui maneno gani
Mpangishie baba yako
 
Kuna watu wana comment tu, hivi biashara mnaijua na mzunguko mnaujua? Hapa mjini kwangu kuna Fremu walipokuwa Voda wanaiachia sababu kodi kubwa. Kodi ni 6M kwa mwezi. Sasa watu kama voda wana lia lia juu ya suala la kodi ya pango sisi wananchi wa uchumi wa kati feki je?

Kodi kama hizo zitawezekana kwa mzunguko wa kariakoo labda.
 
Kama hizo data ni za ukweli basi tuendako si swali.lakn kwa akili za kawaida hakuna biashara ya aina hiyo kwa mzunguko upi?cjui na siamini kama ni kweli anyway basi yajao yanashangaza.
 
Hizo data ni za kweli kabisa na zilipatikana kutokana ma release ya DCC December 2020 kwa wazabuni 200 walisemekana wameshinda tender kituoni hapo (online tendering) iliyoendeshwa na TAMISEMI. Mleta mada yeye alifanya analysis tu na kupablish.
Kama hizo data ni za ukweli basi tuendako si swali.lakn kwa akili za kawaida hakuna biashara ya aina hiyo kwa mzunguko upi?cjui na siamini kama ni kweli anyway basi yajao yanashangaza.
 
Hizi bei zilipangwa lini? JPM alibahatika kuziona au kuzifahamu wakati wa uhai wake?
JPM hakua mmiliki wa stendi wala nchi....alipaswa afanye kazi kwa taratibu za kisheria...hata asipokuwepo wanaotekeleza wajibu wake hawawezi kukosa
 
Kuna upotoshaji mkubwa sana hapa
 
wamefikaje kwenye hizi hesabu? ama jiwe ndio aliwapa maelekezo?

maana sioni biashara za kuingiza pesa namna hii na faida ikawepo.

kwani pamekuwa 'Kalia-koo'?
 
wamefikaje kwenye hizi hesabu? ama jiwe ndio aliwapa maelekezo?

maana sioni biashara za kuingiza pesa namna hii na faida ikawepo.

kwani pamekuwa 'Kalia-koo'?
kuna phrase ya "white elephant" huwa inatumika kuelezea projects kama hizi .
 
Hivi mabasi yote yanaanzia hapo hata zile El Saedy za Mbeya?
 
Investment ya 60B mnataka mlipe kodi ya laki na nusu kwa mwezi, unategemea huo mradi utarudisha lini hela?

Miaka michache ujayo wakishindwa kuendesha stend kwa uchafu na uchakavu bado mtarudi kuwasema wameshindwa, poor management sijui maneno gani
36m frame kwa mwezi hata iwe investment gani hamna Kodi kama hyo kwa biashara za stand
 
Wameanza kwenda kinyume na kauli za rais, hawa watu ni washenzi sana wanadhani maisha in rahisi waanzaishe wao hizo biashara tuone kama watalipa hizo kodi. Kodi ya miaka mitano unalipa kwa mwaka.
 
Hahaaaaa mitano tena wanawaneeeeeeeee , napata raha sana kwenye haya mambo
 
Hiv is this real au kuna errors zilifanyika?
 
Hehehe ni kama vile natazama picha la kutisha hivi
 
Duh kama ni kweli basi kunashida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…