DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Aly Senga Gugu, amezindua rasmi kituo kipya na cha kisasa cha polisi cha daraja B Wilaya ya Namtumbo, kilichojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 798. Uzinduzi huo umefanyika tarehe 20 Juni 2025 katika eneo la Namtumbo, mkoani Ruvuma.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mkuu Gugu amewataka maafisa wa ukaguzi na askari wa Jeshi la Polisi nchini kote kuendelea kuzingatia misingi na maadili ya jeshi hilo. Ameeleza kuwa upelelezi bora wa mashauri ni msingi muhimu wa haki na utawala wa sheria katika jamii, hivyo ni jukumu la askari kuhakikisha hawawi chanzo cha ucheleweshaji wa mashauri hayo.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco Chilya, amesema ujio wa kituo hicho kipya ni faraja kwa jeshi hilo na wakazi wa Namtumbo, kwani awali walilazimika kutumia kituo chakavu na cha kuazima, jambo lililokuwa likihatarisha ufanisi na usalama wa askari na wananchi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mhe. Bi Ngolo Malenya, amemwomba Katibu Mkuu Gugu kusaidia wilaya hiyo kupata mahabusu, akieleza kuwa kwa sasa watuhumiwa wanaoshtakiwa katika Namtumbo wanalazimika kusafirishwa hadi Songea, hali inayowapa changamoto ndugu wa watuhumiwa hao kufuatilia kesi na kuwaona wapendwa wao.
=============================
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Senga Gugu, amefungua rasmi Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma chenye hadhi ya Daraja B, kilichojengwa kwa gharama ya Shilingi milioni 798
. Ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha miundombinu ya usalama nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mkuu Gugu alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mahiri unaotoa kipaumbele kwa sekta ya usalama.
Aidha, alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Namtumbo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Vita Kawawa, kwa mchango wake mkubwa katika kufanikisha mradi huo.
Gugu alieleza kuwa katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Serikali imeongeza juhudi kubwa katika kuboresha mazingira ya kazi kwa askari polisi, kwa kujenga na kukarabati vituo vya polisi nchini, hatua inayolenga kuimarisha huduma za ulinzi kwa wananchi. Alisisitiza kuwa ujenzi wa kituo hicho ni mfano wa namna Serikali inavyowekeza katika usalama wa wananchi wake.
Chanzo: ruvuma.go.tz/n