Tatizo ni viongozi wetu....sijui kuna shida gani kwenye nyazifa za juu pale...watu wakizipata hakuna kinachofanyika, mfano tulipata shida sana ya umeme miaka kama kumi nyuma, huko..mpaka tukaingia kwenye kashfa za richmond, IPTL etc.....mvua za kutengeneza kutoka Malaysia etc...Cha ajabu kama taifa hatukujifunza kitu..leo hii...tumerudi tena kule kule..umeme wa mgao....hivi kweli jamani??
Magufuli alikuja na Bwawa lake la maji tena, hivi kweli kwa jinsi mabadiriko ya hali ya hewa duniani kuna uhalali wa kurisk kuwekeza kwenye umeme wa maji ya mvua kweli???
Binafsi kama taifa tungefanya tafuatayo:
1.Kutokuongeza ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme badala yake twende kwenye vyanzo mbadala.
2.Vyanzo mbadala kama Gas ( Mtwara), Upepo (Tanzania ya kati-Singida etc)
3.Umeme wa Jua (Tabora, Shinyanga, Singida huko).
4.Mabwawa yaliyoko sasa etc....
Tuunde kikosi mkakati chenye maslahi ya Taifa, cha vijana wenye akili, utashi, elimu, wapandikizwe kwenye mabalozi yetu nje huko, watutafutie elimu hizo, hata kama kwa kuiba teknologia....vyuo vyetu vitengeneze maabara ya utafiti zaidi, vijana wapelekwe kusoma kwa malengo maalumu warudi na taaluma ambazo tunazihitaji kwanza kwa vitu basic...sio lazima tutumie wawekezaji wa nje...sisi wenyewe tufanyekazi kama kitu kimoja......wengine wakete elimu, tuzifanyie utafiti sisi wenyewe..tuanze mdogo mdogo..baada ya miaka kumi....tuko mbali..
Tujikite katika matokeo kuliko maneno na siasa