Kiufupi Yanga hawana kocha, ligi ya mabingwa makundi itapata aibu

Hii takataka inaondoka muda si mrefu! Kocha asiyejua sub ni kocha gani huo? Kama hawawezi kumrudisha Nabi basi watafute kocha mwingine mzuri!

* Mshery

* Hussein

* Komara

* Kazimoto

* Abdulhassani

* Ngoma

* Abushiri

* Mwijage


* Mzize

* Toure
Kwa wachezaji hao wewe ungekuwa kocha ungemwingiza nani
 
Kufungwa na Simba tu amekuwa mbovu!
Mimi nilianza kutia mashaka kwanzia mechi ya Pamba na ile ya Fountain gate. Alivyocheza dhidi ya Gaborone na dhidi ya Geita nikaona mashaka yangu yapo sahihi. Jana dhidi ya Simba ndio akaamua kupigia mstari kabisa. Kama timu inaomba mpira uishe dhidi ya Geita Gold na Gaborone tutegemee nini?
 
Wabongo ujuaji mwingi, vigeugeu tu. Yaani Yanga kufungwa na Simba eti leo imekuwa mbovu. Ngao ya jamii timu ilisifiwa na nyie wenyewe. Mechi moja kocha hawezi kuwa mbovu.
 
* Mshery

* Hussein

* Komara

* Kazimoto

* Abdulhassani

* Ngoma

* Abushiri

* Mwijage


* Mzize

* Toure
Kwa wachezaji hao wewe ungekuwa kocha ungemwingiza nani
Kwa upande wa sub huwezi kumlaumu kocha. Vipi kuanza kudefend baada ya kupata goli moja dakika za mwanzo kabisa?
 
Wabongo ujuaji mwingi, vigeugeu tu. Yaani Yanga kufungwa na Simba eti leo imekuwa mbovu. Ngao ya jamii timu ilisifiwa na nyie wenyewe. Mechi moja kocha hawezi kuwa mbovu.
Mkuu kwenye mpira kuna performance na kuna matokeo. Kama unaangalia matokeo pekee basi sawa kuwa kocha kafungwa mechi moja ila kama unaangalia mpira kwa angle ya kimbinu na ufundi basi kwanzia mechi dhidi ya Gaborone na Geita ilitoa picha juu ya mwenendo wa timu. Na kabla ya hapo kulikuwa na mechi ya Pamba na Fountain Gate ambazo zote hizo ilionesha Yanga kupungua makali. Hayu kipindi cha pili mara zote timu hushuka kiwango kwa Sub zake za hovyo.
 
Wewe unaujua mpira
 
Kwa upande wa sub huwezi kumlaumu kocha. Vipi kuanza kudefend baada ya kupata goli moja dakika za mwanzo kabisa?
Ni kwa sababu walikuwa wanashanbuliwa sana. Ukiwa unashambuliwa sana unatakiwa kujilinda na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
 
Tutatoboa tu na haya matokeo ya juzi ndo yatafanya tujiimarishe.
 
Tutatoboa tu na haya matokeo ya juzi ndo yatafanya tujiimarishe.
Jana mlikata moto mapeema

Sasa hebu tudokezee CCL tunakwenda na Mamqoba sijui Maboga au mnaleta mwingine wa kuja kumpa lawama?

Kumbuka Aragija hatakuwepo kwenye mechi zenu ujue 😂🤣😜
 
 
Jana mlikata moto mapeema

Sasa hebu tudokezee CCL tunakwenda na Mamqoba sijui Maboga au mnaleta mwingine wa kuja kumpa lawama?

Kumbuka Aragija hatakuwepo kwenye mechi zenu ujue 😂🤣😜
Kwa kipindi kifupi alichokaa mi nafikiria wampe tena nafasi ili kuepuka fukuza fukuza ambayo kuna saa haiwi na afya kwenye mustakabali wa timu na hata kwa wachezaji wenyewe.
 
Huyu kocha alizidiwa mbinu hadi na kocha wa Gaborone aliyekuwa na wachezaji wa kawaida tu, alizidiwa na Geita Gold iliyo na wachezaji wa kawaida tu. Huko ligi ya mabingwa si tutapata aibu huko?
Mimi siyo mtaalam sana wa mpira ila nilivyoona uchezaji wa Yanga kwenye mechi ya Geita Gold na Gaborone United hadi washabiki tunaomba Mungu mechi ziishe, nikajua hatuwezi kuifunga Simba this time. Ukichangia na sub za kocha nikasema hatutoboi. Mimi sikupoteza muda kuangalia hiyo mechi. Niliangalia Barcelona na Getafe.
 
Hili pia ni tatizo. Kipindi cha pili wanachoka na kushambuliwa sana.
 
Kwa kipindi kifupi alichokaa mi nafikiria wampe tena nafasi ili kuepuka fukuza fukuza ambayo kuna saa haiwi na afya kwenye mustakabali wa timu na hata kwa wachezaji wenyewe.
Kweli wewe unajua mpira. Tatizo la team zetu wanataka walime leo, wapande leo wapalilie leo na kisha wavuna leo hiyohiyo

Sasa soka halipo hivyo kuna wakati lazima ujipe muda wa kujenga team na kuvumilia makocha kama wenzetu wa Uingereza

Tatizo jingine ni viongozi wa klabu kutaka umaarufu mwepesimwepesi. Matokeo yake wanamtoa kafara kocha kwa kumfukuza huku makosa ni ya kwao kwa kutosajili vizuri
 
Kwa kipindi kifupi alichokaa mi nafikiria wampe tena nafasi ili kuepuka fukuza fukuza ambayo kuna saa haiwi na afya kwenye mustakabali wa timu na hata kwa wachezaji wenyewe.
Wampe nafasi ili afanye kipi ikiwa tunakoelekea ni kugumu zaidi? Kwenye klabu bingwa Yanga inaenda kukutana na timu yenye viwango zaidi ya Gaborone, Geita Gold na Simba. Sasa kama hizo timu zimeisumbua Yanga unadhani kuna lipi jipya atafanya?

Tuliona kwa Nabi, Gamond na Miloud wakati wanapewa timu, kadri muda utavyoenda na ndipo unaona kuboreka kwa viwango vya wachezaji na kiwango cha timu kwa ujumla, hapo ni sahihi kumpa nafasi kocha kwavile unaona kuna mwanga. Ila timu baada ya graph kupanda, inashuka tu, unatoa nafasi kwaajili ya lipi mkuu? Kama safari hii viongozi wa Yanga wapo serious na kucheza klabu bingwa basi wachukue maamuzi mapema, kocha huyu haiwezi kuifikisha mbali Yanga.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…