Pre GE2025 Kiukweli 2025 simuoni Rais Samia akishinda kwenye Boksi la kura kama upinzani wakiweka mtu mahiri

Pre GE2025 Kiukweli 2025 simuoni Rais Samia akishinda kwenye Boksi la kura kama upinzani wakiweka mtu mahiri

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Habari za usiku wakuu!

Licha ya kuwa Mhe. Rais anajitahidi kwa uwezo wake wote kutoa mchango wake katika kuipa nchi maendeleo lakini bado mwitikio kwa wananchi ni mdogo sana. Bado hajapata nguvu kwa wananchi waliowengi.

Najua wapo wapambe ambao wataukataa huu ukweli kwa manufaa wanayoyajua wao wenyewe. Lakiñi huku mtaani ni dhahiri kuwa Nyota ya Mama bado ipo chini. Hakubaliki.

NI vile upinzani nao upo legelege, haueleweki lakini acha tuone mpaka mwakani huenda mambo yakabadilika.

Akitokea mpinzani mzuri hasa anayetokea Bara nina hakika Samia atakuwa kwenye wakati mgumu kutetea kiti chake kwa njia halali.
Sijui kwa upande wa figisufigisu.

Kingine, Rais Samia kwenye kuongea hasa wakati wa kampeni sina hakika atazungumza kwa namna ipi ili kushawishi wananchi.
Maana uoñgeaji wake haupo kwa namna ya kushawishi. Anawéza akawa anaelezea vizuri lakini sio kueleza katika kiwango cha kumshawishi mtu kitu ambacho kwenye siasa ni kikubwa.

Binafsi nasubiri kwa hamu panapo majaliwa nione hizo kampeni.

Acha nipumzike sasa
Mbona mwamba Tundu Lissu yupo?
 
Kosa kubwa walilofanya ccm wote kuanza kumsema vibaya magufuli, issue ya bandari ndio ikafanya wananchi wamtoe kabisa vichwani mwao, na wale wsliomlinganisha Rais samia na magufuli ndio walimpoteza kabisa jumla
 
Ukiacha wakati wa Mkapa awamu ya 2 na Kikwete awamu ya 1, hakuna kipindi kingine CCM walishinda Uchaguzi
Sina uzoefu na awamu ya kwanza ya Mkapa, ya pili kidogo ila nina hakika kwa asilimia zifuatazo

Kikwete awamu ya kwanza alishinda kihalali, na Magufuli awamu ya Pili alishinda kihalali kabisa


Twende mbele turudi nyuma

Wengi walimpigia Magufuli sababu ya kazi aliyoifanya ijapokuwa mwaka 2015 hawakuwa wengi kivile ila baada ya kazi yake 2020 watu walifanya kweli

(Hii nina shuhuda kabisa kwenye eneo ambalo lilisifika kuwa ngome ya upinzani, nikaomba usimamizi wa kituo na nikayashuhudia yaliyo ndani ya boxsi la kura, na sio eneo langu tu hata kwa wenzangu)
 
Kosa kubwa walilofanya ccm wote kuanza kumsema vibaya magufuli, issue ya bandari ndio ikafanya wananchi wamtoe kabisa vichwani mwao, na wale wsliomlinganisha Rais samia na magufuli ndio walimpoteza kabisa jumla

Kwenye suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Samia yupo 75% wakati Magufuli 20%

Magufuli shida yake ilikuwa ni moja tuu. Ambayo ni kubwa, nayo ni kuminya haki za kujieleza hasa kwa wapinzani wake.

Huko kwingine alikuwa vizuri
 
Ila kupunguza zereuuu za CCM inabidi kweli apite mpinzani 2025,Heshima itarudi hata wakija kuchukua nchi.Angalizo,Mbowe hatumtaki,Lisu atulie tunajua nimtu smart lakini Energy ya kazi kubwa kama Urais hataweza.Wamchukue Makonda au Mpina au yeyote hakika nchi wanabeba.
Makonda kwako ndiyo anafaa kuwa rais ?

Hivi hii nchi mnaichukuliaje ?
 
Back
Top Bottom