Kiukweli kabisa hii wala sio timu yetu. Timu yetu ameondoka nayo Gamondi

Tulitegemea kuwa na msimu mzuri sana kwenye CL mwaka huu ila viongozi wameuharibu kwa sababu wanazozijua wao.
Pole mwana YANGA mwenzetu. Tunapitia wakati mgumu sana. Tuendelee ku support team yetu tu. Hakuna namna.
 
Kwakweli hili limetuumiza sana wananchi.....na Leo MBUMBUMBU wakishinda, moyo UTARARUKA vibaya sana.
Mimi leo ninaiombea Simba ifunge magoli mengi ili iwe ni funzo zaidi kwetu Yanga. Itakavyozidi kutuuma ndio tutazidi kujifunza.
 
Kijana sikuonagi kwenye jukwaa la chelsea
 
Tulitegemea kuwa na msimu mzuri sana kwenye CL mwaka huu ila viongozi wameuharibu kwa sababu wanazozijua wao.
Mkuu viongozi wetu walilewa sifa kiasi waliamini wao ni kama malaika, mwisho wa siku ndio haya.
Ni kama kijana umsifu mbio mwisho wa siku apitilize kwao.

Hii dhambi Eng.Hers na genge lake hawawezi iepuka.

Jana nimeiona Yanga ikicheza kama kuku alie katwa kichwa.

Binafs sintoangalia mechi yeyote ya Yanga mpaka msimu ujao.
 
Itoshe kusema wana utopolo wenzangu Germany machine tumesajili gobole
Hamna kocha mule, ndio maana hata huko alikotoka (Tx galax) pia kaacha majanga.

Kocha ndio mala yake ya kwanza kufundisha club bingwa, yani ni sawa umpe kichwa chako kinyozi anae jifunza.

Hivi Eng.Hers aliwaza nini hapa?

Nashauri kabla hajaachia uongozi wa timu yetu, inatakiwa achapwe viboko vingi sana, ili iwe fundisho kwa atakae kuja kukaimu nafasi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…