Kiukweli kabisa hii wala sio timu yetu. Timu yetu ameondoka nayo Gamondi

Kiukweli kabisa hii wala sio timu yetu. Timu yetu ameondoka nayo Gamondi

IMG-20241103-WA0066.jpg
 
Kumfuta Gamond ilikuwa kosa kubwa sana ambalo viongozi wetu walifanya, huyu mandevu hawajui wachezaji wala haelewi wanahitaji mfumo gan kuendana na vipaji vyao!
Hili kosa tulifanya chelsea kwa kuweka makocha wasioendana na characteristics za wachezaji kosa hili naliona kwa yanga, msimu huu hata kombe la mbuz hatuchukui kummmkkkk🚮
 
Kuna mpira wa kushambulia na kukaba kitimu alifundisha Nabi ukatupa mafanikio, Gamondi akasafiria hiyo nyota na ikafikia tamati timu ikapoteza ule mpira na kuanza kufungwa akasepa , akaja Ramovich timu ikiwa kwenye downfall. Hana baya, Ramovich atafute kilichoishusha Yanga arekebishe.

Ramovich awape nafasi wachezaji wote asikariri, mf jana Max hakuwa mchezoni alipoteza mipira mingi pasi mkaa na faulo ya goli la kwanza alisababisha yeye Max kwa kumsukuma mwarabu kipumbavu bila umuhimu wowote mpira ushaenda ye anasukuma mtu na hakutolewa. Mudathir pia alikosa umakini kabisa papara kibao kama anafukuzwa pasi zote mkaa na Abuya hivyo hivyo.

Timu ilimkosa Aucho ikakosa balance na kushindwa kumiliki mpira juu ya msitari wa kati. Pasi mbili tu mpira umepotea, timu ilikosa mbinu za kupasua ngome ya MC Alger katikati. Timu haikucheza kitimu kila mchezaji kivyake! Wachezaji hawakuwa faster kila mara walichelewa kwenye matukio na kucheza rafu zilizoigharimu timu.

Kocha Ramovich apewe muda kuijenga upya Yanga iliyoporomoka ila mwaka huu club bingwa si fungu letu, tuko mkiani tunapostahili.

Jana nilijua Yanga itafungwa nikaongea kwenye kahawa wenye akili walielewa sababu binafsi naamini ile Yanga yetu haijarudi sisi ni timu kubwa si wa kukaa nyuma kusubiri, sisi si wa kuwa timu ya pili uwanjani , jana ilikuwa ni suala la muda tu kufungwa, ukijilinda sana lazima utachoka, huo si mpira wetu, njoo nasisi tunakuja.

Ramovich aambiwe akiamua kujilinda aweke mabeki watatu wa kati (Nondo, Job na Baka), beki line inakuwa na wachezaji watano na acheze Mkude si Abuya, si kama alivyofanya Ramovich jana.
 
Back
Top Bottom