Kiukweli kuna baadhi ya watu mavazi fulani au sare fulani zinawapendeza na wanatokelezea. Shuhudia wanavyopendeza!

nilimlaumu aliposema wewe ni mtu wa njaa ila kadri muda unavyoenda nathibitisha maneno yake, pasco wa leo sio pasco wa zamani mwenye kuandika vitu vyenye akili na kufikilisha umebakia kuwa chawa mkongwe
 
Mkuu Pascal nimekufahamu 2016 nikaanza kukufuatilia kwa undani sn, mbona mwanzo ulikuwa unaleta hoja nzito hapa unachambua mpaka sisi vilaza tunapata maarifa? ni kweli JF ni user generated forum lakini kwa mtu ambaye ulijijengea heshima kubwa kama wewe kwa hoja zenye mashiko tunashangaa sn kuona unazidi kupotea, utumbo kama huu ungeandikwa na johnthebaptist hakuna mtu angeshangaa. Bashiru, Polepole sijui Kabudi nani leo anaweza kuwasilikiza au Dr Rioba hawana issue tena sababu jamii ilikuwa inawaheshimu sn lakini baada ya kuisaliti jamii wanaonekana ni watu wa hovyo sn. Wewe tuna kulalamikia sababu ya background yako nzuri kabla ya kuingia tamaa.
 
Paschal jiulize mbona mwanzo hapa jukwaani ulikuwa una heshimika sn na kila mtu siyo CCM wala CDM? Kaa utafakari brother kuna kitu hakipo sawa.
 
Mkuu Tate Mkuu , please don't!. Sisi sio tumekuwa baridi kwa kutaka ni umri ndio umetutupa mkono. Sasa tunageuka waalimu kufundisha vijana.
JF ni very addictive, hata mimi niliaga

Lakini mpaka leo nipo!.
Ukiamua kuondoka, then ondoka kimya kimya, usiage utashindwa!.
P
 
Dada angu mbona unawashwa sn?
 
Daaa Natamani hawa wanaokutukana nao wangeelewa ulichoandika kama Mimi. Anyways, we mzee akiri kubwa na uzuri umetanguliza angalizo kuwa not for average minds.
 
Inasikitisha sana, Waandishi wa habari nguli tunaotegemea waongelee mambo yanayoigusa jamii wanashindwa kuyaongea na baadala yake wanaongelea mavazi ya watawala.
 
Angalizo la uchangiaji: Kuna watu humu wana vijiba vya roho, akitokea mtu akapendeza wao wanakereka au akisifiwa wao wanakereka na kukasirika. Kama wewe ni mmoja wa kundi hili, nakuomba ushia hapa ili huko mbele usikereke.
JPM ni kweli zimempendeza kwa sababu umbo lake linamruhusu...

Halafu sijui kwanini huwa naamini moja ya mambo ambayo huenda JPM alijilaumu, ni kwanini hakujiunga na jeshi...

I believe, lau kama saa ingerejeshwa nyuma hadi wakati anamaliza Kidato cha VI na kuambiwa would you like kuendelea na taaluma yako ile ile ya ualimu au ungependa kubadili, I guess angebadili na kuamua kuingia JWTZ!

Halafu sijui kwanini nahisi hapo Mwalimu kapekua pekua kutafuta gwanda, hakuziona kwa sababu hakuwa nazo, na hivyo akaamua kuchukua gwanda kama sio za Andrew basi zitakuwa za Makongoro!!

Au hizo gwanda alizopiga Mwalimu zilikuwa ni maalumu kwa wale wenye presidential status peke yake?!

Au wakati huo Makongoro au Andrew walikuwa bado hawajajiunga na jeshi?!
 
Mkuu Pasco, kwa jicho la tatu naona kama umempiga jungu chifu wa machifuπŸ’
Mzee nawe ni great thinker. πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™ na Great Thinker ndo watamuelewa huyu mzee kwenye huu uzi. Anapiga mawe kinyume nyumeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu Tony Laurent , kwanza naheshimu mawazo yako kuwa mimi ni mfano mbaya kwa jamii. Human beings are different, we can't all be the same, we can't all be like Jenerali, Jenerali ni Jenerali hivyo ndivyo Jenerali alivyo na Pasco Mayalla ni Pasco Mayalla hivi ndivyo Pasco Mayalla alivyo. Kwa vile Jenerali is good on his ways, kama Pasco Mayalla anao uwezo huo kama wa Jenerali, then kumshauri Pasco Mayalla awe kama Jenerali is fine, lakini kama Pasco Mayalla hana huo uwezo hata nusu ya Jenerali, kumtaka awe kama Jenerali, ni kumuonea bure!. Naombeni msinionee!.

As a retired now, kiukweli kati ya vitu ambavyo I do best ni kucheza na wajukuu.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…