Kiukweli kuna baadhi ya watu mavazi fulani au sare fulani zinawapendeza na wanatokelezea. Shuhudia wanavyopendeza!

Kiukweli kuna baadhi ya watu mavazi fulani au sare fulani zinawapendeza na wanatokelezea. Shuhudia wanavyopendeza!

Wanabodi,

Angalizo la uchangiaji: Kuna watu humu wana vijiba vya roho, akitokea mtu akapendeza wao wanakereka au akisifiwa wao wanakereka na kukasirika. Kama wewe ni mmoja wa kundi hili, nakuomba ushia hapa ili huko mbele usikereke.

Kufuatia mimi mwana jf mwenzenu umri wangu umesonga songa, nimefikia level ya kustaafu, hivyo nakuwa sina tena zile mada moto moto au maswali magumu magumu kama enzi zile kijana nikiendesha kipindi cha Kiti Moto.

Kufuatia neno "ukubwa dawa", mimi sasa ni mtu mzima hivyo napandisha mabandiko ya dawa kama bandiko hili.

Declaration of Understanding. Naomba kukiri, naaandikia kwa members wenye uwezo tofauti tofauti wa uelewa, hivyo ukikutana na bandiko langu ukajiona kama huelewi elewi, nakushauri jipitie zako tuu uendelee na safari yako, maana mabandiko mengine, nawaandikia watoto wa chekechea, wewe wa Ph.D utaishia chaka.

Leo naomba kutoa somo kuhusu mavazi fulani fulani, jee wajua mavazi yanazungumza?. Jee wajua dress code ni kiashiria cha the state of mind ya mvaaji na action anayoweza kufanya?.


Mfano mtu akikukaribisha kwake ukaenda the way utakavyomkuta amevaa utajua amekuitia nini na ni nini kitafuatia.

Wenzetu wazungu wana dress code kabisa ya matukio mbalimbali, kwa matukio serious wana vaa formal dress, yaani kuiambia, na kwa matukio ya kawaida, wanavaa kawaida, yaani casual but smart, sisi wabongo hatuna any specific dress code kwa matukio serious na yale ya kawaida.

Pia aina ya mavazi ni kwa maeneo au matukio fulani, mfano ukienda beach, unavaa beach wear, ukienda church unavaa vazi la heshima na ukitoka out kama ni first date out, usually wadada they dress to kill!.

Leo nimemuona Mama kavaa Combat, kwa jinsi hiyo combat ilivyo mkaa, imemtoa kweli kweli na kumpendezea, hivyo Mama ametokelezea.

Kwa sisi wenye jicho la tatu, hiyo combat ya mama inaongea, only wenye jicho la tatu ndio wanaona, na wenye sikio la tatu ndio wanaweza kusikia hiyo dress code inaongea nini.
View attachment 2011474
Kwa vile macho hayafanani, na kwa vile hakuna taarifa zozote za mama kuwa mjeshi kabla, hivyo wale wenye macho ya kawaida tuu, wakiona hii picha ya amevaa combat, wao wanaona ni mtu tuu wa kawaida yule yule Mama Samia waliyemzoe ila tuu leo amebadilika kwa kuvaa sare za jeshi, lakini sisi wenye jicho la tatu, hatuoni sare tuu tunamuona mtu ambaye ni mjeshi kweli kabisa, ndani ya sare yake, ila kabla ya kuvaa sare za jeshi, hatukumjua, kuwa ni mjeshi mpaka alipovaa sare ya jeshi, kwa jinsi zilivyo mkaa, ndipo macho yetu yamefunguka, kuona na kubaini kumbe ni mjeshi kabisa!.

Zingatia tofauti kati ya mtu asiye mjeshi by nature na kuvaa sare za jeshi na mtu mjeshi by nature na kuvaa sare za jeshi. Asiye mjeshi by nature,
View attachment 2011725
kama huyu, akivaa sare za jeshi anakuwa amevaa tuu sare,
Lakini mtu mjeshi by nature, hata kama sio mwanajeshi, akivaa sare za jeshi, anakuwa ni mwake mwake!, huyu ni jeshi kama huyu
View attachment 2011739

Hata huyu Mzee wetu
3001226_nYERERE_COMBAT.jpeg

Mwalimu Nyerere, alikuwa mjeshi.
View attachment 2011753
Naomba kutoa onyo kwa wale wenzangu na mimi waliozoea, rais ikitokea upande ule, wa ma ustaadhi, basi wanajiachia na kupanga kufanya au kuleta ile michezo michezo yao!. Kama hata baada ya kusoma hapa na kumjua ni mjeshi na kama wanaweza kumletea mchezomchezo mjeshi...endeleeni ila msilalamike kuwa hamkujua, au hamkuambiwa, mlidhani ni sare tuu za jeshi! hii ni taarifa kwenu kuwa sio sare tuu!, msithubutu, na mkithubutu, shauri yenu!. Mimi mwenzenu Paskali Mayalla, japo wengi humu mnanifahamu kama mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea, wengi humu wasicho kijua kuhusu mimi, kabla ya uandishi wa habari nilikuwa mjeda from JKT straight to JWTZ!. Chezea vitu vingine vyote ila geshi, usichezee kabisa!. Chezea watu wengine wote, ila Wajeda usichezee kabisa. Kazi ya jeshi ni moja tuu... "zikimkosa mbili...utaandika maelezo"!.

Kwa wale wenzangu na mimi wasio na uwezo wa kuisikia sauti ya mavazi fulani, this is a very loud and clear signál she is a very serious person, she is no nonsense lady, sio mtu wa kuletea mchezo mchezo, hivyo huu ni ujumbe mzito loud and clear kwa wote wanaopanga kuleta au kufanya mambo yao ya ile michezo michezo yao ya ajabu ajabu, before they do, they better think twice, and if possible waache kabisa!. kama hapo mwanzo iliyokuwa "hapa kazi tuu" naona sasa kuna relaxation mood na laxity ya watu ku relax na kuanza kuleta tena ile michezo michezo..., hii dress code ya leo inaniambia ile slogan ya "hapa kazi tuu", inaendelea kwa "kazi iendelee".

Paskali

View attachment 2011746
Pascal hujachoka tu!!
Jitahidi huenda ikawa sawa na nia yako.
Watu wanajadiri mambo muhimu yahusuyo usitawi wa nchi,dhulma za haki za watu wewe unakuja kusifia mtu kupendeza kuvaa sare za jeshi?

Mdogo wangu umefilika kabisa.
Hivi mayalla umefikia mahali hata familia unashindwa kuipatia mkate wa kila Siku?
MAANA UNAJIPENDEKEZA KITOTO SANA.

NIKUPE MAARIFA
Njia unayotumia ni ndefu sana na yawezekana hao wakuu wa uteuzi hawaioni au wameichoka.
NENDA KAONANE NAE USO KWA USO MWELEZE TAKWA LAKO.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Pakawa , kuna kitu kinaitwa kutazama kitu kwa different perspectives, wengi uwezo wenu ni kuona sare tuu za jeshi, sisi wenye eyes to details jicho letu linaona beyond mavazi, hivyo unapoleta hoja zinazohitaji wenye uwezo to read in between the lines, na wengi humu ni vilaza tuu, then vilaza hawa watatoka kapa na ndio kama hivi kuambiwa hili ni bandiko la utoto!. Look beyond mavazi, mavazi yanazungumza, lazima uwe na jicho la kuona visivyo onekana na sikio la kusikia visivyo tamkwa. Jee wewe Mkuu Pakawa by your look na michango yako humu, unaonekana sio kilaza, how can you miss the point usijue nazungumzia nini kwenye bandiko hili?.
P
Huna jipya zaidi ya kukazimusha uteuzi na kaa ukijua kuwa hutapata uteuzi hata wa nyumba 10
 
When Pasco is reduced to discuss costume, outfits and gear,know that there is a big problem within himself
Mkuu Missile of the Nation , in life kuna political issues, economical issues na social issues, costumes is a social issue. Hizi discussion za costumes sikuzianza leo, ila it's not about costumes only, there is more than just costumes, ila kama hauna jicho la kuona hayo, huwezi kuona na kuishia kuona costumes only!.



P.
 
Ebu twambie ni mambo gani hayo ambayo wewe unayaona kuwa wameyafanya na Mkapa na Kikwete hawakufanya

JK alikuwa mpenzi wa siasa jeshini akiwa na mwenzake Kinana wenzake hawakuwa na hayo mambo.

JK alitanguliza diplomasia sana kuliko wengine wote, alipendelea na aliiendekeza diplomacy mpaka kwenye maamuzi tofauti na mkapa na JPM.

Mkapa roho yake ilikuwa kwenye thamani ya TSH na taasisi ya kukusanya kodi wengine walijikita kwenye miundo mbinu(JPM) na diplomasia(JK)

Utendaji wa maraisi umetofautiana sana hatutamaliza mambo ni mengi hatutayamaliza.
 
JK alikuwa mpenzi wa siasa jeshini akiwa na mwenzake Kinana wenzake hawakuwa na hayo mambo.

JK alitanguliza diplomasia sana kuliko wengine wote, alipendelea na aliiendekeza diplomacy mpaka kwenye maamuzi tofauti na mkapa na JPM.

Mkapa roho yake ilikuwa kwenye thamani ya TSH na taasisi ya kukusanya kodi wengine walijikita kwenye miundo mbinu(JPM) na diplomasia(JK)

Utendaji wa maraisi umetofautiana sana hatutamaliza mambo ni mengi hatutayamaliza.
Awamu ya 5 hakuna cha kujibunia maana miradi yote ilikuwa ya Kikwete
 
Mkuu Pascal nimekufahamu 2016 nikaanza kukufuatilia kwa undani sn, mbona mwanzo ulikuwa unaleta hoja nzito hapa unachambua mpaka sisi vilaza tunapata maarifa? ni kweli JF ni user generated forum lakini kwa mtu ambaye ulijijengea heshima kubwa kama wewe kwa hoja zenye mashiko tunashangaa sn kuona unazidi kupotea, utumbo kama huu ungeandikwa na johnthebaptist hakuna mtu angeshangaa. Bashiru, Polepole sijui Kabudi nani leo anaweza kuwasilikiza au Dr Rioba hawana issue tena sababu jamii ilikuwa inawaheshimu sn lakini baada ya kuisaliti jamii wanaonekana ni watu wa hovyo sn. Wewe tuna kulalamikia sababu ya background yako nzuri kabla ya kuingia tamaa.
Mkuu Babati , kiukweli kuna michango mingine inakugusa hadi inakuumiza kwasababu ina ukweli mkubwa ambao unauma hivyo unaumia ila ndio ukweli wenyewe.

Human beings are not static, they are dynamic and hence, they changes with time, as days go by, the young and energetic people changes into old age and always try to fit and live in a certain lifestyle, while life also changes, with time, and place, hivyo if you can't change and adapt to the changing environment, then you just perish.

Naomba ni reserves mwingine ila kiukweli nimeguswa na jinsi nilivyo kuwa highly regarded humu jf na jinsi sasa ninavyo dharauliwa humu, hivyo na mimi nimebaini jf ina vilaza wengi kuliko tunavyotegemea, wao wanaona hili ni bandiko la mavazi tuu, hadi kuliita "utumbo".

Najitafakari
P
 
Back
Top Bottom