Kiukweli mambo yanaenda kasi sana, Dar bila Makonda wananchi wameshazoea CHADEMA mwendo mdundo

hapo ndio ujue maendeleo yana vyama
 
naona unamtafuta Makonda kwa nguvu - utampata tu ni suala la muda.
 

Mary Chips😄😄..... mama aliinyoosha Dar huyu

Ila unewasahau

Mustapha Songambele,John Mhavile,Ditopile Mzuzuri na Christopher Lihundi
 
Hivi Makonda ndio alipiga marufuku mikutano ya kisiasa nchi nzima?

Japo simkubali Makonda,lakini katika hili,tusimsingizie kwani alikuwa anasimamia utekelezaji wa maagizo kutoka juu.

Unasahau mapema hivi? Au ni unafiki umekushika mkono?? Unasahau habari ya kuwarudisha wahuni Dodoma na kuwa mkoa wa dar es salaam sio wa wazururaji na kuwa atawapeleka Dodoma kwa nguvu wakahudhurie bunge??

DAB alitoa matamko mengi ya kiutawala kulenga taasisi za kiraia - rejea kuhusu sababu za “kuwanyima wenzake haki ya kuishi na kufanya siasa” - Ubalozi wa Marekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…