..Wamaasai hawakutoa taarifa kwa Polisi kuwa wataandamana na Polisi wakawa wamejizatiti eneo la tukio wakiwasubiri wawauwe.
..Maandamano au mgomo hufanikiwa au kufeli kwa kuzingatia upande upi utamuwahi mwenzake kufika eneo la tukio.
..Wamaasai walifika eneo la tukio kabla ya Polisi,matokeo yake Polisi wakasalimu amri.
..Chadema siku ya kumpokea Lissu walifika uwanja wa ndege kwa wingi kabla Polisi hawaja-secure eneo hilo.
..Matokeo yake Polisi wakasalimu amri , na mapokezi ya Lissu yakafunga barabara kwa maandamano toka uwanja wa ndege mpaka Kinondoni Ufipa.
..Kilichotokea ni ELIMU tosha kwa Chadema, vyama vya upinzani, na wanaharakati, kuhusu namna bora ya kuandaa maandamano.
..Bila ELEMENT OF SURPRISE dhidi ya vyombo vya dola hakuna maandamano ya kushinikiza serikali yatafanikiwa.