Kiundwe chombo huru cha kusimamia Jeshi la Polisi

Kiundwe chombo huru cha kusimamia Jeshi la Polisi

Polisi Tanzania limekuwa jeshi ambalo linaweza kubambika kesi kwa yeyote wamtakae na lisihojiwe na chombo chochote.

Wameenda mbali wanaua mtu yeyote hasa wafanyabishara endapo wataona ana mali za kumpora,wanamuua na wanamtupa na kuchukua mali zake kwa jeuri kabisa wakijua kabisa kwamba hakuna chombo kingine kinachoweza kupepeleleza jinai zaidi yao.

Polisi Tanzania ni janga kuu,serikali unda chombo kipya kilisimamie jeshi la polisi,hawawezi tena kujisimamia ,wamegeuka laana kwa nchi

Serikali fanyeni haraka tuokoe wananchi dhidi ya wapumbavu hawa!!! Kama mishahara midogo waongezeni.
Kama mtu anapobambikiwa kesi na kucheleweshwa kupelekwa mahakamani ama mtu kupigwa na kufia kituo cha polisi ama inapotukia mtu kurushiana risasi na polisi ni nani wakuchunguza na kusema jeshi lipo sahii au limekosea jinsi gani raia anaweza kujiponya kwenye uonevu kama huo
 
Nimejikuta naingiwa na hili wazo ghafula.
Kutokana na matukio yanayoendelea hivi sasa, kama kweli tunataka nchi yetu ipone, hawa polisi wangechunguzwa na wanajeshi.

Na kama wakibainika hukumu zao zipelekwe jeshini, hata kule kuna jela maalumu jamani.

Tena jela za kule watu wanachapika na msosi wanapewa. Ukishiba tu unachapika tena mpaka msosi wote uishe.

Hata hawa polisi wala rushwa, wangekua wanapelekwa kupigwa nua huko.

Kama kuna mwenye nyongeza labda uwanja ni wako.
 
Nyongeza nyingine ni kwamba Meneja Wa Makampuni hapaswi kuzungumzia masuala ya kiusalama kwa vile yeye hana ujuzi huo. Just endelea tu na umeneja wa kampuni yako ya kuzalisha Hill Water, tupate afya.
 
Waache wafanye kazi zinazowahusu!Watawezaje kufanya kitu ambacho hawana taaluma nacho!
 
wanajeshi juzi wamemnywesha mzee wa watu cement iliyochanganywa na maji
 
Nimejikuta naingiwa na hili wazo ghafula.
Kutokana na matukio yanayoendelea hivi sasa, kama kweli tunataka nchi yetu ipone, hawa polisi wangechunguzwa na wanajeshi...
Hawawez hukumiwa jeshini. Hizo ni taasis mbili tofauti zenye sheria tofauti.

Polis wenyewe wana mahaka zao za kiaskari hawaingiliani na jeshi la wananchi.
 
Nimejikuta naingiwa na hili wazo ghafula.
Kutokana na matukio yanayoendelea hivi sasa, kama kweli tunataka nchi yetu ipone, hawa polisi wangechunguzwa na wanajeshi...
Nasikia nao kuna mswada wamepeleka bungeni eti wasiwe wanashitakiwa wakikiuka sheria kwenye uchunguzi
 
Wanajeshi wenyewe wameng'atishwa gunzi la muhindi mdomoni wanaacha tu wahuni watuharibie nchi yetu.

Wahuni wanawalipa wanafiki mshahara mdogo ili wawatie hofu raia. Hapa utaona wanafiki wanaogopa kupoteza kazi zao kwasababu njia za kwenda chooni zitaota majani wakipoteza kazi zao. Kamwe wahuni katika nchi hii hawatapandisha mishahara ili wanafiki wasiache kwatetemekea kwasababu ya kuwa na vihela.

Hii chain ya wahuni---->wanafiki---->wenye hofu ni hatari sana na hapa utaona wanafiki wanatumika kama catalyst.

Wanafiki ni wale walio kabidhiwa silaha za moto na vyombo vingine vya dola.
 
We hujui hao ni taasisi mbili tofauti?unajua maovu ya jeshini au unasema tu kwasababu polisi wanakutana na raia moja kwa moja katika utekelezaji wao wa majukumu?

Unadhani polisi wakifutwa nchini na majukumu yao yakafanywa na hao unaosema wanajeshi,wananchi hawatalalamika? Usisifu au kutaka kitu kwasababu hukijui kiundani.

Wewe ni mmoja wa watu ambao mnaamini kua mwanajeshi anapiga Kijiji au mji mzima peke yake,unasahau akina Adamoo waliteswa na polisi na wakalia huku wakiwa wamepitia mafunzo hadi ya ukomando.

Hujui mengi wewe, tulia.
 
We hujui hao ni taasisi mbili tofauti?unajua maovu ya jeshini au unasema tu kwasababu polisi wanakutana na raia moja kwa moja katika utekelezaji wao wa majukumu?...
Wewe utakua ni polisi lazima mkuu. Ni kichapo cha jeshini unakielewa vizuri ndio maana unatolea maelezo mengi hivi. Sasa ulitaka polisi wachunguzwe na mbunge au.
 
Wewe utakua ni polisi lazima mkuu. Ni kichapo cha jeshini unakielewa vizuri ndio maana unatolea maelezo mengi hivi. Sasa ulitaka polisi wachunguzwe na mbunge au.
Umeambiwa ni idara tofauti,polisi ana mafunzo yake,huyo mwingine anayo mafunzo yake.
 
Naona waziri wa mambo ya ndani amekiri uozo ndani ya jeshi la polisi. Kwa mantiki hii ipo haja ya kuundwa kikosi kazi maalumu ili waliodhulumiwa haki zao kwa kuteswa, kuuliwa au hata kubambikiwa kesi wapate haki zao za msingi.
Screenshot_20220212-213821.jpg
 
Hivyo vikosi kazi sio vya kuundwa ndo vinakuwa vikosi vya waalifu, vinageuka na kuwa vikosi vya waalifu
 
Siku hizi hakuna maswala ya tume. Ni mwendo wa kukusanya ushahidi na kifunguliwa kesi moja kwa moja. Mama akitoka Ubelgiji atakuwa na nondo kutoka kwa yule mnayemwita mkimbizi na hapo ndo 🚔 watajua hawakujua.
 
Back
Top Bottom