Mimi naamini mambo anayoyafanya Trump ndio mambo ambayo the Americans wants, hiyo impeachment ni just wapinzani tuu wa kazi nzuri ya Trump kwasababu kuna mambo makubwa mabaya yamefanywa na marais wa Marekani waliostahili sio tuu impeachment bali walipaswa wapelekwe na Hague!.
The Iraq war, wakamsingizia Saddam ana WMD, wakamtoa wakamnyonga!. Angalia sasa Iraq!.
Wakamvaa Quadafi kwa kosa la kuhamasisha muungano wa Africa, tuunde taifa moja kubwa lenye nguvu kama USA, ndilo bara lenye rasilimali nyingi kuliko bara lolote, Africa is the richest continent, hivyo tusinge hitaji IMF wala WB, na UN tungekuwa na kura ya Veto!. Wakamshughulikia!.
Angalia walichofanya Afghanistan?. Angalia ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadam uliofanywa katika gereza la Guantanamo!.
All these ni mambo yaliwahitaji marais wa Marekani wafikishwe the Hague, but this is what the Americans wants, kadri rais wao anapokuwa mbabe mbabe, ndivyo the American people wanavyozidi kumpenda na kumuona ni hero, hayo mambo ya impeachment ni politics tuu za Democrats na ni upepo tuu ambao utapita.
Ni kama mambo anayoyafanya Magufuli wetu, anakanyaga katiba, anaminya demokrasia kiaina, freedom of speech, freedom of expression, freedom of association, freedom of movement, freedom of the press, some civil
rights na political rights, mashakani, sasa ndio tunaelekea 2020 October na kuirejesha Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja, kikatiba, kisheria, kikanuni na kiutaratibu, ilipaswa Magufuli awe amewekwa pembeni tangu pale alipozuia mikutano ya siasa, kitu ambacho katiba imeruhusu, rais wetu ameapa kuilinda, halafu amepata wapi mamlaka ya kuja kuikiuka?.
Jee umewahi kusikia mtu yoyote, chama chochote au taasisi yoyote ikipinga rasmi haya Magufuli anayoyafanya?. Ukiondoa hizi kelele tuu za hapa na pale, hakuna yoyote anayepinga lolote la rais Magufuli, kwasababu haya anayoyafanya rais Magufuli, ndio Watanzania tunayoyataka, Watanzania wanataka maendeleo, rais Magufuli analeta maendeleo, hata kama some of the expenses za maendeleo hayo ni pamoja na pyu pyu 16 kwa wasaliti wa kasi yake, au kupotea kwa vimbelembele wa kuusema ukweli kama Azory Gwanda au wafukunyuku kama Ben Saanane, miili ya watu kuokotwa kwenye viroba, simu za watu kudukuliwa na voice notes kutupwa public, etc etc, if that is the price of the development Tanzanians wants, we will pay that price, and in fact we are now paying that, vile vipengele vya Ibara ya 46 kwenye katiba yetu, viliwekwa kuwafurahisha tuu wafadhili, kama tunavyofanya maigizo ya chaguzi za kidemokrasia kama huu wa juzi wa serikali za mitaa, na funga kazi ni 2020!.
If anachofanya Trump ni what the American's people wants nashauri the wishes of the people ziheshimiwe, hizo impeachment proceedings ni just wastage of time money and resources
P