Kiutaniutani Trump anaondoka White House

Trump hata Kama asipogombea mwakani hakuna atakachokipoteza, Kama ni sifa ameshajijengea tayari na rekodi keshaiweka maishani mwake kuwa aliwahi kuwa Rais wa taifa kubwa Kama Marekani.
 
P hata leo umenilet down. uliyoandika ni ya mwana kijiji. waachie wao. naona unazidi kuweka taaluma yako ya sheria pembeni. na pengine ni kweli wewe si mwanasheria, ulisomea sheria. academic! mwanasheria anashindia, anawaza, akilala anaota sheria. oxygen yake ni sheria. mitazamo yake ni kisheriasheria hadi kero. kuvaa, kutembea, taja chochote au lolote kwake sheria tu.
marekani sio tanzania, ukishtakiwa upelelezi umekamilika. mashtaka tumeyaona wote. kwa mwanasheria yana maana kubwa. hatuendi kwenye uchaguzi bali impeachment. huko sio popular vote na ambayo ilimkataa trump save electoral college.sijui kama zile kura milioni tatu kazipunguza au zimezidi na kuwa milioni tano! tuhuma nzito.ushahidi ukoje? nusanusa kama mwanasheria na si mwanakijiji. mimi na wengi tulitaka kuona jibu la hilo kutoka kwako. mapenzi yako sawa unayo na kwa nani potelea pote. anafanya nini, anapendwa vipi na mengine kibao ya uzuri wake hashtakiwi kwayo. P tenda haki jikite kwenye tuhuma na ushahidi uliopo.
 
Anawajibishwa kwa[emoji117][emoji117][emoji117]
1.Kutumia mamlaka vibaya (abuse of power)

2.Kuingilia Uhuru na mamlaka ya bunge //Congress obstruction.

[emoji115][emoji115]this will never happen in Africa superbug,
S/Africa hio wanaweza kuifanya bila shida.
 
Tatizo ni moja tu,Saudi Arabia ndio walishambulia ,marekani wakaenda kupiga afaghnistan na Iraq,
Kwanini?,....kwasababu Hilo shambulizi lilipangwa na rais Bush alijua kabla nini kitatokea
 
Umejitahidi kuandika lkn wenzetu wanajali democrasya hawajali matumbo yao na wanatofautisha sana bunge na mahakama zisiingiliwe na muhimili mwengine kwani watajua kama mbele italeta athari lkn huku kwetu Africa bunge limeingiliwa na mahakama ndiyo kabisa wengine wanamsifia MTU ambae katiba kaitia mfukoni
 
Trump hawezi kuondolewa. Kinachoganyika ni kumnyanyasa na kumkejeli. Hata wanaosema wanaanzisha mchakato wa kumwondoa wanajua kabisa hawatamwondoa.
Wenzetu wanajielewa hawaendeshwi kwa kumsifia mtu na wala hawataki matamshi ya kumwambia spika ww washuhulikie ndani ya bunge wakitoka njee nitawashuhulikia mm njee ya bunge
 
Humu kuna wamarekani wengi sana!

Mwingine anaishi kule kwenye mashimo ya rejects waliotelekezwa na jamii, naye anajua mustakabali wa Trump kwa vile tu yuko Marekani!

Mwingine naye aliajiriwa na CCM kuwa mpiga propaganda (wenyewe wanajiita usalama wa Taifa), na yeye pia anajua mambo yote ya siasa za Marekani kutokana na "ujasusi" wake nguli.

The bottom line ni kwamba, ninyi ni waswahili tu. Hamjui lolote wala hamna upeo wa ku comprehend levels za civilization za watu weupe katika dunia ya kwanza.

Mjikite tu kupiga porojo uchwara kuhusu madikteta uchwara wa humu Tanganyika!

Nje na hapo, ufahamu wenu ni kiduchu mno!
 
Haya kaka
 
Mkuu Bungua, kwa vile huma jf tunajuana, japo sina uhakika kwa sababu hakuna research yoyote ambayo imefanyika kuthibitisha hili, lakini naamini, hakuna mwana jf, ambaye amelipigia kelele hili la udikiteta wa Magufuli, kama mimi.
Matakwa ya katiba, sheria, taratibu na kanuni ni jambo moja, na matakwa ya Wananchi, wanataka nini ni jambo jingine.
Kuna kitu kinaitwa, "is" and "ought". Is ni kile kinachofanyika sasa, ought ni kile kilichopaswa kufanywa na kufanyika.
Magufuli tumemchagua kwa mujibu wa katiba na akaapa kuilinda katiba, lakini katika kutimiza maendeleo anayoyataka, akajikuta akiifuata katiba, itamchelewesha, hivyo akaamua kuikanyaga katiba ili kuwaletea Watanzania Maendeleo.
Kama wananchi wanachotaka ni maendeleo, na hata kama maendeleo hayo yatapatikana kwa udikiteta, then Magufuli is their hero.

Karibu baadhi ya mada zangu za udikiteta
  1. Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
  2. Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi ...
  3. Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
  4. Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali ...
  5. Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade ...
  6. Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio ...
  7. Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
  8. Fungia Fungia Magazeti: Ni Udikiteta wa Serikali Magufuli ...
  9. Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia ...
  10. UDIKTETA: Hongera Sana TWAWEZA, TZ hakuna Udikteta! Ila ...
  11. Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni ...
  12. Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
  13. Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili ...
  14. Zitto Kabwe na wapinzani wote, kwanini mnapiga tu kelele kuhusu ...
  15. Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
  16. CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue ...
  17. Timua Timua CCM, Hongera M/Kiti Magufuli, Wapinzani Mjifunze ...
  18. Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
  19. Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni ...
  20. Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
P
https://www.jamiiforums.com/threads...t-it-a-nuisance-je-2020-ni-ccm-pekee.1635309/
 
Mkuu.

Hivi nchi ya kidemokrasia inapoamua kwenda vitani. Ni kwa maagizo ya kutoka mamlaka ipi?..

Sababu vita vinagharimu uchumi wa nchi na maisha ya watu tena wengi ni wasio na hatia.

Tafadhali.
 
Niliwahi sikia mahala kua kosa kubwa lililofanya jamaa achukiwe kwanza na kupinga vikali issue za ushoga na mapenzi ya jinsia moja pili ku cancel pesa zote za serikali zilizokua zinaenda kwenye masuala ya abortion wao wanaita haki za binadamu
Ndio maana wanamfanyia visa juu chini atoke
 
ahsante kwa yote. mwandishi mzuri kwa mambo popular. mwanahabari habari wa kawaida. kwa leo mada ni impeachment ya trump. swali ni wastage of time and money, really? na kama ni hivyo kwetu ndio kabisa wasithubu! hata hizo kelele zao waache kabisa. wasubiri wakiwa tayari kufa waingie mtaani kupinga udikteta. rais wa wanyonge hatangoja wamwage damu, wakikojoa tu wameisha. rais anaumia kutawala wafungwa na mahabusu. magereza na mahabusi zimejaa kwa maelekezo kutoka juu kwa rais huyohuyo kipenzi cha watu.
mahakama ya hakimu mkazi wana usongo na ujaji, bwana. anayetaka haki akate rufaa. funga mpinzani upate ujaji. mahakama kuu wanataka ujaji wa mahakama ya rufani. hukumu ya matupa kiboko yafaa awe jaji kiongozi au apande mahakama ya rufani. juzi mahakama kuu ikakataa wakurugenzi kusimamia uchaguzi. jana mahakama ya rufani wakasema ruhusa kusimamia. mahakama ipi upeleke kesi yako?
"is" waachie wao mbona wengi tu. impeachment inataka kutoa "is" na kuweka "ought" na wewe je?
 
Huwa nalikumbuka swali lako tu ulilomuuliza mkulu dah niswali bora la muda woote mayalla njaaa
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Trump amenyanyua sana uchumi wa Marekani, hakuna wakumtoa, ndio rais anaeongoza kwa kutengeneza ajira nyingi, hizo nyingine ni propaganda tu za vyombo vya habari
Acha uongo trend ilianza kipindi cha mwisho cha Obama, kama alinyanyua uchumi wa marekani republican wasingepoteza majority kwenye house of representative kipindi cha mid tearm election
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…