Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Ni lazima nikiri wazi kabisa, mimi nilikuwa ni mmoja wa wanaomuunga mkono JPM kwa muda wote aliokaa madarakani. Sikuficha kuunga kwangu mkono, nilisimama nae muda wote. Bahati mbaya Binadamu siku zake chini ya jua huwa zina mwisho hata afanye mema mengi kiasi gani.
Kipindi chote cha msiba wa JPM nilijawa na huzuni kuu, isiyoweza kuandikika. Lakini alipoapishwa Rais Samia kuwa wa sita tangu tupate uhuru sikuona sababu ya kutunza chuki kwake. Nilijua ni kudra ya mwenyezi Mungu anayemuandikia kila binadamu riziki yake na sikuwa nina wasiwasi na utendaji wake kwani alikuwa msaidizi mkuu wa hayati JPM kwa miaka yote ya urais wake.
Naona kama kivuli cha JPM kinataka kitumike kummaliza SSH. Ni wale wale waliokuwa wafuasi kindakindaki wa JPM ndio wanaogeuka maadui namba moja wa awamu ya sita!. Wanataka kumuona SSH akipita njia zile zile alizopita hayati ili wauone urais wake umekamilika.
Na hata akijaribu kurithi njia za kiuongozi za mtangulizi wake bado anacho kikwazo kingine kinachoangaliwa na hawa walioivaa roho mbaya awamu hii. Kigezo cha jinsia yake kudharaulika na kuonekana ni dhalili isiyo stahili kupewa nafasi ya juu ya uongozi. Akili zile zile duni za mfumo dume ndio zinazotawala baadhi ya vichwa.
JPM alikuwa na mfumo wake uliopambana sana kuhakikisha hakosolewi humu jukwaani na hata katika majukwaa mengine ya habari, hakupenda kukosolewa na huo ni udhaifu wake mkubwa.
Hakupenda kupokea ukosoaji kama changamoto ya mtu anayempenda bali alichukua kukosolewa kama ni uadui akiamini kwamba anajua kila kitu kinachoendelea duniani!. Huo ni udhaifu mkubwa sana na nadhani ni hulka aliyokuwa nayo tangu utotoni.
Akawa akitumia mbinu zile zile za ulaya mashariki za kuwa na wapelelezi wa chini kwa chini ili mradi tu Bwana Mkubwa asiguswe nafsi yake kitu ambacho kingemfanya akachukia. Hapa ndio naiona tofauti ya JPM na SSH.
JPM alitumia nguvu kubwa ili utendaji wake uonekane umekamilika kabisa (perfection) wakati SSH anafanya kazi na kuachia uhuru mpana wa maoni ya watu yakosoe kile ambacho wanaona hakiwafai. Wafuasi wa kudumu wa JPM sijui kama wanauona huo ufa wa awamu ya tano kwamba ni tatizo katika utendaji serikalini au upofu wa mahaba ni tatizo lao lisiloweza kutibika.
Naamini serikali ya awamu ya sita inaendeleza yale mema yaliyofanywa na awamu ya tano, kwani wote ni wale wale tu CCM. Na kwa wale wafuasi kindakindaki wa JPM kwao urais wa Samia utakuwa umekamilika iwapo atapita njia zile zile za mtangulizi wake.
Kwamba kama JPM aliwabagua na kuwaletea dharau jamii ya kimataifa na uwakilishi wao hapa nchini basi na SSH nae apite mule mule tu hata kama ni kwa madhara ya uchumi wetu kukosa kukua na kukosekana kwa harmony kwa maana ya uwepo wa uhusiano hasi wa TZ na jamii za nje.
Kwamba kama JPM alifukuza wakurugenzi na mawaziri kwa habari ambazo hakuwa na uhakika nazo basi na SSH nae apite mule mule tu, wawepo mawaziri na wateule wengi waliofukuzwa kazi huku wakiendelea kulipwa mshahara wa bure.
Kwamba kama JPM aliikuza chuki kati ya wanyonge na matajiri akiamini kuwa umaskini wa mnyonge chanzo chake ni utajiri wa tajiri basi na SSH aendeleze mateso kwa matajiri tena yale ya kihisia tu!.
SSH ameelewa umuhimu wa kujichanganya kimataifa, anajua ni kwa namna gani binadamu hajaumbwa aishi kama kisiwa hivyo amehakikisha sekta ya mahusiano na mataifa mengine inakuwa na watendaji nguli na wenye uzoefu nayo.
JPM alifanya mema lakini awamu yake isipewe sana utakatifu ambao haikuwa nao. Na SSH asipewe sana ushetani akionekana kama vile anakosea pale anapokwenda tofauti na mawazo au itikadi za mtangulizi wake.
Wote wawili kwa wakati wao wamebarikiwa kuwa marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.