Kivuli cha Hayati Magufuli kinataka kumtingisha Rais Samia

Kivuli cha Hayati Magufuli kinataka kumtingisha Rais Samia

Utata tu wa sukari ulioibuka Kwa utawala wake JPM, ufumbuzi haikuwa ni kwenda ulaya kuomba misaada, Bali Kwa kauri yake njema, alitumia vema watu waliopo,

Bakhlesa akampa shamba bagamoyo, basi mambo ya sukari yamepoa,

Uongozi ni ubunifu bhana, embu fikilia kwamba mvua hazitanyesha, tutakaa kusubiri miujiza ya Mungu.?
 
Sjaelewa hata, ulichoandika, Sjui unataka useme nini hasa!

Wafuasi wa falsafa za JPM tunataka kuona Rais akimkemea waziri wake kama Makamba Kwa kukosa njia ya kutatua tatizo la umeme

Amkemee waziri wake wa maji Kwa nini maji ni shida ili hali kuna mafungu ya dhalula na maji kuchimbwa Kwa udhalula hapo kigamboni na kuingizwa kwenye sistimu ya Dawasiko Kwa udharula uleule

Tunataka kuona Mh wetu akiwa siriazi kwenye mambo yanayogusa maisha ya watu wake

Angelikuwa kaitisha vikao vya haraka kutaka kutafuta suruhisho la maji, umeme na kupanda Kwa bidhaa

Sasa Sjui unataka kusema nini mwandishi
Pamoja nakuorodhesha hayo, raisi pia ni mfariji mkuu kwa watu wake.

Na sifa ya kuu ya kiongozi duniani ni kuaminika na watu wako; ndio science ya siasa za uchaguzi ilipo unataka wananchi wakikusikiliza na kuona matendo yako wanapata imani na wewe. Sasa kwetu kukaripia uzembe ni sehemu ya kuonyesha unajali.

Ukienda nchi zilizoendelea kama wako vitani nchi imevamiwa mwanajeshi aliekwenye chama ndio watataka awaongoze, uchumi mmbaya chaguzi zinazofuata ni economists watatawala.

Sisi tunaufisadi na uzembe uliokithiri tunataka raisi mpole asiekaripia watu; binafsi sikuwa na afiki kila kitu cha Magufuli ila alikuwa mtu sahihi kwa mazingira ya Tanzania.
 
Ni lazima nikiri wazi kabisa, mimi nilikuwa ni mmoja wa wanaomuunga mkono JPM kwa muda wote aliokaa madarakani. Sikuficha kuunga kwangu mkono, nilisimama nae muda wote. Bahati mbaya Binadamu siku zake chini ya jua huwa zina mwisho hata afanye mema mengi kiasi gani.

Kipindi chote cha msiba wa JPM nilijawa na huzuni kuu, isiyoweza kuandikika. Lakini alipoapishwa Rais Samia kuwa wa sita tangu tupate uhuru sikuona sababu ya kutunza chuki kwake. Nilijua ni kudra ya mwenyezi Mungu anayemuandikia kila binadamu riziki yake na sikuwa nina wasiwasi na utendaji wake kwani alikuwa msaidizi mkuu wa hayati JPM kwa miaka yote ya urais wake.

Naona kama kivuli cha JPM kinataka kitumike kummaliza SSH. Ni wale wale waliokuwa wafuasi kindakindaki wa JPM ndio wanaogeuka maadui namba moja wa awamu ya sita!. Wanataka kumuona SSH akipita njia zile zile alizopita hayati ili wauone urais wake umekamilika.

Na hata akijaribu kurithi njia za kiuongozi za mtangulizi wake bado anacho kikwazo kingine kinachoangaliwa na hawa walioivaa roho mbaya awamu hii. Kigezo cha jinsia yake kudharaulika na kuonekana ni dhalili isiyo stahili kupewa nafasi ya juu ya uongozi. Akili zile zile duni za mfumo dume ndio zinazotawala baadhi ya vichwa.

JPM alikuwa na mfumo wake uliopambana sana kuhakikisha hakosolewi humu jukwaani na hata katika majukwaa mengine ya habari, hakupenda kukosolewa na huo ni udhaifu wake mkubwa.

Hakupenda kupokea ukosoaji kama changamoto ya mtu anayempenda bali alichukua kukosolewa kama ni uadui akiamini kwamba anajua kila kitu kinachoendelea duniani!. Huo ni udhaifu mkubwa sana na nadhani ni hulka aliyokuwa nayo tangu utotoni.

Akawa akitumia mbinu zile zile za ulaya mashariki za kuwa na wapelelezi wa chini kwa chini ili mradi tu Bwana Mkubwa asiguswe nafsi yake kitu ambacho kingemfanya akachukia. Hapa ndio naiona tofauti ya JPM na SSH.

JPM alitumia nguvu kubwa ili utendaji wake uonekane umekamilika kabisa (perfection) wakati SSH anafanya kazi na kuachia uhuru mpana wa maoni ya watu yakosoe kile ambacho wanaona hakiwafai. Wafuasi wa kudumu wa JPM sijui kama wanauona huo ufa wa awamu ya tano kwamba ni tatizo katika utendaji serikalini au upofu wa mahaba ni tatizo lao lisiloweza kutibika.

Naamini serikali ya awamu ya sita inaendeleza yale mema yaliyofanywa na awamu ya tano, kwani wote ni wale wale tu CCM. Na kwa wale wafuasi kindakindaki wa JPM kwao urais wa Samia utakuwa umekamilika iwapo atapita njia zile zile za mtangulizi wake.

Kwamba kama JPM aliwabagua na kuwaletea dharau jamii ya kimataifa na uwakilishi wao hapa nchini basi na SSH nae apite mule mule tu hata kama ni kwa madhara ya uchumi wetu kukosa kukua na kukosekana kwa harmony kwa maana ya uwepo wa uhusiano hasi wa TZ na jamii za nje.

Kwamba kama JPM alifukuza wakurugenzi na mawaziri kwa habari ambazo hakuwa na uhakika nazo basi na SSH nae apite mule mule tu, wawepo mawaziri na wateule wengi waliofukuzwa kazi huku wakiendelea kulipwa mshahara wa bure.

Kwamba kama JPM aliikuza chuki kati ya wanyonge na matajiri akiamini kuwa umaskini wa mnyonge chanzo chake ni utajiri wa tajiri basi na SSH aendeleze mateso kwa matajiri tena yale ya kihisia tu!.

SSH ameelewa umuhimu wa kujichanganya kimataifa, anajua ni kwa namna gani binadamu hajaumbwa aishi kama kisiwa hivyo amehakikisha sekta ya mahusiano na mataifa mengine inakuwa na watendaji nguli na wenye uzoefu nayo.

JPM alifanya mema lakini awamu yake isipewe sana utakatifu ambao haikuwa nao. Na SSH asipewe sana ushetani akionekana kama vile anakosea pale anapokwenda tofauti na mawazo au itikadi za mtangulizi wake.

Wote wawili kwa wakati wao wamebarikiwa kuwa marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwadera mwanambate!!
 
Mlianzisha propaganda za kukauka kwa mto Ruvu na ukosefu wa maji chanzo ni kukatwa kwa miti ili kujenga bwawa la Nyerere

Baada ya video ya afande Sele kuwaeleza tatizo lilipo kwenye vyanzo sasa hivi serikali ndio imezinduka na maziara kila siku kukagua na kujionea uharibifu unao endelea kwenye vyanzo na njia za mito.

Ina maana bila ya video ya afande Sele kisingefanyika kitu au hao maafisa wa mabonde na NEMC walikuwa hawaoni huo uharibifu.

Hiyo kazi sio size yake Bi Tozo huo ndio ukweli, ni kuwapa watanzania shida tu kumlazimisha abaki.

Kazi ya SSH ni kubwa kuliko unavyodhania. Kurudisha mahusiano na mataifa makubwa ya nje ambao ulipotea kabisa awamu ya tano sio shughuli ndogo.

Kusaidia upatikanaji wa masoko ya bidhaa zetu kimataifa ni kazi inayotaka ubunifu mkubwa na kujua namna ya kujichanganya.

Ukame ni kweli unaleta matatizo makubwa ya maji na umeme pia, hiyo video ya afande sele ni sehemu ndogo tu ya tatizo lililoanza miaka zaidi ya thelathini la majiji kama Dar kukaisha miti ya mkoa wa Pwani kwa kukata mikaa miezi yote kumi na mbili ya mwaka.
 
Watanzania ata kesho ukimuweka ‘Angela Kairuki’ kuwa raisi awatojali ili mradi maisha yawe na unafuu.

Wanajua uwezi watengenezea ajira wote, uwezi zuia mijizi yote serikalini na wala kutatua shida zao zote pamoja na kuwaondolea umaskini.

Watanzania wanataka kiongozi anaewajali, walau anaguswa na shida, huruma nao, na mwenye kujaribu kuzitatua hata kwa kupiga mikwara, wanataka waheshimiwe kwenye huduma za serikali na kupewa haki kwenye nchi yao.

Huko juu kwenye power struggle mkifungana na kutishana kama mnavyodai Magufuli ndivyo alivyokuwa anaongoza nchi au kuachiana majukwaa ya kutukanana sawa tu.

Tofauti ya Samia na Magufuli mmoja anapendwa na wanasiasa/vigogo serikalini na mwingine alikuwa anapenda na wananchi aliokuwa anawaongoza.

Liko wazi raisi Samia hajali watanzania, yeye kajikita kufurahisha watu wenye nguvu ya kumlindia uraisi wake mpaka 2030 tu, hiyo ndio agenda yake; ila shida za watanzania sio zake.
Kazi kweli kweli !!
 
Sjaelewa hata, ulichoandika, Sjui unataka useme nini hasa!

Wafuasi wa falsafa za JPM tunataka kuona Rais akimkemea waziri wake kama Makamba Kwa kukosa njia ya kutatua tatizo la umeme

Amkemee waziri wake wa maji Kwa nini maji ni shida ili hali kuna mafungu ya dhalula na maji kuchimbwa Kwa udhalula hapo kigamboni na kuingizwa kwenye sistimu ya Dawasiko Kwa udharula uleule

Tunataka kuona Mh wetu akiwa siriazi kwenye mambo yanayogusa maisha ya watu wake

Angelikuwa kaitisha vikao vya haraka kutaka kutafuta suruhisho la maji, umeme na kupanda Kwa bidhaa

Sasa Sjui unataka kusema nini mwandishi
Tatizo la ukame wataalam wanasema ni kila baada ya miaka kumi huwa linajirudia.

Je wataalam wetu wa wizara husika chini ya mbunge wa kisarawe wanalo suluhisho la tatizo hili?.
 
Kazi ya SSH ni kubwa kuliko unavyodhania. Kurudisha mahusiano na mataifa makubwa ya nje ambao ulipotea kabisa awamu ya tano sio shughuli ndogo.

Kusaidia upatikanaji wa masoko ya bidhaa zetu kimataifa ni kazi inayotaka ubunifu mkubwa na kujua namna ya kujichanganya.

Ukame ni kweli unaleta matatizo makubwa ya maji na umeme pia, hiyo video ya afande sele ni sehemu ndogo tu ya tatizo lililoanza miaka zaidi ya thelathini la majiji kama Dar kukaisha miti ya mkoa wa Pwani kwa kukata mikaa miezi yote kumi na mbili ya mwaka.
Hizo porojo bakini nazo huko huko serikalini, na chawa mnaowatumia.

Tanzania aijawahi kutengwa kimataifa, raia wake na raisi wao ajawahi kuzuiwa kwenda nchi yeyote na wala aijawahi kuwa na mgogoro na nchi yeyote wenye kuathiri deplomatic relations.

Hakuna nchi mvua zinanyesha miezi 12 ni uzembe tu wa wizara ya maji na TANESCO ndio ulioleta shida.
 
Kwani Tanzania ilivunja uhusiano na Nchi ngapi katika kipindi cha JPM !! Maana umesema kurudisha mahusiano !! Au Rais kutokwenda nje ya Nchi maana yake mahusiano hayapo tena. ? Kwani hao mabalozi huwa wanawakilisha nini huko walipo ?!!
 
pole inakuhusu wewe unaeteseka na kivuli cha marehemu na kujifanya ulikua unamuelewa huku ukiandika gazeti refu kujustify incompetence ya bibi wa unguja
Uelewa wangu ni tofauti kabisa. Rais kutolazimika kuwa karibu na media kwa nia ya kutaka kuitawala hakumfanyi akawa dhaifu.

Ni sawa sawa na JK tulivyomuona kama vile hafai kumbe hali ni tofauti kabisa, kukubali kukosolewa na kupokea maoni tofauti na kila upande hakumfanyi rais akawa na sifa ya kuitwa dhaifu,
 
Kama haelewi Hilo watammaliza ila Kama anaelewa lazima ajipambanue kitofauti..

This time around Sukuma gang wameungana na Chadomo japo kwa maslahi tofauti..

Chadomo wanatafuta upenyo wa madaraka na Sukuma gang wanapigania Ligacy na Kutaka Mambo yaendelee Kama awali..

But Kama walishindwa mapema kabisa enzi za kina Jobo naona hiyo Ni nafasi ndogo kwao ila Chadomo ndio wanapuliza Sana..

Samia hawezi pita njia ya uovu maana kwa vigezo vyote iwe kwa namba au ufanisi Samia keshawafunika,Ni vile hapa Kuna Mambo ya dini,jinsia na Uzanzibari nothing else..

Kuliko Sukuma gang kurudi Madarakani Bora Nchi iende kwa Chadomo..

Sijawahi mkubali Mwendazake Wala siasa za CCM ila awamu hii Niko na SSH.
kwenye "chadomo" mm nikafikiri umemaanisha Chadema!
 
Uelewa wangu ni tofauti kabisa. Rais kutolazimika kuwa karibu na media kwa nia ya kutaka kuitawala hakumfanyi akawa dhaifu.

Ni sawa sawa na JK tulivyomuona kama vile hafai kumbe hali ni tofauti kabisa, kukubali kukosolewa na kupokea maoni tofauti na kila upande hakumfanyi rais akawa na sifa ya kuitwa dhaifu,
JK sio ulimuona hafai. Ni hafai.
 
Hizo porojo bakini nazo huko huko serikalini, na chawa mnaowatumia.

Tanzania aijawahi kutengwa kimataifa, raia wake na raisi wao ajawahi kuzuiwa kwenda nchi yeyote na wala aijawahi kuwa na mgogoro na nchi yeyote wenye kuathiri deplomatic relations.

Hakuna nchi mvua zinanyesha miezi 12 ni uzembe tu wa wizara ya maji na TANESCO ndio ulioleta shida.
Mtazamo na kutengwa ni vitu viwili tofauti. Tunauongelea mtazamo wa awamu ya tano na huu wa awamu ya sita.
 
Kwani Tanzania ilivunja uhusiano na Nchi ngapi katika kipindi cha JPM !! Maana umesema kurudisha mahusiano !! Au Rais kutokwenda nje ya Nchi maana yake mahusiano hayapo tena. ? Kwani hao mabalozi huwa wanawakilisha nini huko walipo ?!!
Kuna mikutano ya kusimamiwa na balozi na kuna inayomhitaji rais mwenyewe awepo ili aonyeshe uzito wa hicho ambacho taifa lake linakihitaji.

Kuna masuala kama ya vibali vya kazi, zipo zinazoweza kufanywa kwa umahiri na wataalam kutoka nje, akaanzisha utaratibu kuwa kibali kikimaliza muda wake huyo mgeni aondoke amuachie kazi mzalendo.

Yale yale ya Mugabe na uporaji wa mashamba ya wazungu, waafrika walioachiwa yamewafia mikononi huku wazungu wakiwacheka tu.

Labda nia ilikuwa nzuri lakini inapokosewa katika utekelezaji wake inaleta picha ya serikali nzima kuwa na hulka za kibaguzi.
 
Kazi ya SSH ni kubwa kuliko unavyodhania. Kurudisha mahusiano na mataifa makubwa ya nje ambao ulipotea kabisa awamu ya tano sio shughuli ndogo.

Kusaidia upatikanaji wa masoko ya bidhaa zetu kimataifa ni kazi inayotaka ubunifu mkubwa na kujua namna ya kujichanganya.

Ukame ni kweli unaleta matatizo makubwa ya maji na umeme pia, hiyo video ya afande sele ni sehemu ndogo tu ya tatizo lililoanza miaka zaidi ya thelathini la majiji kama Dar kukaisha miti ya mkoa wa Pwani kwa kukata mikaa miezi yote kumi na mbili ya mwaka.
Hapa ndio nimekuelewa ulianza kumsifia marehemu kumbe kinafiki, kumbe ni mlamba asali.

Leta maji na umeme, wacheni propaganda za kishamba. Kuongoza nchi sio kama kucheza mdako
 
Mtazamo na kutengwa ni vitu viwili tofauti. Tunauongelea mtazamo wa awamu ya tano na huu wa awamu ya sita.
Diplomatic relations ni factual sio mtazamo. Either upo au aupo.

Shida hapo ni story za social media mlizokuwa mnajiambia na kujiaminisha wenyewe; lakini Tanzania aijawahi kuwa na diplomatic issues na nchi yeyote.

Labda kama kuweka msimamo kwenye mambo yako ya kujiamulia kinyume na mabeberu wanavyotaka, panapo tokea majibizano ya hapa na pale ndio tafsiri yako kuharibika kwa diplomatic relations.
 
Until that day...,
When we the people will know its not who is up there who makes things happen, but rather we the people down here who can make a change...., And not through voting but through demanding day to day what is right, and what should be done, and make our voices heard now and not waiting 5 more years for the chance to vote

Until that day....,
When we will know its us who decides what the person up there should do and not her / his favor to do what's supposed to be done...

Until that day...,
When we will know individuals won't make a dent of change but having strong institutions and knowledgeable citizens who are patriotic...

Before then we will continue writing and commenting on such threads with nothing to show for it....
 
Back
Top Bottom