Kivuli cha Hayati Magufuli kinataka kumtingisha Rais Samia

Kivuli cha Hayati Magufuli kinataka kumtingisha Rais Samia

nadhani huyo unayetaka kumsifu hivyo wee endelea kumsifu tu, ila naye ana mwisho wake. Niliwaona mama ntilie na machinga dodoma wanavyohangaika barabarani, wanabomolewa mabanda yao alafu kule kule machinga hakutoshi. migambo wamepata nguvu tena kama awamu zile kabla ya JPM, ila nawaambieni nyie wote ambao hamjui shida za watu wa chini endeleeni kujitia wazimu ila mjue ipo siku ipo mwisho
Magufuli alikuwa ni populist president alifanya mambo ambayo busara ya kawaida isingeweza kuyaelewa ilmradi tu yalimhakikishia kupendwa na umma.

Machinga wanapokosa kuwa na utaratibu maalum wa kufanya biashara miji inageuka sehemu za kufanyia biashara na unakuwa ni uchafu fulani mkubwa. Unakuwa ni ukosefu wa mpangilio.

JPM aliwahurumia wafanya biashara ndogo ndogo lakini nini kinafuata baada ya huruma kwisha?. Hatupendi kuambiwa ukweli na uongo una gharama zake tena kubwa tu.
 
Kwa ujumla Rais Samia kafanya kazi kubwa mno. Mfano tu mfumuko wa bei ukilinganisha na Kenya au Uganda upo chini.
Ajira zinafunguka kwa wingi muda huu. Polisi kunafumuliwa kote ili kuendana na jamii ya kistaarabu.
 
Magufuli alikuwa ni populist president alifanya mambo ambayo busara ya kawaida isingeweza kuyaelewa ilmradi tu yalimhakikishia kupendwa na umma.

Machinga wanapokosa kuwa na utaratibu maalum wa kufanya biashara miji inageuka sehemu za kufanyia biashara na unakuwa ni uchafu fulani mkubwa. Unakuwa ni ukosefu wa mpangilio.

JPM aliwahurumia wafanya biashara ndogo ndogo lakini nini kinafuata baada ya huruma kwisha?. Hatupendi kuambiwa ukweli na uongo una gharama zake tena kubwa tu.
nisipojibiwa baadhi ya maswali huwa naona maneno hayo yote ni porojo tupu na siasa. Magufuri alikuwa hana siasa za muundo huo...alikuwa anaishi na maumivu ya wanyonge.
wewe nikikuuliza maswali haya utanijibuje?
1. kwasasa mmewaondoa machinga ni miji gani imegeuka kuwa misafi?, uchafu wake ulikuwa upi?
2. Baada ya machinga kuondolewa miji imepangiliwa kwa kiasi gani?, nini kimepangwa ktk yale maeneo mliyoondoa machinga? au mnafurahia kuona maeneo yapo wazi tu?
3. Nitajie vitu ambavyo vingefuata baada ya huruma ya JPM kwa machinga?, mtuambie wazi msiishie kutufumbia mafumbo tupu, wekeni wazi tuelewe nia yenu ni nini?, ni kuvuruga maisha ya watu wa chini?, au mna maana gani?
 
JPM alikuwa ni populist president, rais mpenda umaarufu. Ni bahati mbaya TZ haina mambo ya kura za maoni (opinion polls) vinginevyo JPM angependa awe anapata alama zaidi ya 85 kila inapopigwa kura kuhusu maamuzi yake fulani.

Tembea na hiyo kichwani mwako kwanza kwa sasa.
 
hujanijibu swali hata moja, unanipa historia tupu ndugu yangu
 
Machinga kwa wingi wao na kukosa mpangilio kwa biashara zao walikuwa wakichafua miji. JPM aliwatumia kisiasa zaidi kuliko kuwa mkweli kwa hatima yao.

Duniani kote wamachinga wapo na kuna mataifa ni wengi kuliko hawa tulionao TZ kwa miaka ya sasa. Lakini upo mpangilio wa kufanya biashara zao, hawavamii tu kila eneo lililo wazi na kuanza kufanya biashara.

Nidhamu ya mpangilio wa miji inatazamwa na uwepo wao pia unatazamwa, JPM hakutaka kuutazama ukweli huo kwa tabia yake ya kiburi na ubishi hata katika mambo ya maana ya kujenga nchi.

Tukumbuke kuwa uzuri wa nchi yetu upo pia huko katika mbuga za wanyama na wazungu wanaokuja hufikia mijini kwanza kabla ya kwenda kutembea na kuangalia mandhari zetu.

Na wanapokuja wanazunguka katika mitaa ambayo ina usafi, wanapata kutembea kwa amani. Sio kila mtalii anapotia mguu awe na wasiwasi wa kukanyaga biashara za watu.

JPM hakutazama upande wa pili wa ukuzaji wa uchumi kwa kutegemea ndege hizo hizo alizokuwa anazinunua, kwamba zinaleta watalii wanaokuja na mitazamo yao ya kidunia hivyo miji yetu haiwezi kugeuka uwanja wa fujo kwa kuitii tu nguvu ya machinga.
 
Kila Rais ametimiza wajibu wake kuanzia awmu ya 1 hadi 5 tusiwe watu wa kubeza kila kitu. Awamu ya sita naye anatimiza wajibu wake mbali na changamoto zilizojitokeza kila awamu. There is no absolute perfection in leadership.
 
Watanzania wanataka kiongozi anaewajali, walau anaguswa na shida, mwenye huruma nao, na mwenye kujaribu kuzitatua changamoto zao hata kwa kupiga mikwara, wanataka waheshimiwe kwenye huduma za serikali na kupewa haki kwenye nchi yao.
Dume zima unataka uhurumiwe?? uguswe Makalio yenye shida? fanya kazi! huruma za nini?? kwani sie mayatima??....jihesimu weye ukiwa kwenye huduma za serikali!

haki unayataka zaidi ya hii sasa utakuwa ni wenda wazimu binadamu hamuridhiki!! usituletee dhiki za kwenu hukooooo...
 
Ni lazima nikiri wazi kabisa, mimi nilikuwa ni mmoja wa wanaomuunga mkono JPM kwa muda wote aliokaa madarakani. Sikuficha kuunga kwangu mkono, nilisimama nae muda wote. Bahati mbaya Binadamu siku zake chini ya jua huwa zina mwisho hata afanye mema mengi kiasi gani.

Kipindi chote cha msiba wa JPM nilijawa na huzuni kuu, isiyoweza kuandikika. Lakini alipoapishwa Rais Samia kuwa wa sita tangu tupate uhuru sikuona sababu ya kutunza chuki kwake. Nilijua ni kudra ya mwenyezi Mungu anayemuandikia kila binadamu riziki yake na sikuwa nina wasiwasi na utendaji wake kwani alikuwa msaidizi mkuu wa hayati JPM kwa miaka yote ya urais wake.

Naona kama kivuli cha JPM kinataka kitumike kummaliza SSH. Ni wale wale waliokuwa wafuasi kindakindaki wa JPM ndio wanaogeuka maadui namba moja wa awamu ya sita!. Wanataka kumuona SSH akipita njia zile zile alizopita hayati ili wauone urais wake umekamilika.

Na hata akijaribu kurithi njia za kiuongozi za mtangulizi wake bado anacho kikwazo kingine kinachoangaliwa na hawa walioivaa roho mbaya awamu hii. Kigezo cha jinsia yake kudharaulika na kuonekana ni dhalili isiyo stahili kupewa nafasi ya juu ya uongozi. Akili zile zile duni za mfumo dume ndio zinazotawala baadhi ya vichwa.

JPM alikuwa na mfumo wake uliopambana sana kuhakikisha hakosolewi humu jukwaani na hata katika majukwaa mengine ya habari, hakupenda kukosolewa na huo ni udhaifu wake mkubwa.

Hakupenda kupokea ukosoaji kama changamoto ya mtu anayempenda bali alichukua kukosolewa kama ni uadui akiamini kwamba anajua kila kitu kinachoendelea duniani!. Huo ni udhaifu mkubwa sana na nadhani ni hulka aliyokuwa nayo tangu utotoni.

Akawa akitumia mbinu zile zile za ulaya mashariki za kuwa na wapelelezi wa chini kwa chini ili mradi tu Bwana Mkubwa asiguswe nafsi yake kitu ambacho kingemfanya akachukia. Hapa ndio naiona tofauti ya JPM na SSH.

JPM alitumia nguvu kubwa ili utendaji wake uonekane umekamilika kabisa (perfection) wakati SSH anafanya kazi na kuachia uhuru mpana wa maoni ya watu yakosoe kile ambacho wanaona hakiwafai. Wafuasi wa kudumu wa JPM sijui kama wanauona huo ufa wa awamu ya tano kwamba ni tatizo katika utendaji serikalini au upofu wa mahaba ni tatizo lao lisiloweza kutibika.

Naamini serikali ya awamu ya sita inaendeleza yale mema yaliyofanywa na awamu ya tano, kwani wote ni wale wale tu CCM. Na kwa wale wafuasi kindakindaki wa JPM kwao urais wa Samia utakuwa umekamilika iwapo atapita njia zile zile za mtangulizi wake.

Kwamba kama JPM aliwabagua na kuwaletea dharau jamii ya kimataifa na uwakilishi wao hapa nchini basi na SSH nae apite mule mule tu hata kama ni kwa madhara ya uchumi wetu kukosa kukua na kukosekana kwa harmony kwa maana ya uwepo wa uhusiano hasi wa TZ na jamii za nje.

Kwamba kama JPM alifukuza wakurugenzi na mawaziri kwa habari ambazo hakuwa na uhakika nazo basi na SSH nae apite mule mule tu, wawepo mawaziri na wateule wengi waliofukuzwa kazi huku wakiendelea kulipwa mshahara wa bure.

Kwamba kama JPM aliikuza chuki kati ya wanyonge na matajiri akiamini kuwa umaskini wa mnyonge chanzo chake ni utajiri wa tajiri basi na SSH aendeleze mateso kwa matajiri tena yale ya kihisia tu!.

SSH ameelewa umuhimu wa kujichanganya kimataifa, anajua ni kwa namna gani binadamu hajaumbwa aishi kama kisiwa hivyo amehakikisha sekta ya mahusiano na mataifa mengine inakuwa na watendaji nguli na wenye uzoefu nayo.

JPM alifanya mema lakini awamu yake isipewe sana utakatifu ambao haikuwa nao. Na SSH asipewe sana ushetani akionekana kama vile anakosea pale anapokwenda tofauti na mawazo au itikadi za mtangulizi wake.

Wote wawili kwa wakati wao wamebarikiwa kuwa marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kila mtu alimuunga mkono JPM wakati wa utawala wake . Wale ambao hawakumuunga mkono waliwekwa katika viroba.
 
Dume zima unataka uhurumiwe?? uguswe Makalio yenye shida? fanya kazi! huruma za nini?? kwani sie mayatima??....jihesimu weye ukiwa kwenye huduma za serikali!

haki unayataka zaidi ya hii sasa utakuwa ni wenda wazimu binadamu hamuridhiki!! usituletee dhiki za kwenu hukooooo...
Hizo ajira ziko wapi? Ulimsikia kilaza mwenzio juzi (waziri wa fedha) ye mwenyewe hana mbinu za kuwasaidia watanzania millioni moja kila mwaka wanaoingia kwenye soko la ajira.

Sasa hujui utawapa vipi vijana kazi, hapo hapo unawawekea mitozo, bei ya chakula inapanda, usalama wa ndani ya familia tu una mashaka (kila siku mauaji), huduma za serikali rushwa kwenda mbele.

Huyo mama kazi analazimisha tu.

Zamani Lumumba Nape alikuwa na team rasmi, sio kila mwenye njaa avae njuga kutukana watu mitandaoni, maana hiyo inaweza ruhusu na wengine kutukana baadhi ya watu kwa lengo la kusaidia mashambulizi.

Sasa we endelea kama umeamka unawashwa nitakuwa happy kumpa huyo mama yako dose tosha.
 
Matusi ni kielelezo cha maumivu uliyonayo moyoni na kuyaweka hapa jukwaani hayakusaidii wala hayamsaidii mchangiaji yoyote.

Changamoto ya ajira ni ya dunia nzima usidhani ni TZ peke yake. Ongezeko la watu linalizidi ongezeko la ajira zenye kueleweka, hii ni changamoto ya wachumi popote walipo. JPM alizalisha ajira ngapi zilizo rasmi?, au Kikwete na Mkapa walizalisha ajira ngapi?. Mwinyi na Nyerere angalau TZ yao haikuwa na idadi ya watu kama tatizo la kiuchumi.

Unamsema Nape, umesahau ule ushamba wa Makonda alipokuwa RC wa Dar?. Umesahau unyama uliofanyika kule kaskazini baada ya yule dogo kujigeuza Mungu mtu akawa anawapiga misumari ya miguu wasio na hatia?.

SSH anaifaa Tanzania anaiongoza kistaarabu sana.
 
Ukusoma post ya huyo mtu alie ni quote lugha aliyotumia ama, umeona yangu tu.

Mimi sijamzungumzia Nape kwa nia mbaya ila walikuwa na team rasmi ya kujibu mashambulizi humu na viji agenda uchwara.

Sio hawa chawa aina ya kina Babalevo ambao badala ya kujibu hoja jitu linaanza na kutukana watu.
 
Back
Top Bottom