Kivuli cha Kwame Nkrumah katika TANU

Ongezeo, tumemsoma Kwame, Nelson, Keneth, Ghaddafi, Mugabe, BenBella, Nujoma na wengineo wa nyakati hizi katika contemporary African politics.
Lakini bado kwa sisi wengine tunamuona Nyerere kama aliwazidi wengi ktk uongozi hasa ktk kujenga msingi wa uongozi katika awamu ya kwanza ya uongozi baada ya uhuru.
 
ndo Mana na nyerere senior hawakuiva waliiva kiupande upande
 
Unaulizwa Malealle wewe unadakia Sykes
 
Mzee,
Nimepata shauku, andiko la Nguruvi linatakiwa kudhibitishwa.
Kwa ufahamo wako, ni kweli kuwa Ally Sykes hakuwai toa hutuba yoyote ya kudai uhuru nje ya Mwembe Togwa au nje ya Dar esam Salaam?
James...
Nguruvi haipendi historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ambayo mimi nimeandika katika kitabu cha Abdul Sykes.

Kabla ya mimi kuandika historia hii historia ya TANU na uhuru ilikuwa ikitamtaja Nyerere peke yake.

Hapo ndipo mimi nikaandika historia ya harakati za uhuru kupitia Nyaraka za Sykes.

Ukifanya rejea nyuma utaona niliyoandika.

Yeye anaemkusudia ni Abdul Sykes si Ally Sykes mdogo wake.

Kleist Sykes baba yao hawa ndugu wawili na Abbas Sykes ndiye aliyeasisi African Association mwaka wa 1929 lakini hakuna popote nilipokuta kuwa alikuwa anahutubia mikutano ya hadhara.

Sababu ni kuwa wakati wa African Association hadi TAA viongozi hawakuwa wanaitisha mikutano ya hadhara.

Mikutano ya hadhara ilianza baada ya TANU kuundwa 1954.

Nguruvi tatizo lake ni kuwa nisingeandika historia ya Abdul Sykes anataka tubakie ni ile historia rasmi ya Chuo Cha CCM Kivukoni ambayo Abdul Sykes na wazalendo wengine hawakutajwa ila Julius Nyerere peke yake
 
Unaulizwa Malealle wewe unadakia Sykes
Kolola,
"Marealle."

Hapana sikudakia.
Hii ni katika kuieleza historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Mangi Mkuu Chief Thomas Marealle alikuwa rafiki mkubwa wa Abdul Sykes na kila akifika Dar es Salaam ilikuwa lazima amtembelee Abdul nyumbani kwake.

Na machifu wote wakifanya hivi.

Nimesoma barua ambazo Thomas Marealle alikuwa akiandikiana na Ally Sykes wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hizi barua zinasisimua sana.
 
Vipi kuhusu Chief Edward wa UMASSAI, alifahamiana na Nkurumah lini ??
 
Marealle alienda kudai Uhuru wa Wachagga, hakuwa na Chama.
Laki...
Akiwa hana chama cha siasa sasa atatoa au alitoa vitambulisho ''credentials,'' gani UNO?

Ungetusaidia sana kama ungetupa ''source,' ya hizi taarifa zako.
 
Vipi kuhusu Chief Edward wa UMASSAI, alifahamiana na Nkurumah lini ??
Malcom...
Sijapata kumsikia huyu Chief Edward wa Umasai lakini kwa ufupi machifu wote walikuwa upande wa serikali ya kikoloni na ndiyo maana ikawa tabu kwao kujiunga na harakati za kudai uhuru.
 
Malcom...
Sijapata kumsikia huyu Chief Edward wa Umasai lakini kwa ufupi machifu wote walikuw aupande wa serikali ya kikoloni na ndiyo maana ikawa tabu kwao kujiunga na harakati za kudai uhuru.
Mtafute, alikuwa ni moja ya wapambania uhuru wa mapema kabisa nchini Tanganyika. Alishauriwa na baadhi ya viongozi wa dini wenye asili ya Kimarekani kudai uhuru wa maeneo ya wamassai tu. Alikuwa na ushawishi mkubwa sana tu kwenye eneo lake.

Ukipitia baadhi ya nyaraka za Foreign Affairs zinazoelezea kilichotokea kuanzia mwaka 1949-1964 utakutana na majina ya watu ambao walianza kudai uhuru wa maeneo yao husika wakishirikiana na taasisi kubwa za kidini duniani.

Huu ukurasa wa historia haujawekwa wazi,......
 
Malcom...
Chief Edward ni nani na alikuwa chief wa wapi?
Alikuwa ni Chief wa wamassai, alikuwa na ushawishi mkubwa sana akisaidiwa na viongozi wa dini (Catholic Priests) kutoka Marekani ili kudai uhuru wa eneo lake pekee. Huwezi kumkuta kwenye vitabu vya historia, mpaka ufanya jitihada za ziada ndiyo utamfahamu. Nyaraka za historia za Ministry of Foreign Affairs zimewahi kumtaja, fanya kuzitafuta.
 
James...
Inataka uwe umesoma vitabu vya kutosha.
Historia ya Tanzania ina mengi sana wengi hamyajui.

Labda nikuulize swali moja kisa tuendelee.
Ulikuwa unaijua historia ya Abdul Sykes na TANU?
 
Malcolm...
Hebu weka hapa rejea tusome.

Mimi nimesoma kila kilichoandikwa kuhusu Tanganyika lakini haya unayosema sijayaona popote.

Hizo Nyaraka za Foreign Affairs ni zipi na ziko katika maktaba gani?
Chief Edward lipi jina lake la pili?


Maasai society is organised into male age-groups whose members together pass through initiations to become warriors, and then elders. They have no chiefs, although each section has a Laibon, or spiritual leader, at its head.
 
Malcolm...
Hebu weka hapa rejea tusome.

Mimi nimesoma kila kilichoandikwa kuhusu Tanganyika lakini haya unayosema sijayaona popote.

Hizo Nyaraza za Foreign Affairs ni zipi na ziko katika maktaba gani?
Mkuu una maana gani kusema umesoma yote yaliyoandikwa kuhusu Tanganyika ??? Kuna tafiti za wizara ya mambo ya nje ziliandikwa na Earl Seaton na Sosthenes Maliti zimeyaweka haya wazi kabisa. Kuna chapisho lao linaitwa Tanzanian Treaty Practice litafute uzipate hizi taarifa.
 
Malcom,
Mimi sina tatizo na taarifa hizi nauliza ili nipate kujua.

Earle Seaton nimemkuta katika Nyaraka za Sykes na mimi naamini ndiye mwandishi wa kwanza kumuhusisha na harakati za uhuru wa Tanganyika watu wakamsoma.

Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes utakuta historia yake humo.
 
Malcom...
Nimeanza kutafuta hizi taarifa:

Sijapata hiyo taarifa lakini naendelea.

Nimeona na hiyo hapo chini:


Bahati mbaya sijaweza kufungua na kusoma kuhusu Wamasai kudai uhuru wao.

Lakini umenisaidia kwa kueleza kuwa "Chief" Edward alishauriwa na watu kutoka Amerika adai uhuru.

Ndiyo kusema yeye mwenyewe hakuwa na fikra ya kuutaka uhuru wake?

Je aliunda chama cha kuwaunganisha watu wake?

Maswali ni mengi.
 
Acha kujirudiarudia kila siku wewe Mzee. Wewe si mzima tushang'amua hilo, una ugonjwa wa akili kila mara kujirudiarudia na stories zako na kutafuta mwanya wowote lengo lako kuu likiwa kusifia Sykes kwa namna yoyote. Unajishushia hadhi na maandiko yako hayana credibility ya kuwa historia sababu una upendeleo wa wazi.
 
Unaulizwa swali kuhusu uhusiano wa Marealle na Nkrumah, badala ya kujibu swali kwa vithibitisho, wewe unaanza kuwasifia Sykes eti walifahamiana na Nkrumah hata kabla ya Nyerere. Ni sawa na pale ulipoulizwa swali Sykes kahutubia wapi nje ya Kariakoo, wewe badala ya kujibu swali, unaleta story ya Sykes kumliki Mercedes Benz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…