Nguruvi,
Mimi sikejeli wala kukebehi.
Nakueleza historia ya TANU kama ukweli wake ulivyokuwa.
Na nimenyanyua kalamu baada ya kuona hizo historia zilizoandikwa zimepotoshwa.
Nani alikuwa anaijua historia ya African Association, TAA hadi kuundwa kwa TANU kwa kiwango nilichoeleza mimi?
Kadi ya TANU No. 1 Territorial President Julius Kambarage Nyerere, kadi No. 2 Ally Kleist Sykes, kadi No. 3 Abdulwahid Kleist Sykes, kadi No. 4 Waziri Dossa Aziz, kadi No. 5 Denis Phombeah (Mnyasa) Kadi No. 6 Dome Okochi Budohi (Mkenya).
Nani alikuwa anaijua historia hii?
Katika hao wanachama wa TANU sita ambae sikupata kuwajua ni wawili - Nyerere na Phombeah.
Hawa nimewasoma katika Nyaraka za Sykes.
Lakini hao wote sita nimeeleza historia zao katika kitabu cha Abdul Sykes.
Kitabu hiki kimevunja rekodi tunakwenda toleo la tano Kiswahili na Kiingereza.
Kwa nini kitabu hiki kimependwa kiasi hiki?
Sababu ni kuwa hii ndiyo historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Nikejeli na "Mwembe Togwa," na maneno yote upendayo mimi sirejeshi kejeli narejesha maneno ya kweli katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika kwa ushahidi wa picha na nyaraka.
Ndiyo maana hapa nimeingia na jina langu halisi.
Wewe unaweza ukatukana, ukakejeli na kukebehi.
Anakujua nani?
Mimi niko hapa kwa picha na sauti.
Hakuna asiyenifahamu.
Mimi nimebeba dhima ya elimu yangu na heshima ya walimu wangu na heshima ya mama yangu aliyenifunza adabu.
Sithubutu kukurejeshea ufedhuli.