Uchaguzi 2020 Kiwanda alichoahidi Godbless Lema kukijenga kwa pesa yake Arusha kipindi hiki cha Awamu ya Tano kimefikia wapi?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Godbless Lema ni mmoja wa wawekezaji ambaye alinunua hadi mitambo ya kujenga kiwanda cha kutengeneza toothpick na leseni ili nchi isiendelee kuagiza toka nje kipindi hiki cha serikali ya Awamu ya Tano.

Kama kimeshakamilika ni vizuri akakitumia kueleza mafanikio yake alivyosaidia nchi kwa kuokoa pesa za kigeni na kuunga mkono juhudi za serikali za ujenzi wa viwanda na kuongeza ajira kwa wasiokuwa nazo.

Godbless Lema aliitikia wito wa Serikali wa ujenzi wa viwanda sijui kwa nini anaona aibu kusimama na kusema mimi ni mmoja niliyejenga kiwanda. Anafanya siri ili iweje?

Upinzani mara ingine unaonekana bogus bila sababu wakati kuna vitu vipo na upinzani umefanya vya kusaidia nchi na jamii lakini mtu anakauka tu ili tu ionekane Serikali haijafanya kitu .Sema basi walau chako ulichofanya,Usiposema Serikali inaonekana haijafanya kitu na wewe hujafanya kitu so what?
 
Kama alipewa misamaha ya kodi na hakujenga TRA kwa kweli inabidi muufuatilie huo mradi wa hicho kiwanda
 
Hicho kiwanda si ndio kile ex-RC Gambo alienda kukihujumu?
 
hakiwezi kufika kwasababu alifungwa jela na wakandamizaji, ule mda ndio angeweza
 
Hicho kiwanda si ndio kile ex-RC Gambo alienda kukihujumu?
Sio chake alikopa karibu bilioni moja akijenge kilitajwa hadi na waziri wa biashara na viwanda bungeni ni cha toothpick hakijulikani kiko wapi? ndio maana nauliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…