Kiwanda cha Cement Tanga chasimamisha uzalishaji kutokana na ukosefu wa umeme

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
866
Reaction score
1,109
Taarifa ya habari ya UTV imeripoti leo magari ya kubeba cement yamekwama kwa zaidi ya siku saba kwa ukosefu wa mzigo wa cement kutokana na kusimama uzalishaji.

TANESCO imeshindwa kutoa umeme wa kutosha kwa uzalishaji na meneja wa kiwanda amedai wanatumia zaidi ya milioni 500 kwa mwezi kununua dizeli ambayo pia yanasaidia uzalishaji kidogo kwa ajili ya miradi ya kimkakati. Je, kwanini uongozi wa Tanesco usiadhibiwe kwa kushindwa kuondoa hili tatizo?

Kwa hali hii kweli tuko serious kuita wawekezaji kuanzisha viwanda nchini? Kwa nini haya matatizo ya TANESCO yamekuwa mengi katika siku za karibu?
 
Imeripotiwa leo tar, 18/08/2022 magari ya kubeba cement yamekwama kwa zaidi ya siku saba kwa ukosefu wa mzigo wa cement kutokana na kusimama uzalishaji.

TANESCO imeshindwa kutoa umeme wa kutosha kwa uzalishaji na meneja wa kiwanda amedai wanatumia zaidi ya milioni 500 kwa mwezi kununua dizeli ambayo pia yanasaidia uzalishaji kidogo kwa ajili ya miradi ya kimkakati.
 
Tatzo unakuta meneja nae n mbogamboga sema ukweli kama kodi lukuki,bei ya dizel ndio imesababisha mshindwe kuendesha kiwanda
 
Utendaji siku zote huwa hautaki maneno mengi, wala interviews kwenye kila chombo cha habari kuelezea mikakati ya gas wakati umeme tulionao bado hautoshi mahitaji, hizi siasa ndio zinalirudisha nyuma hili taifa, na hizo show off naona waachiwe wasanii tu.
 
Halafu walisema Magufuli aliuwa uchumi, sasa hivi nimekuja kuelewa kwamba ambao walimpinga Magufuli hawakumuelewa kwa maana Intelligence yao haikuruhusu kuelewa intelligent things.

Hilo halikutokea na lisingewezekana kama Magufuli angekuwepo!
 
Tatizo ni kwamba Makamba ni mgeni na mama hana maarifa hivyo watumishi wanawachezea
 
Kama umeme hautoshi utawaadhibu vipi Tanesco?
 
Mmeipenda wenyewe mbambamba chaguo lenu milelee nawavimbe wapasukeee acha waisome namba eeee ccm MBELE kwa mbeleee....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…