Kiwanda cha Cement Tanga chasimamisha uzalishaji kutokana na ukosefu wa umeme

Kiwanda cha Cement Tanga chasimamisha uzalishaji kutokana na ukosefu wa umeme

Tatizo letu hatuna akili. Huku tozo huku viwanda vinafungwa. Hii wizara angepewa mh. Bashe hao akina ma K ni wapigaji tu.
 
Taarifa ya habari ya UTV imeripoti leo magari ya kubeba cement yamekwama kwa zaidi ya siku saba kwa ukosefu wa mzigo wa cement kutokana na kusimama uzalishaji.

TANESCO imeshindwa kutoa umeme wa kutosha kwa uzalishaji na meneja wa kiwanda amedai wanatumia zaidi ya milioni 500 kwa mwezi kununua dizeli ambayo pia yanasaidia uzalishaji kidogo kwa ajili ya miradi ya kimkakati. Je, kwanini uongozi wa Tanesco usiadhibiwe kwa kushindwa kuondoa hili tatizo?

Kwa hali hii kweli tuko serious kuita wawekezaji kuanzisha viwanda nchini? Kwa nini haya matatizo ya TANESCO yamekuwa mengi katika siku za karibu?
Hakuna crisis yoyote ya umeme iliyoripotiwa mkoani Tanga, iweje itokee Kwa kiwanda kimoja? Una uhakika tatizo ni TANESCO? Tafuta habari iliyobalance kuliko kuleta uwongo uwongo JF.
Weka taarifa rasmi kutoka kwenye menejimenti ya kiwanda hicho umma ujiridhishe.
 
14 October 2019

Bei ya makaa haitaongezeka - Waziri Biteko



Waziri wa Madini, Doto Biteko amesisitiza kwamba bei ya ununuzi wa makaa ya mawe haitaongezeka zaidi ya bei elekezi ya Serikali. Waziri Biteko ametoa kauli hiyo Oktoba 14, 2019 jijini Mwanza alipokutana na wanunuzi wa madini hayo kutoka makampuni ya Tanga Cement, Lake Cement pamoja na KEDA (Tanzania) Ceramics wanaotumia madini hayo kama nishati ya viwandani kwa ajili ya uzalishaji wa saruji na vigae vya majumbani.

Hatua hiyo inatokana na wanunuzi wa makaa ya mawe nchini kuwa na mvutano wa bei baina yao na kampuni ya TANCOAL inayowauzia madini hayo. Mvutano huo ulianza baada ya Serikali kuitaka kampuni ya TANCOAL kulipa deni la Tsh. Bilioni 23.9 ambazo ni mrabaha wa mauzo na usafirishaji wa makaa ya mawe pamoja na adhabu ya asilimia 50 kuanzia Septemba mwaka 2011 hadi Juni 2019 ambapo kampuni hiyo ilitaka kuongeza bei ya madini hayo ili kufidia gharama za deni hilo.

Source : BMG Online Media
 

Thursday, 1 December 2016​

MADINI ya Makaa ya Mawe (Coal Mines) Tanzania​


Nchi yetu ni tajiri mkubwa wa madini mbali mbali yakiwemo madini ya MAKAA YA MAWE.

Makaa ya mawe ni nini?

Makaa mawe ni aina ya mwamba mashapo au mwamba metamofia na fueli kisukuu muhimu. Ilitokea kutokana na mabaki ya mimea ya kale iliyogeuzwa kuwa aina ya mwamba katika mchakato wa miaka mamilioni.

Kikemia ni hasa kaboni. Kijiolojia inatokea kama kanda pana au nyembamba katikati ya miamba mengine. Huchimbwa mara nyingi katika migodi chini ya ardhi au kama iko karibu na uso wa ardi katika machimbo ya wazi yaliyo kama mashimo makubwa.




Katika nchi yetu madini haya yanapatikana maeneo ya fuatayo (kwa sasa):-

-KIWIRA
-LUDEWA
-RUVUMA
-MBINGA
-SONGEA

UTAFITI umebaini kuwa madini ya makaa ya mawe ambayo yanachimbwa kwenye Mgodi wa Ngaka, wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma yanaongoza kwa ubora duniani.

Kabla ya kuanza rasmi mgodi huo, taarifa zinaonesha kwamba zaidi ya tani 1,000 za makaa ya mawe zilisafirishwa kupelekwa nchini Afrika ya Kusini ili kuchunguza ubora wa madini hayo.

Matokeo ya utafiti huo uliofanyika kuanzia mwaka 2008 umeonesha kuwa ubora wa madini hayo haufanani na madini ya makaa ya mawe yanayochimbwa katika nchi yoyote duniani. Utafiti umebaini kuwa mgodi huo unakadiriwa kuwa na zaidi ya tani milioni 400 za makaa ya mawe.

Kiasi hicho, kwa mujibu wa wataalamu waliofanya utafiti, kinaweza kuchimbwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100.

Utafiti wa madini hayo ulifanyika kwa kuangalia wingi wa madini ya makaa wa mawe, unene wa mwamba na ubora wa makaa hayo.

Utafiti umebaini kuwa kijiji cha Ntunduwaro kipo juu ya mwamba bora wa madini ya makaa ya mawe ambayo yamesambaa pia na maeneo jirani ya kata ya Ruanda.
Mkuu wa Masoko wa Mgodi wa Ngaka, Christopher Temba anasema mgodi huo unazalisha tani za makaa ya mawe laki tano kwa mwaka lakini lengo ni kufikia tani milioni moja.



Madini hayo yanasafirishwa katika nchi za Kenya, Zambia na Malawi.
Mgodi wa Ngaka, unamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania yenye asilimia 30, na Kampuni ya Intra Energy ya Australia yenye hisa ya asilimia 70.

Kulingana na Kaimu Meneja Mkuu Uzalishaji wa Kampuni ya TANCOAL, Boscow Mabena, kampuni hiyo kuanzia Julai 2014 hadi Desemba 2015 imezalisha tani 272,852 za makaa ya mawe na kati ya hizo, tani 257,570 zimeuzwa na kuwezesha Serikali ya Tanzania kuingiza fedha kwa kodi zaidi ya Sh bilioni 2.

Mabena anawataja wateja wakuu wa madini hayo hapa nchini kuwa ni viwanda vya Lake Cement, Tanga Cement, Mbeya Cement, Dangote, Mufindi Paper Mills na Mohamed Interprises.

Anasema, awali viwanda hivyo vilikuwa vinaagiza madini ya makaa ya mawe toka nchini Afrika ya Kusini jambo lililosababisha gharama kuwa juu huku serikali ikikosa mapato.


Anabainisha kuwa Kampuni ya TANCOAL imepewa vitalu saba vya kuchimba madini ya makaa ya mawe ambapo kila kimoja kina ukubwa wa kilomita za mraba 9.9 na shughuli ya uchimbaji katika mgodi huo imetimiza miaka mitano hadi kufikia mwaka 2015.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ntunduwaro, John Haule, Agatha Mapunda na Mary Komba wanatoa rai kwa serikali kuhakikisha madini hayo yanawanufaisha Watanzania na kuinua uchumi wa taifa. Wanaiomba Wizara ya Nishati na Madini kusimamia rasilimali hiyo kwa mujibu wa sera na sheria zilizopo ili Watanzania wanufaike kwanza badala ya wageni kupata manufaa zaidi.

Lakini pia wameonya kwamba kama una madhara ya kiafya wanayopata wananchi wanaozunguka mgodi yasifumbiwe macho bali itafutwe njia za kuyaondoa.

Kwa upande, wake serikali imesema itahakikisha mgodi wa madini ya Makaa ya Mawe ya Ngaka unakuwa chanzo kingine muhimu cha uzalishaji umeme nchini.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyasema hayo mapema mwaka huu alipotembelea Mgodi wa Ngaka ambao hisa za Serikali zinawakilishwa na Shirika la NDC.

Ili kufikia lengo hilo, Waziri Muhongo anasema serikali itahakikisha inafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na mgodi huo.

Ameagiza wadau muhimu wa madini hayo ambao ni Kampuni ya TANCOAL, NDC, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, na wananchi wanaozunguka mgodi kukutana ili kujadili na kukubaliana kuhusu masuala kadhaa yakiwemo fidia na uhifadhi wa mazingira.

Profesa Muhongo amevitaka viwanda vilivyoingia mkataba wa mauziano na mgodi huo kuacha kununua madini hayo kutoka nje kwa kuwa makaa ya mawe ya Ngaka yanakidhi viwango na ubora unaotakiwa.

“Nimeelezwa makaa ya Ngaka yana ubora na kiwango cha hali ya juu na nimeelezwa kwamba kuna baadhi ya viwanda vimeingia mkataba na Ngaka, lazima tutumie bidhaa za nyumbani,” anasisitiza Profesa Muhongo.

Anasema ni muhimu kutumia makaa ya mawe kuzalishia umeme kwa sababu gharama zake ni nafuu kwa wananchi na pia umeme huo utachochea ukuaji wa viwanda nchini.

Licha ya madini ya makaa ya mawe kulalamikiwa kuchafua mazingira duniani kote, utafiti umebaini kuwa umeme unaotokana na madini hayo ndio unaotegemewa zaidi na mataifa mengi yaliyoendelea duniani.

Takwimu zinaonesha kuwa makaa ya mawe yanachangia asilimia 41 ya umeme unaozalishwa duniani, umeme wa maji asilimia 16, umeme wa gesi asilia asilimia 20, nyuklia asilimia 15 na umeme wa mafuta kwa kutumia jenereta ni asilimia sita tu kutokana na kuwa umeme ghali.

Utafiti umebaini kwamba miongoni mwa mataifa yaliyoendelea kiuchumi duniani ni yale ambayo yanatumia umeme wa makaa ya mawe.

Mataifa hayo ni pamoja na Afrika Kusini inayotumia asilimia 93 ya umeme wa makaa ya mawe, Poland asilimia 92 na China asilimia 79. Nchi nyingine ni Australia asilimia 77, Kazakhstan asilimia 70, India asilimia 69, Israel asilimia 63, Jamhuri ya Czech asilimia 60, Morocco asilimia 55, Ugiriki asilimia 52, Marekani asilimia 49 na Ujerumani asilimia 46.

Katika kutekeleza Dira ya Taifa ya mwaka 2025 Tanzania inatarajia kuzalisha umeme wa makaa ya mawe ambayo yameenea katika mikoa ya kusini, hususan mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Iringa na Njombe.

Sera Taifa ya Madini ya mwaka 1997 inasisitiza juu ya sekta binafsi kuendeleza madini ambapo serikali katika sera hiyo ina jukumu la kuidhibiti, kuikuza na kuiendeleza sekta hiyo.


Chanzo: http://www.habarileo.co.tz/index.php/makala/16227-makaa-ya-mawe-ya-tanzania-bora-zaidi-duniani


 
02 Juni 2016

NI FEDHEHA KUAGIZA MAKAA YA MAWE KUTOKA NJE

TANZANIA kuna rasilimali kubwa ya makaa ya mawe ambayo mpaka sasa inafikia tani trilioni 1.5. Makaa hayo yapo ukanda wa Kusini mwa Tanzania ambayo ni Mbeya-Kiwira na Ruvuma katika ukanda wa Mto Ruhuhu. Makaa ya mawe ni nishati lakini uzoefu uliopo hayajatumika katika kuchangia upatikanaji wa nishati nchini za viwanda na majumbani.

Upande wa viwandani kuna mtambo mmoja wa Kiwira ndio unazalisha umeme,Vile vile viwandani unatumika kwenye viwanda vya saruji Tanga, Mbeya, kile cha karatasi kilichopo Mgololo na cha Dangote kilichoko Mtwara.

Katika hili nasikitika sana kwa Dangote Kuwa JIPU la kutisha nchini, Wanamkataba TANCOAL kila mwezi Tani 13,500 cha kushangaza tangu kiwanda hiki kimefunguliwa wamenunua Tani 2000 tu,Wanaingiza Makaa ya Mawe toka Afrika kusini na November mwaka jana waliingiza Tani 45,000, Agent akafanya manuva wakaclea mizigo kwa provision clearance wakapewa siku 14 kulipa VAT ama kupeleka msamaha wa kodi amabao kwa taarifa tu walishawahi kupewa na TIC lakini hadi leo daa siku kumi na nne hazijaisha, hawajalipa na hivi sasa Meli ya Makaa ya Mawe yenye Tani 36,000 kutoka Afika Kusini na na Nyingine ya Gypysum Tani 36,000 kutoka Oman bila kibali cha Importation kutoka Wizara husika Nishati na madini,Nasasa wanashinikiza mzigo ushuke Daaa!!

Ukakasi huu na hujuma mbaya kwa Taifa vinaifanya Dangote kuwa moja ya majipu ya kutisha wakisaidiwa na mzawa mwenzetu KAZIMOTO wa Pale PTA akisaidiwa na Wahindi kadhaa na wazawa wengine Majipu.

Nakumbuka Waziri Muhongo alifanya ziara nchi nzima na kuwatambua wachimbaji wadogo wenyeuwezo wa kuzalisha mamilioni ya Madini haya, aliwataka waunde umoja na aliagiza Makampuni haya kununua Madini haya kutoka kwa wazawa kuzalisha ajira na Faida kwa Taifa na alienda Mbali zaidi na kutukumbusha kwamba haya madini yanaubora kuliko madini hayo kwa kiwango kikubwa,TBS sinauhakika juu yenu kwa hili maana sina uhakika kama ukaguzi wa ubora wa bidhaa kwa yale ya November

Je ni kweli Ubora wa Dangote na ahadi zenye neema kwa nchi hasa mikoa ya kusini ndiyo hiyo,Najiuliza juu ya wakala mzawa kuwatetea wawekezaji juu ya kutolipa VAT Jipu hili ni ukakasi kwa Serikali ya Magufuli maana siku mbili tu alipopokea kijiti Amiri jeshi wetu mkuu pale Wizara ya Fedha alifoka kutotoa misamaha ya kodi lakini nakumbuka mwaka jana Bunge letu tukufu lilifuta utoaji misamaha ya VAT kwa wawekezaji wote wa TIC,hawa wawekezaji nchi zote walizowekeza wanalipa Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na wanauwezo wa kulipa.

Gypysum inapatikana kwa wingi pale Lindi inakuwaje wanaagiza kutoka Oman,nawaita Takukuru kuchunguza Majipu ya mawakala wa namna hii,What about our National interest?
Hata hivyo moja ya Dangote kujengwa Mtwara ni matumizi ya Gesi yetu asilia,kupata pesa na kusaidia ajira Ukakasi unaikumba Dangote upande wa ajira pia kunaunyanyasaji na rushwa ya kutisha kupata ajira vinavyo fanywa na HR(Chapalwa).

Takukuru nendeni Pale ni aibu kwa Taifa,Kapwapwa na HR Chapalwa anatumika katika kuwawahujumu waliokosa vigezo kupata ajira ndani ya kiwanda wafunga Tulubai za magari yanayopakia Sementi wanakatwa posho zao malalamiko yako hadi kwa Wenyeviti wa maeneo husika yanayozunguka Majirani wa Aliko Dangote.

Udereva unatoa laki 3 na wafunga turubai wako katika vikundi wanatozwa 5000 kwa kila Lori linapolipa ujira wake wa 15,000 kufungiwa ikumbukwe Kiwanda kinauwezo wa kuzalisha kwa siku Tani 7500 hata kuingiza zaidi ya Maroli 500 kwa siku. Mmoja wa Wenyeviti analalamika anasema Toka wakati wa ujezi HR huyu amehujumu wananchi wetu wengi ni aibu hapa mtu huyu,uliza dada yoyote hapa atakupa sifa zake,Wizi wa Mafuta uliokithiri vinatia doa nchi yetu kwa wawekezaji. Serikali ya Tanzania ilitoa msamaha wa kodi lita zaidi ya milioni 2 kwa Dangote wizi huu kwa siku unaihujumu Dangote lita 1000 kila siku unafanywa na wazawa washirika wa HR Takukuru Mpoo????

Pongezi za dhati kwa Waziri wa Fedha kwa kulinda maslahi ya Taifa na Pongezi Prof. Muhongo kwa kuthamini wachimbaji na kusimamia Taratibu, Sheria na Maslahi mapana ya Taifa Letu baada ya kubaini Jipu hili la Dangote na kuchukua hatua kali dhidi ya hujuma hii kwa Taifa. Sisi Wazawa wachimbaji wadogo wadogo tuko pamoja nanyi tutapigania haki na maslahi ya Taifa letu Tunapongeza juhudi za Rais wetu katika Vita dhidi ya Rushwa, ubadhirifu vilivyolitafuna Taifa letu kwa kiwango kikubwa.

Source : Ni aibu na fedheha kwa Tanzania kuagiza nje makaa ya mawe na gypsum
 

15 October 2019​

WAZIRI BITEKO AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUJADILI CHANGAMOTO ZA MAKAA YA MAWE​


3ce44192-1bcd-470d-99b9-a82850024a1a.jpg


Viongozi wa Makampuni ya Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake Cement Ltd wakimsikiliza Waziri wa Madini Doto Biteko walipokuwa wakijadiliana changamoto za bei ya Makaa ya Mawe jijini Mwanza.
85ea1734-140f-4b0f-8660-88bd0f17c72d.jpg


Waziri wa Madini Doto Biteko akisalimiana na Viongozi wa makampuni ya Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake Cement Ltd.
91d03731-5c0c-46f6-891b-bb4eabecd614.jpg


Waziri wa Madini Doto Biteko akiwafafanulia Viongozi wa makampuni ya Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake Cement
Ltd kuhusu utaratibu wa bei za Makaa ya Mawe.
697537b8-97a7-4925-910a-00fab491433b.jpg


Waziri wa Madini Doto Biteko akiwasikiliza Viongozi wa makampuni ya Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake Cement
Ltd, kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza Fredy Mahobe Na Tito Mselem, Mwanza

Waziri wa Madini Doto Biteko amewatoa wasiwasi Wawekezaji wa Viwanda vinavyotumia Makaa ya Mawe na kuieleza Kampuni
inayochimba Makaa ya Mawe ya TANCOAL kuwa hairuhusiwi kuongeza bei kiholela badala yake inatakiwa kuuza kulingana na bei elekezi
iliyopangwa na serikali.

Kauli hiyo ilitolewa Septemba 15, 2019 na Waziri Biteko baada ya kukutana na wawekezaji wa Viwanda vya Saruji na Vigae kujadili changamoto za Makaa ya Mawe katika kikao kilichofanyika katika Ofisi
ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza.

Katika Kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Biteko, kilihudhuriwa pia na
Mkurugenzi wa huduma za Leseni wa Tume ya Madini Mhandisi,Yahaya Samamba, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mwanza Fredy Mahobe, Afisa Kodi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Venance Kasiki pamoja
na wawekezaji wa viwanda vya Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake Cement Ltd.

Kampuni hizo tatu za Tanga Cement, Kada (T) Ceramics Company pamoja na Lake Cement Ltd. zinatumia kiasi kikubwa cha Makaa ya
Mawe kwa matumizi ya kuyeyushia Mawe kwa ajili ya uzalishaji wa saruji na vigae ambapo zaidi ya nyuzi joto 2000 zinatakiwa ili kuyeyusha
Mawe hayo ziliomba kukutana na Waziri wa Madini ili kueleza
changamoto zao.

Hatua hiyo ilikuja kutokana na wanunuzi wakubwa wa makaa yam awe nchini kuwa na mvutano wa bei ya Makaa ya Mawe kati yao na mzalishaji wa Makaa hayo kampuni ya TANCOAL anayozalisha Mawe
hayo katika eneo la Kitai Mkoani Ruvuma katika Mgodi wa Ngaka.

Mvutano huo ulianza mara baada Serikali kupitia Tume ya Madini Kuitaka Kampuni ya TANCOAL Kulipa deni lake la kiasi cha shilingi Bilioni 23.9 ambazo zilitokana na malimbikizo ya kutolipa mrabaha wa mauzo na usafirishaji wa Makaa hayo pamoja na adhabu ya asilimia 50 kuanzia Septemba 2011 mpaka Juni 2019.

Aidha, Waziri Biteko amezitaka kampuni hizo kuendelea na uzalishaji wa Saruji na Vigae bila kuhofia kupandishiwa bei kwa maana bei hazitapanda kiholela, ameeleza kuwa, Makaa ya Mawe kote nchi yatauzwa kulingana na bei iliyo elekezwa na serikali.

Imeonekana kwamba, deni la kampuni ya TANCOAL kuwa kubwa, kampuni hiyo imeonesha nia ya kupandisha bei kwanye Makaa ya Mawe ili kufidia deni wanalodaiwa na Serikali.

Kwa upande wake, Mdhibiti wa Fedha wa Tanga Cement, Issac
Lupokela alimweleza Waziri Biteko kuwa, kitendo cha kupandishiwa bei na kampuni ya TANCOAL ni kama wanawaadhibu kutokana na ukweli kwamba hakuna mbadala wa kununua kwa wingi sehemu ingine makaa
hayo baada ya serikali kusitisha uingizwaji wa Makaa ya Mawe nchini.

“Kipindi cha Nyuma tulikuwa tunanunua Makaa ya Mawe kutoka Afrika ya Kusini kwa kuwa Makaa yaliyokuwa yanazalishwa nchini hayakuwa
na kiwango cha kutosha hivyo baada ya serikali kusitisha uingizwaji wa Makaa ya Mawe nchini, tulilazimika kushirikiana na kampuni ya TANCOAL ili kutoa elimu ya namna bora ya uzalishaji wa Makaa hayo,
leo tunashangaa wameamua kutupandishia bei,” alisema Lupokela.
 
Hakuna crisis yoyote ya umeme iliyoripotiwa mkoani Tanga, iweje itokee Kwa kiwanda kimoja? Una uhakika tatizo ni TANESCO? Tafuta habari iliyobalance kuliko kuleta uwongo uwongo JF.
Weka taarifa rasmi kutoka kwenye menejimenti ya kiwanda hicho umma ujiridhishe.
Haya ni maelezo kutoka uongozi wa kiwanda live kwenye taarifa ya habari UTV sasa wewe unataka kubalance kitu gani?tatizo siku hizi mnajibebesha mizigo yaani taasisi isipofanya vizuri isisemwe eti kwa sababu tu mnaiunganisha na serikali.kila mtu asemwe upande wake
 
Ikivuma sana hupasuka.

Sasa mambo yameanza kubumbuluka. hakuna kuficha maradhi.
 
Back
Top Bottom