Kiwanda cha Cement Tanga chasimamisha uzalishaji kutokana na ukosefu wa umeme

Kiwanda cha Cement Tanga chasimamisha uzalishaji kutokana na ukosefu wa umeme

NINI KINAKWAMISHA UPATIKANAJI WA MAKAA YA MAWE YA KUTOSHA KUZALISHA NISHATI ? ILI TATIZO HILO LIWE HISTORIA

Kwa miaka mingi mawaziri kuanzia Prof. Sospeter Muhongo, Dr. Medard Kalemani, Dr. Doto Bitego, January Makamba wamekuwa wakiongoza mapambano kutafuta muarobaini, vikao kazi vya viongozi wa mawizara na sekta ya viwanda kujadili mikakati, kuweka mpango kazi endelevu na kufika katika maeneo husika ya wazalishaji mkaa na yale ya watumiaji makaa ya mawe ili kila kitu kiende sawa lakini mpaka leo 2022 bado kuna tatizo la upatikanaji wa nishati kupitia makaa ya mawe!
 
Taarifa ya habari ya UTV imeripoti leo magari ya kubeba cement yamekwama kwa zaidi ya siku saba kwa ukosefu wa mzigo wa cement kutokana na kusimama uzalishaji.

TANESCO imeshindwa kutoa umeme wa kutosha kwa uzalishaji na meneja wa kiwanda amedai wanatumia zaidi ya milioni 500 kwa mwezi kununua dizeli ambayo pia yanasaidia uzalishaji kidogo kwa ajili ya miradi ya kimkakati. Je, kwanini uongozi wa Tanesco usiadhibiwe kwa kushindwa kuondoa hili tatizo?

Kwa hali hii kweli tuko serious kuita wawekezaji kuanzisha viwanda nchini? Kwa nini haya matatizo ya TANESCO yamekuwa mengi katika siku za karibu?
Sijaelewa, kwamba umeme hautoshi Tanzania au miundo mbinu ya kuupeleka hujo kwenye kiwanda ndio hautoshelezi, naomba ufafanuzi
 
Hakuna crisis yoyote ya umeme iliyoripotiwa mkoani Tanga, iweje itokee Kwa kiwanda kimoja? Una uhakika tatizo ni TANESCO? Tafuta habari iliyobalance kuliko kuleta uwongo uwongo JF.
Weka taarifa rasmi kutoka kwenye menejimenti ya kiwanda hicho umma ujiridhishe.
 

13 Jan 2016​

UMEME WA MAKAA YA MAWE LAZIMA: Prof. Muhongo​



Serikali imesema itahakikisha inafanya Makaa ya Mawe yanakuwa chanzo kingine kikubwa cha uzalishaji umeme Nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alipotembelea Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka unaomilikiwa kwa ubia Kati ya Kampuni ya TANCOAL na Serikali kupitia shirika la NDC. Mgodi huo upo katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Aidha, ili kufikia lengo hilo ,Prof. Muhongo amesema Serikali itahakikisha inafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Mgodi huo ambao Serikali ina umiliki wa hisa ya asilimia 30 kupitia Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) ili kuimarisha uchumi wa taifa kupitia Makaa ya Mawe.

Ameongeza kuwa, ili kuhakikisha kwamba Kampuni ya TANCOAL inaendelea kuzalisha makaa na kutumiwa na viwanda vya ndani, Prof Muhongo amevitaka viwanda vilivyoingia Mkataba wa mauziano na mgodi huo kuacha kununua Makaa kutoka nje ikiwa makaa ya Ngaka yanakidhi viwango na ubora unaotakiwa.

"Nimeelezwa Makaa ya Ngaka yana ubora na kiwango cha hali ya juu na nimeelezwa kwamba kuna baadhi ya viwanda vimeingia mkataba na Ngaka lakini badala yake wananunua makaa kutoka nje. Hilo halikubaliki ikiwa makaa ya ndani ya nchi yana ubora lazima tutumie bidhaa za nyumbani,"amesisitiza Prof. Muhongo.

Kutokana na malalamiko ya Mgodi kuhusu hali ya Mkataba ya kuuziana makaa kutoafikiana, Waziri Muhongo ameutaka mgodi huo,NDC,EWURA, Kampuni za Saruji za Dangote, Tanga Cement na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kukutana Makao Makuu ya Wizara tarehe 14 Januari,2016, ili kujadili kuhusu suala hilo na pia kujadiliana juu ya gharama za kuuziana umeme na TANESCO pindi mgodi huo utakapoanza kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe.

" Umeme wa makaa ya mawe Tanzania ni lazima. Tutapigana kufa na kupona kuhakikisha tunazalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe kwa sababu gharama zake zitakuwa nafuu kwa wananchi na pia umeme huu utachochea ukuaji wa viwanda nchini," amesisitiza Prof. Muhongo.

Kadhalika Prof. Muhongo amerejea kauli yake ya kuwataka wazalishaji umeme hususan wa makaa ya mawe na vyanzo vingine kuhakikisha wanaiuzia TANESCO umeme wa bei ya chini na kuongeza "mauziano ya umeme wa makaa ya mawe lazima yafuate viwango vya kimataifa. Lazima yawe ya gharama nafuu."

Katika hatua nyingine, Prof. Muhongo amewataka EWURA kubadilika na kushiriki katika hatua za mwanzo za majadiliano ya gharama za kuuziana umeme katika utekelezaji wa miradi mbalimbali badala ya kusubiri kushiriki katika hatua za mwisho na kulieleza jambo hilo kuwa ushiriki wao katika hatua za awali unawezesha majadiliano na makubaliano kufanyika kwa haraka.

Aidha, Prof. Muhongo amechukua fursa hiyo kuzitaka Mamlaka chini ya wizara kuzingatia suala la usawa na namna Serikali inavyonufaika na makubaliano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kitaifa kwa kuzingatia kuwa rasilimali ni za nchi , hivyo taifa linapaswa kunufaika na uwekezaji husika.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko wa mgodi wa Ngaka, Christopher Temba, mgodi huo unazalisha tani za makaa ya mawe Laki Tano kwa mwaka lakini lengo ni kufikia tani milioni moja.

Tayari makaa hayo yanasafirishwa katika nchi za Kenya, Zambia, Malawi na vilevile katika viwanda kadhaa hapa nchini vikiwemo vya Saruji Tanga Mohamed Enterprises na viwanda vingine


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na baadhi ya watendaji wa Mgodi wa Makaa ya Mawe ya Ngaka mara baada ya kuwasili katika mgodi huo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoa wa Ruvuma. Wengine ni ujumbe aliofuatana nao pamoja na Mbunge wa Mbinga vijijini, Martin Msuha, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga, Kamishna Msaidizi wa Madini, anayeshughulikia Leseni John Nayopa, Watendaji toka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa Nyasa, baadhi ya Maafisa toka Wizara ya Nishati na Madini na EWURA.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo, (kulia) akiwasikiliza wawakilishi wa wananchi wa Kijiji cha Mtundualo, Wilaya ya Mbinga ambao walimwomba waziri asikilize malalamiko yao ikiwemo kuhusu suala la fidia kupisha mradi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka na ombi la kijiji hicho kupatiwa umeme. Kwa mujibu wa Meneja wa Tanesco Kanda ya Kusini, Joyce Ngahyoma, amewahakikishia kuwa ifikapo mwezi Aprili mwaka huu kijiji hicho kitakuwa kimeunganishwa na nishati ya umeme.

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga, akijadiliana jambo na baadhi ya Watendaji wa Mgodi wa Ngaka kampuni ya TANCOAL, mara baada ya waziri kukagua shughuli za mgodi huo na kusikia malalamiko ya wananchi kuhusu fidia. Waziri Muhongo amezitaka pande mbili kati ya Kampuni, Halmashauri na wananchi kukutana ili kujadili na kukubaliana kuhusu masuala kadhaa yakiwemo fidia na uhifadhi wa mazingira.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akimsikiliza Mwendeshaji Mitambo wa kituo cha kufua umeme cha Tulila kinachomilikiwa na Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole, Sister Maria Katani (OSB),. Wengine wanaofuatilia nia Meneja wa Tanesco Kanda ya Kusini, Joyce Ngahyoma na Afisa toka Wizara ya Nishati na Madini, Christopher Bitesirigwa.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisalimiana na Mfadhili wa Kituo cha Kufua umeme kinachomilikiwa na Watawa wa Shirika la Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole, Albert Cock (kushoto). Kituo hicho chenye uwezo wa kuzalisha kilowati 800 kipo Kata ya Magarura, wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma. Aidha, sehemu ya umeme unaozalishwa na kituo hicho unasambazwa Songea, JKT Mlale na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale. Vilevile, Kituo hicho kipo katika hatua za ujenzi wa kituo kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha megwati 7.5.

Meneja wa Tanesco Kanda ya Kusini, Joyce Ngahyoma akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati alipotembelea kituo cha mwekezaji binafsi cha Kufua umeme kinachomilikiwa na Familia ya Andoya, Wilaya ya Mbinga. Mradi huo wa Mbangamao unazalisha megawati 0.2, huku malengo ni kufikia megawati 2. Anayemsikiliza nyuma yake ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Ruvuma, Patric Lwesya, wengine ni ujumbe uliofuatana na Waziri.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja na Watawa wa Shirika la Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole, Mfadhili wa Kituo hicho cha kufua umeme Albert Cock, ujumbe aliofuatana nao wakiwemo Maafisa toka Wizara ya Nishati na Madini, EWURA, Shirika la Umeme Nchini, Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Uongozi wa Wilaya ya Mbinga, Mbunge wa Mbinga Vijijini Martin Msuha, Uongozi wa Kijiji, Wakandarasi wanaojenga kituo cha kuzalisha umeme cha megawati 7.5, na baadhi ya wananchi wanaozunguka eneo hilo.

Baadhi ya Maafisa Kutoka Wizara ya Nishati na Madini (Mbele) na ujumbe uliofuatana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (nyuma) kutembelea kituo cha Kufua umeme cha Tulila kinachomilikiwa na Watawa wa Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole,wakiangalia maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Bwawa la kufua umeme. Imeelezwa kuwa, kukamilika kwake kutawezesha uzalishaji wa umeme wa kiasi cha megawati 7.5.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, katika picha ya pamoja na Watawa Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole na Mfadhili wa Kituo hicho Albert Cock.

Source : SOSTENES LEKULE JR at January 13, 2016

 
HeidelbergCement further strengthens business in Tanzania
26 October 2021

HeidelbergCement has signed an agreement to acquire 68 % of the shares in the Tanzanian cement producer Tanga Cement. With this step, the company further strengthens its local business and creates significant synergies with its existing assets in Tanzania.

Through its subsidiary Tanzania Portland Cement, the largest cement producing company in the country, HeidelbergCement already has a good market position in Dar es Salaam in the Eastern part of Tanzania. As part of this transaction, HeidelbergCement secures an important limestone quarry with measured resources for at least 30 years on top of its already existing reserves. The quarry and the associated cement plant with a capacity of 1.3 millions tonnes of Tanga Cement are located in the Northern part of Tanzania.

The closing of the transaction is subject to the fulfillment of customary conditions precedents (especially the clearance by several local authorities), which have to be fulfilled or waived within an agreed timeframe. As of today, closing of the transaction is expected in the second quarter of 2022. Upon closing, HeidelbergCement will make a public tender offer to acquire the remaining outstanding shares in Tanga Cement, following Tanzanian law and in alignment with the respective local authorities.

Both companies, Tanzania Portland Cement und Tanga Cement, are publicly listed.

About HeidelbergCement
HeidelbergCement is one of the world’s largest integrated manufacturers of building materials and solutions, with leading market positions in aggregates, cement, and ready-mixed concrete. Around 53,000 employees at more than 3,000 locations in over 50 countries deliver long-term financial performance through operational excellence and openness for change. At the center of actions lies the responsibility for the environment. As forerunner on the path to carbon neutrality, HeidelbergCement crafts material solutions for the future.
Christoph-Beumelburg.jpg

Christoph Beumelburg​

Group Spokesman, Director Group Communication & Investor Relations
Source : HeidelbergCement further strengthens business in Tanzania
 
Taarifa ya mbia mkubwa wa kiwanda cha cement Tanga aliye na hisa 68 % ni kuwa hali ya biashara kwa ujumla imekuwa nzuri kwa kundi la makampuni Heidelberg Cement Group na kuwa soko siyo tatizo kwani kuna mahitaji makubwa ya cement duniani. Mbali ya changamoto za ughali wa uendeshaji na MaliGhafi. Hivyo kama kundi / group la makampuni tunajivunia taarifa hiyo ya mwaka 2021.

24 February 2022

HeidelbergCement’s CEO talks about the successful business year 2021



2021 was a successful year for HeidelbergCement - despite significant cost headwind. Our CEO Dr. Dominik von Achten is proud on the improvements in all key performance indicators.

Source : HeidelbergCement Group
 
Ludewa, Njombe
Tanzania

18 January 2022​

Makaa ya Mawe Ludewa rasmi kuanza kusafirishwa / mkaa upo wa kutosha / Fursa za kutosha kwa vijana.​



Miundombinu kwenda machimbo ya makaa ya mawe
Mradi wa makaa ya Mawe Ludewa chini ya kampuni ya Maxcoal umekamirika Sasa rasmi kuanza kusafirishwa / transporters wanakaribishwa kuleta Magari ya kubeba mkaa huo mkaa upo wa kutosha Fursa za ajila za muda na za kudumu zinapatikana Fursa za biashara pia zipo

Source : em onlinetv
 
Ludewa, Njombe
Tanzania

18 January 2022​

Makaa ya Mawe Ludewa rasmi kuanza kusafirishwa / mkaa upo wa kutosha / Fursa za kutosha kwa vijana.​



Miundombinu kwenda machimbo ya makaa ya mawe
Mradi wa makaa ya Mawe Ludewa chini ya kampuni ya Maxcoal umekamirika Sasa rasmi kuanza kusafirishwa / transporters wanakaribishwa kuleta Magari ya kubeba mkaa huo mkaa upo wa kutosha Fursa za ajila za muda na za kudumu zinapatikana Fursa za biashara pia zipo

Source : em onlinetv

Kwahiyo mnawanyima umeme ili wanunue makaa ya mawe?
 
Kwahiyo mnawanyima umeme ili wanunue makaa ya mawe?
Hawajui kuwa hayo makaa ya mawe kufika Tanga inahitaji malori mengi ambayo inajumuisha matumizi makubwa ya mafuta hivyo gharama za usqfirishaji qmbazo zipo juu kutokana na bei ya mafuta kupanda itaenda kuathiri bei ya cement kwa mlaji wa mwisho
 
SEKTA YA MAKAA YA MAWE NA CHUMA INAHITAJI KUPELEKEWA KIPANDE CHA RELI

Sekta ya makaa mawe na chuma inatakiwa vipelekewe reli haraka badala ya malori kusafirisha makaa ya mawe zaidi ya kilometa 300.


Reli ikijengwa kuelekea ktk machimbo hayo kisha makaa ya mawe kusafirishwa kwa reli kwa mzigo mkubwa mwingi kwa bei nafuu ya usafiri kwenda DSM, Tanga, Mtwara pia Taveta kwa soko la Kenya, Tazara kwa masoko ya kusini mwa Afrika kutaweka makaa ya mawe ya Tanzania kuvutia watumiaji wote wa ndani na nje ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom