Kiwanda cha Coca Cola kinauza soda chafu

Unakunywa soda ili iweje...?
Bora hiyo mbao uliyoikuta kuliko hizo kemukali na sukari ya soda
 
Soda waachiwe watoto, mtu mzima kunywa soda ni kufuru.
 
Miaka ya nyuma huko kuna mtu aliwahi kukuta nywele, nadhani naye pia aliwashtaki. Nimewahi kufanya utafiti mdogo kwa kuuliza wakati nafanya kazi ya muda hapo cocacola kwanza, niliambiwa tatizo sio soda bali ni chupa kutokana na utunzaji.

Kuna baadhi ya vitu wakati wa kusafisha vinashindwa kutoka na kama hakuna atakayeona basi soda inajazwa , kufungwa na kusafirishwa hadi sokoni. Ilitakiwa wenye depot wakague maana wakati mwingine kiwandani wanakuwa na kazi nyingi. Akiikagua chupa na kukuta itilafu yoyote anarudisha kiwandani.

Wito wangu ni kwa baadhi ya wateja wanaotumia soda za chupa wajitahidi kuzitunza vizuri. Wengi wanazihifadhi vibaya utadhani hatatumia tena. Na ndio maana binafsi sipendi sana kutumia soda za chupa
 
Na mimi nimeamua kuacha soda Mkuu,
 
tanzania ndio nchi chupa za soda zinarudishwa ila kwa wenzetu chupa za soda au bia zinatupwa na kurudishwa kiwandani kusagwa kwa ajili ya kutengeneza chupa mpya
Ungetaja na nchi kabisa
 
Na mimi nimeamua kuacha soda Mkuu,
Tatizo sio soda. Labda kama utaacha kwa sababu za kiafya.

Tatizo kubwa ni utunzaji wa chupa. Watu wengi kwenye nchi yetu hawana ustaarabu ktk kutunza vitu vinavyoweza kutumika mara kwa mara na watu wengine.

Mfano utakuta mtu anaweka vitu mahali pasipofaa na wala hajali kama atatumia tena.
Vyuoni kuna tabia hii sana. Wanachuo tena wasomi, wanatumia sahani za canteen wakimaliza wanaziacha nje kwenye mifereji na kama wahudumu hawajaziona maana yake ni kwamba zitalala hapo na pengine kulambwa na mbwa au paka.

Sasa hapo labda uamue kununua chombo binafsi au cha take away kama utajisikia vibaya kutumia tena sahani kutokana na hisia (tujue watu unatofautiana hisia)

Hata hivyo elimu ya utunzaji wa mali ya umma na hata binafsi, inahitajika sana!
 
Propaganda za kizamani kabisa za kuharibu biashara za watu, stop that hiyo siyo njia sahihi ya USHINDANI WA KIBIASHARA.
 
siku nyingine tafuta namba zao wapigiye uwajulishe kabla ya haya,mimi niliwahi kuona vichembe vya uchafu kwenye maji ya kitulo nikawapigia kabla ya kufungua wakasema nipeleke niliponunuwa wakanibadilishia.
 
Propaganda za kizamani kabisa za kuharibu biashara za watu, stop that hiyo siyo njia sahihi ya USHINDANI WA KIBIASHARA.
Mkuu una akili timamu ? Niharibu biashara ya watu ili nifaidike nini masikini kama mimi ? ,Sina interest yoyote na post hii
 
Inawezekana ikawa kweli maana hiko kimbao haiwezekani kwamba kiliwekwa kiwandani sababu kimewekwa kwa makusudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…