Kiwanda cha sabuni vs kiwanda cha maji

Kiwanda cha sabuni vs kiwanda cha maji

Mzee uta pata ng'ombe 1 wa maziwa, Kumbuka sisi ni familia😄.
👉Hapo kwenye share holder nime cheka kwa sauti😄😄, Ime bidi nika angalie umiliki wa bakhresa kweenye soko la hisa.

Nika gundua ana miliki asilimia 3, kwenye soko la hisa, na kawekeza mkwanja mrefu.
👉Afu we ushauri tu, una taka upate kizembe , 🤔😂😁.
👉Nisamehe🙏🙏, mjukuu wako bahili🏃🏃🏃
Hahahaha.................kumbuka kupitia report yangu nitakayokuandalia itakusaidia kutopoteza Mtaji kwenye huo Uwekezaji utakaoufanya.

Kwa lugha rahisi, kupitia andiko langu kutafanya uzalishe mabilioni mengine mengi.

Fanya mpango Babu yako nipate hela za kunifanya niongeze dogodogo wa kunifanya nisife haraka Kwa baridi kama Mfalme Daudi Siku za Uzee wake 😜
 
Tuta ona mzee, acha tuendelee kupambania Malengo.
 
Mkuu Utafanikiwa! Japo vita yake sio ndogo maana shetani Mpuuzi sana ameshaliona kuwa unataka kuja kufanya nini na utakua nani anajua kwahiyo atakuja na vipingamizi vya kukukatisha tamaa.

Liweke pia jambo lako kwenye Maombi au Dua kama ni muislamu.
Pamoja mkuu, nita zingatia hilo.
 
Nashindwa kutoa maoni Concrete as Kuna taarifa za msingi zinakosekana kwenye andiko lako.

Ila unapotaka kufanya biashara ambayo tayari ipo (already existing business) unatakiwa kuangalia weakness za washindani wako Kwa kuangalia wapi wamekosea upande wa quality/quantity/market/brandings n.k

Hujasema unataka kufanya at which horizons i.e small scale/medium/large

Kwa kutumia uzoefu naweza kushauri kuhusu biashara ya Maji ambayo haihitaji gharama kubwa za Uendeshaji (O&M) zaidi ya gharama za madawa kwaajili ya kutibu as Maji yanapatikana kiurahisi ambapo unaweza kuyanunua kwenye Mamlaka za Maji iwe DAWASA/MWAUWASA/MORUWASA n.k

Ili ku-penetrate Soko hakikisha unakuwa na packaging nzuri na Maji yawe mazuri. Mikoa ya Mbeya/Iringa/Morogoro/Mwanza/Ruvuma Wana Maji matamu sana

Kama upo serious na biashara moja wapo ya hizo mbili niajiri nikufanyie tathmini ya kina na kuja chaguo sahihi.

Maana factors za kufikia kwenye Chaguo sahihi zipo nyingi ambapo upembuzi wa kina unahitaji.

Kila la heri Bilionea ujaye wa Kitanzania [emoji120][emoji123][emoji109]
Maji lazima ununue mtambo wa reverse osmosis.
 
Binafsi katika harakati za maisha ya ujobless nimefanya kazi za hapa na pale, mojawapo nilikuwa kiraka mmoja mdogo kwenye ujenzi wa kiwanda cha Tajiri mmoja hapa nchini. Kwa hiyo hapa ni uwanja wangu wa nyumbani

Kaa kwa kutulia, nitaelezea vile navyokumbuka.

Naenda moja kwa moja kwenye mada. Hizo ni link za viwanda vya kutengeneza mashine

Nafanya assumption wewe ni Tajiri una mabilioni yako unataka kuwekeza.

1. Tafuta ardhi kwa ajili ya kujenga kiwanda (light industry, medium industry, heavy industry). Ukubwa kuanzia 5000sqm mpaka 10,000sqm mpaka 50,000sqm na zaidi inategemea na ukubwa wa mtaji. Viwanja vinauzwa idara ya ardhi Kwenye mkoa, wilaya, halmashauri, au TIC. Bei inacheza kati ya 5000@sqm mpaka 30,000@sqm mpaka 100,000@sqm. Zingatia pawe location nzuri, pawe na Barabara, umeme, maji. Pasiwe na mafuriko au hali mbaya.

2. Uwe na pesa ya kujenga hicho kiwanda kujenga fence, kujenga magodown makubwa angalau matatu na ofisi ya wafanyakazi au hostel. Magodown yanapaswa kuwa marefu kwenda juu na sakafu kubwa unakuta dude lina mita 20 kwa 20 kwa ndani au mita 25 kwa mita 40. Unaweza kujenga kwa tofali au au chuma kisha ukavisha bati. Huo ukubwa wa sakafu inategemea na ukubwa wa mtambo utakaofunga, store ya malighafi, store ya bidhaa zilizozalishwa na sehemu ya magari au malori kupakia bidhaa zilizozalishwa. Michoro inabidi ikidhi vigezo vya TBS, ISO, ERB, OSHA, FIRE na vibali vingine mbalimbali.

3. Uwe na pesa ya kununua mtambo wa uzalishaji wa bidhaa na raw materials za kuzalisha bidhaa. Inabidi usajiliwe na TIC angalau upate punguzo la kodi Bandarini. Kwa uzalishaji wa maji inabidi uwe na chanzo cha maji cha uhakika kisima, bomba, chemchemi n.k mtambo mdogo full unaanzia $50,000 mpaka $100,000. Ya wastani $200,000 mpaka $800,000. Mikubwa $1m mpaka $5m mpaka $10m. Inabidi uwe na pesa za kununua mitambo, kulipia kodi Bandarini, kulipia usafiri wa mitambo toka Bandarini mpaka kiwandani, kulipia wachina nauli na posho ya kufunga mitambo na kufundisha wafanyakazi wako. Na kutest mitambo kama inafanya kazi na kuzalisha. Mitambo inategemea na mtaji, kuna mitambo ya China, india, Uturuki, Ulaya, Marekani n.k

4. Uwe na pesa ya kuvuta huduma za kijamii kwenye kiwanda chako, kama umeme,maji n.k

5. Uwe na pesa ya kuajiri na kulipa mishahara wafanyakazi wako utakao waajiri.

6. Uwe na hela ya kukiendesha kiwanda bila ya kuzalisha hela kwa muda angalau kuanzi miezi mitatu mpaka 6.

7. Uwe na hela ya kuitangaza bidhaa na kuisambaza bidhaa yako ili iwafikie wateja. Pia uwe na mtandao wa wanunuzi wa jumla au maagent wa bidhaa yako. Uwe na malori au usafiri wa kufikisha bidhaa kwa wateja.

Pesa inawekezwa ya kutosha. Sio poa.

Ukisikia mtu ana kiwanda muheshimu.
 
Asante mkuu, jobless nime kusoma vyema.
👉Ngoja tusubiri labda Dreams LLC ana kitu Cha ziada🙏
 
Back
Top Bottom