Kiwanda cha Tommy Dairy bado kipo?

Kiwanda cha Tommy Dairy bado kipo?

Showme

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
1,251
Reaction score
498
Habarini za kutwa

Kuna kiwanda tajwa hapo juu kilikuwepo maeneo ya Kimara, naomba kufahamu kama bado kipo na kama kipo kipo maeneo gani yaani Kimara ipi na kama kuna yeyote ana mawasiliano na mfanyakazi yeyote kwenye kiwanda hicho naomba aniunganishe nae tafadhali.
 
Jamaa nadhani amefilisika, lakini ingekuwa nchi za wenzetu au rangi ya kina Bakhressa jamaa sasa hivi angekuwa Billionaire.

Nakumbuka alivyosambaza vibanda vya maziwa ndivyo pia Bakhresa alianzaga na vibanda ya kuuza ice cream (koni)
 
Kilishakufa zamani

Sijui kama Thomas lyimo kama yupo bado

Tulikunywa maziwa yake sana enzi zile tuko shule ya msingi.

Nimesoma karibu na kiwanda

"Maziwaaa halisiii ya tommy dairy..enhee!! Yana sukariii,..enhee!! yana vitamini...yananenepesha..mshikirika utakua kua.[emoji444][emoji445]
 
Ok Thomas Lyimo itakuwa ndio mmiliki wa hotel pale kwenye mataa ya Akiba kwenye shule ya msingi Mtendeni opp na brach ya Azam.
 
Jamaa nadhani amefirisika, lakini ingekuwa nchi za wenzetu au rangi ya kina Bakhressa jamaa sasa hivi angekuwa Billionaire.

Nakumbuka alivyosambaza vibanda vya maziwa ndivyo pia Bakhresa alianzaga na vibanda ya kuuza ice cream (koni)
Tanzania yetu
 
Kilishakufa zamani

Sijui kama Thomas lyimo kama yupo bado

Tulikunywa maziwa yake sana enzi zile tuko shule ya msingi.

Nimesoma karibu na kiwanda

"Maziwaaa halisiii ya tommy dairy..enhee!! Yana sukariii,..enhee!! yana vitamini...yananenepesha..mshikirika utakua kua.[emoji444][emoji445]
Yupo hai anakula kodi za majumba yake Kariakoo gerezani
 
Huyo ankoli tulikuwa tunafanya jogging nae halafu inaishia kiwandani kwake

Kisha tunapewa packet za maziwa tunarudi nyumbani

Nashangaa sijui niliwezaje kupata ujasiri wa kukimbia umbali ule kisa Maziwa.!? Utoto raha
 
Back
Top Bottom