Kiwanda gani naweza fungua/anzisha kwa gharama ya millioni nne?

Kiwanda gani naweza fungua/anzisha kwa gharama ya millioni nne?

Hata ukiweka korona ukaanza kukamua miwa ni kiwanda pia mkuu na kwa mtaji huo ni safi
 
Kwa wadogo zetu mnaokua na watu wazima ambao bado akili zinakua tungependa kuwaarifu kuwa sisi tunajua kuandika utani na pumba zaidi yenu lakini tufahamu tuandike wapi na wakati gani, kuna majukwaa mengi ya utani lakini when it comes to business kuweni na adabu tafadhali
 
Binafsi ni muumini wa kilimo na Teknolojia. Najaribu kuwaza kiwanda gani naweza kununua au kutengeneza kwa gharama ya millioni nne za kitanzania angalau kije kufunguliwa na kiongozi wangu wa mtaa.

Kiwanda chochote cha kuongeza thamani bidhaa za shamba au asili.

Naamini hakuna ambacho kimewahi shindikana humu.

Msaada please.
Pata ushauri kutoka kwa mkulu, atakuja kukifungia mwenyewe.
 
Kwa kiwango cha pesa ulicho nacho nakushauri ufanye kati ya biashara zifuatazo:
1. Nunua mashine za kutengeneza peanut butter. Mashine hizo ni peanut grinder, peanut roster na meza ya kufanya sorting. Hiyo hela itatosha na utabakiwa na kiasi fulani cha kunjnua raw materials (karanga) za kutosha za kuanzia.

2. Biashara ingine nunua mashine ya kusaga na kukoboa unga wa mahindi na uwe unapaki. Mashine hizo fanya zitumie motor moja ku run mashine zote mbili ili kuokoa gharama. Hapa sidhani kama utakuwa na hela ya materials ya kuanzia.

Pia kwenye case zote mbili nime assume utakuwa na shed ya kuweka hizo mashine.

Kila la heri
Nimekuwa interested na peanut butter ila changamoto naona iko kwenye bidhaa kuweza kupenyeza sokoni pamoja na vibali kama vya TFDA na TBS. Nahitaji mwanga zaidi.
 
Anzisha kiwanda cha kutengeneza unga wa nazi.unakausha zile nazi halafu unazisaga.halafu unazitia kwenye paketi.hakikisha paketi haiingizi hewa ndani ili huo unga usiharibike.hapo utatafuta kampuni ikutengenezee hizo paketi.halafu uzipige nembo yako. Kuna watu wengi hawana mda wa kukuna nazi hivo utapata wateja wengi tuu hata nje ya tz utauza.na machine unayohitaji kwa kuanzia ni moja tu ya kusaga.
 
Nimekuwa interested na peanut butter ila changamoto naona iko kwenye bidhaa kuweza kupenyeza sokoni pamoja na vibali kama vya TFDA na TBS. Nahitaji mwanga zaidi.
Hakuna ugumu wowote. Kwa kuanzia tbs utaiomba kupitia sido ni mchakato rahisi sana na kulipa fee kidogo sana. Tfda hawana complication unafuata tu masharti yao na kulipa gharama kidogo.

Wengi wanaogopa bila kujaribu
 
Dah.... Angalia hitaji LA soko kwanza..... Usijerudi unalialia hapa[emoji87] [emoji41]
 
Kwa wadogo zetu mnaokua na watu wazima ambao bado akili zinakua tungependa kuwaarifu kuwa sisi tunajua kuandika utani na pumba zaidi yenu lakini tufahamu tuandike wapi na wakati gani, kuna majukwaa mengi ya utani lakini when it comes to be business kuweni na adabu tafadhali

Aisee bora hata umesema mkuu, kuna watu wanamambo ya kitoto sana. Tuwe na tabia ata ya kujionea aibu wenyewe haiwezekani mtu anaandika ujinga sehemu kama hii ambayo mtu unaweza ukapata jambo linaloweza kukusahidia.

Id fake na kutokujulikana kusifanye tuwe wapuuzi JF si humu ni watu wazima.

Wanakera sana
 
Back
Top Bottom