Kiwanda gani naweza fungua/anzisha kwa gharama ya millioni nne?

Kiwanda gani naweza fungua/anzisha kwa gharama ya millioni nne?

Napenda nachokisoma kwenye huu uzi watu bila choyo wanatupa technique za maisha safi sana huu ndio undugu wa Afrika tunatakiwa kuwa nao tutafika mbali sana tukishirikiana hivi hivi bega kwa bega Kesho ni ya kwetu najua kuna wajinga wachache wanajaribu kuharibu uzi siwalaumu maana bado hawajayajua maisha [emoji1490][emoji1490] Jamii Forums idumu "Too much sauce" in here.
 
Unaweza kusaga kwa kutumia food grinder au waambie sido watakupa machine ndogo hivi itakufaa au nunua machine yoyote ya kusaga ambayo ni ndogo.si lazima usage unga uwe laini sana. Tui utapata kwa kuongeza maji moto kwenye huo unga halaf unakamua.
9aab84f705107911e8d0fea6d3c6f00a.jpg
43c5bde8680467225966857d9793ef9a.jpg
 
Kwa kiwango cha pesa ulicho nacho nakushauri ufanye kati ya biashara zifuatazo:
1. Nunua mashine za kutengeneza peanut butter. Mashine hizo ni peanut grinder, peanut roster na meza ya kufanya sorting. Hiyo hela itatosha na utabakiwa na kiasi fulani cha kunjnua raw materials (karanga) za kutosha za kuanzia.

2. Biashara ingine nunua mashine ya kusaga na kukoboa unga wa mahindi na uwe unapaki. Mashine hizo fanya zitumie motor moja ku run mashine zote mbili ili kuokoa gharama. Hapa sidhani kama utakuwa na hela ya materials ya kuanzia.

Pia kwenye case zote mbili nime assume utakuwa na shed ya kuweka hizo mashine.

Kila la heri
12ad4afa278ba74468d855796d4ace26.jpg
3c2d138ef4a16a47553820e13fd2fc22.jpg
65f60aff581b950071e0eb61712f875d.jpg
 
Kwa wadogo zetu mnaokua na watu wazima ambao bado akili zinakua tungependa kuwaarifu kuwa sisi tunajua kuandika utani na pumba zaidi yenu lakini tufahamu tuandike wapi na wakati gani, kuna majukwaa mengi ya utani lakini when it comes to be business kuweni na adabu tafadhali
Umenena! Wengine tunapatia mawazo humu na kuya implement kabisa.
 
Ni wazo zuri, jaribu kuwekeza kwenye Mini grids I mean off-grids electricity hasa katk maeneo ambayo mpango wa usambazaji wa umeme vjjn hayajafikiwa, unaweza ukara hela.
Hii ndio nini mkuu?
 
Wakuu nawashukuru kwa maoni na mapendekezo mazuri sana.
Maoni zaidi yanahitajika.
 
Unaweza kuzisaga kwa mashine gani mkuu,

Pili, ukikausha ule unga tui litapatikana kweli ?
haliwezi patikana,
jamaa anafikiri ile nazi ya unga inapatikana kwa kusaga nyama ya nazi,wakati kinachokaushwa ni tui,baada ya kuchuja machicha
 
haliwezi patikana,
jamaa anafikiri ile nazi ya unga inapatikana kwa kusaga nyama ya nazi,wakati kinachokaushwa ni tui,baada ya kuchuja machicha
Nilijiuliza ivo kama inawezekana kweli baada ya kukausha,
Jamaa anatetea kwamba ukiweka na maji ya moto inapatikana,
Labda nifanye majaribio.
 
baishara ya ku-process na ku-tui au unga wa nazi naona kama itakua ngumu sana. Bakhressa analeta toka Indonesia ila zimekua branded, hata american gardens pia. Bei ya nazi ipo juu, umeme sio rafiki na hata vifungashio ni ghali. Ukiwa mzalishaji mdogo itakusumbua sana kushindana kwenye bei.

Siku hizi mjini watu wanatumia sana tomato paste na nyingi inatoka china au uarabuni. Naona kama nyanya ni nyingi na bei iko chini kama ukiweza kufanya uchunguzi wa kibiashara hii inaweza kukutoa. Kuna kampuni 1 tu ya kitanzania ambayo ikoa arusha ambayo inajihusisha na utengenezaji wa tomato paste.
 
haliwezi patikana,
jamaa anafikiri ile nazi ya unga inapatikana kwa kusaga nyama ya nazi,wakati kinachokaushwa ni tui,baada ya kuchuja machicha
Hio unayoisema wew siijui.mimi niliyonunua na kuitumia haiko laini.unga wake uko katika chembechembe.na nilitia maji moto.kwa hio nipe hio brand uliyowahi kutumia na tuelimishe uliitumiaje.
 
Anzisha kiwanda cha kutengeneza unga wa nazi.unakausha zile nazi halafu unazisaga.halafu unazitia kwenye paketi.hakikisha paketi haiingizi hewa ndani ili huo unga usiharibike.hapo utatafuta kampuni ikutengenezee hizo paketi.halafu uzipige nembo yako. Kuna watu wengi hawana mda wa kukuna nazi hivo utapata wateja wengi tuu hata nje ya tz utauza.na machine unayohitaji kwa kuanzia ni moja tu ya kusaga.

Hili wazo nitalifanyia kazi haki
 
Hupati tui mkuu
Ukikausha unga wa nazi tui huondoka kwa njia ya evaporation na kinacho baki ni mafuta tuu!!!
Kinachoondoka sio tui bali majimaji yalio kwenye tui.tui lina vitu vingi ndani yake.unapokausha unaondoa majimaj tuu
 
Back
Top Bottom