Kiwango gani cha mbegu za kiume kinaweza kupelekea mimba?

braity

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2020
Posts
366
Reaction score
478
Wakuu,

Kama uzi unavyojieleza hapo juu, napenda kufahamu ni kiwango gani cha manii chahitajika ili kuweza kurutubisha yai la mwanamke ambaye yupo tarehe za kupata mimba?

Nina maana endapo hujatumia kondomu na ulipanga kuchomoa wakati wa ejaculation na kwa bahati nzuri au mbaya ukachelewa kuchomoa uume na kiwango fulani kikaingia na kiwango fulani kikatoka nje.

Je, kwa mazingira hayo yaweza pelekea mimba?

Naomba kujuzwa

 
Ndio mimba anapata.

Na hapo ukiunganisha cha pili kabla haujaenda kukojoa ( mkojo wa kawaida) zile precum zinatoka na shahawa zilizobaki njiani so anapata tena mimba.

Na kama yai limeshapevuka hata akitumia p2 baada ya lisaa haiwezi kuzuia mimba.

Tumia condom siku nyingine.
 
Itabidi topiki za Mfumo wa Uzazi darasa la 7 na Reproduction kidato cha 3 na 4 zifundishwe kwa undani zaidi. Juzi kuna baharia pia alileta uzi hapa akilalamika kuwa kabambikiwa mimba kisa eti alimwagia nje bao la kwanza halafu akarudi tena na kuunganisha bao la pili...
 
Ichi kitu kilinipata , akatumia p2 , kumbe yai lishapevuka p2 ikagoma, Nashukuru Mungu Sasa Nina mtoto,
 
Sikuwahi kujua we ni mtaalum hivi!
Watu na experience zenu..🤣
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…