Kiwango gani cha umaskini umekishuhudia kikakushangaza na kukusikitisha?

Kiwango gani cha umaskini umekishuhudia kikakushangaza na kukusikitisha?

Mimi kuna Maisha hapo Nimeyaishi..
Tatizo linakuja, Ni maskini wachache Sana wanajionea huruma ambayo wewe Mpitaji Unawaonea...

Mtu anaishi maisha ya Ajabu sana lakini ni kama karidhika.
Umaskini unaanzia kichwani.

Wanaolala pembeni ya Barabara mfano kariakoo kwenye maboksi na mbu wote hawa, tena kipindi kama kile cha mvua
Hamuwaoni?
 
Mkuu vipi ukianzisha chuo cha kufundisha ujasiriamali na/au sanaa ( muziki kuimba, kucheza ngoma) for free kwa vijana wa Lindi mjini na vijijini .

1. Unaweza kupata eneo kwa maana ya madarasa ya kukodi. Je gharama zake zinaweza kuwa Kiasi gani?

2. Vijana wanawaweza kupatikana? Ambao wamefeli form four na walio ishia la saba pamoja na wale walio feli form 2
 
Aisee kweli tunaishi kwenye umaskini wa kutupwa mikoa ya kusini huku vijijini kumezidi sana ninapopita kazini nakutana na hali za kutisha.

1. Watoto wanakula maembe wanashindia kama chakula sio kama matunda. Wazazi wapo shamba huko wamewaacha watoto nyumbani mpaka na vimwali wazuri unakutana nao shida vibaya mno.

2. Mademu kugongwa kwa buku.tulienda site sasa pale tumepiga camp baadae mademu wakawa wanakuja wenzangu wanawachukua wanagonga wanawapa 1000-3000 na mademu wanakubali kabisa wanapishana vibaya mno. Aisee dhiki isikie tu

3. Watu kula kisamvu tupu yaani kisamvu kinachumwa kinachemshwa kinaliwa vilevile kilivyo bila hata ugali maana unga hakuna msimu huu ndo kwanza wanalima.

4. Watu kula takataka zote kama wachina aisee wamakua masasi pamoja na uchu wa kutafuna njaa ila pia umaskini unachangia watu wanakula kenge, panya, chura wakubwa na wadudu sio poa.

5. Watu kunywa maji machafu ya kwenye madimbwi aisee watu wana shida ndugu zangu

6. Kuishi na mifugo kwenye kijumba, mtu anaishi na mbuzi kwenye chumba kimoja na kuku aisee kama unakaa mjini na unawasha taa na kuangalia TV tambua hauna hali mbaya.
Mtaji wa ccm huo
 
Halafu inakuja serikali inasema Kagera ndo mkoa unaoongoza kwa kipato kidogo..
Wakati unaweza tembelea Wilaya nzima usikute hata nyumba ya udongo wala nyasi au ni kawaida kukuta Kijiji kizima msouth tu
Mhm sio kwel
 
Umasikini utaishaje?

Kanda ya ziwa kijana wa miaka 20 ana watoto 8, jiulize atawalishaje , atawavalishaje nk,
Niliifika shinyanga vijijini nikamuuzia dogo mmoja wa bodaboda nimemzoea nikaambiwa na mkewe yupo kwenye ngome yake nyingine sikumuelewa ikabidi nimpigie simu akaniambia yupo kwa mke wake mwingine dah nikachoka. Hali ngumu Sana hasa kipindi Cha kiangazi.
 
Na kuzaliana bila mipango nako ni sababu kubwa ya umasikini.

Mtu kujitunza yeye hawezi, bado analeta na viumbe wengine wengi asioweza kumudu kuwahudumia.
 
We jamaa una inferiority complex kubwa sana ni ukweli kagera ni mkoa maskini sana kuliko yote
Umaskini unaangalia factor nyingi sana
Sasa wanitukania Nini mkuu...Mimi mtu akianza matusi sibishani tena..
Mtu anayetukana mara nyingi ana akili ndogo na uongozwa na emotions ndo maana mara nyingi ni tabia za wanawake...

Turudi kwenye hoja...Mimi nimetoa kulingana na my observation nawe unabidi utoe maoni Yako kwa ushahidi kubisha hoja yangu sio kunitukana
 
Ukitembea Tanzania utaona mengi sana ,ila kiukweli IQ za wengi huenda zisiwe normal.wakati mwingine watu wapo kwenye mazingira wanaweza zalisha kabisa lakini bado wanahali ngumu.Elimu inabidi kutiliwa mkazo na watoto wafundishwe kazi ndogo ndogo walau za kulima hata mboga pindi wanapokuwa mashukeni.wazaz wengi hawawezi kumudu Barbara Milo ya watoto ,hiyo hupelekea udumavu wa akili.ni watoto tuu angalau wa mijini ndio wazazi wanamudu mahitaji,lakini vijijini Kuna Hali mbaya.siku ya mnada Kuna mtu anaenda kwenye mnada na bidhaa za 200/,kwenye Soko jaribu kufikiria kitu kama hicho
 
Sasa wanitukania Nini mkuu...Mimi mtu akianza matusi sibishani tena..
Mtu anayetukana mara nyingi ana akili ndogo na uongozwa na emotions ndo maana mara nyingi ni tabia za wanawake...

Turudi kwenye hoja...Mimi nimetoa kulingana na my observation nawe unabidi utoe maoni Yako kwa ushahidi kubisha hoja yangu sio kunitukana
Onyesha tusi kwenye hio statement kabla sijakujibu
 
Back
Top Bottom