Masikini si masikini.
Masikini ni yule anayeona umasikini na asifanye chochote huku ana uwezo.
1. Wote labda usingeweza kuwatoa,ila hata mmoja ungeweza. Japo hakika na wewe ulitumia. Na jiulize,elfu 1000 wewe ukipewa utanunulia nini? Hata chupi kwake haipo. Huo si ukatili sasa?! Unadhani mtoto wa kike kwa hela hiyo,iwapo anapeleka kwao wakale,baada ya mtanange ule,ulifanya nini?
-Wanaoshindia maembe,uzuri ni kwamba wazazi wameenda shamba kuandaa mazingira ya kesho na keshokutwa. Vimwali vizuri,umeviona wewe,kwao wanajiona wa kawaida.
Na mengine mengi.
Sema,huu umasikini unaouongelea,chanzo ni binadamu hatupendani:
-mtu ana hela nyingi,amezunguukwa na watu wasiojiweza,ila raha yake waone anatembelea gari la bei mbaya,anakura starehe,chakula kizuri anamwagia mbwa, watoto sawa na wa kwake ndo hao wanalalwa kwa buku! Ambayo hata kilo ya unga hamna.
-Wengine wapo tayari kutengeneza siraha za kuua hao hao masikini wasio na hatia,kikubwa tu wao wajaze matumbo yao na familia zao.
Ili uone ambavyo masikini hao ndo matajiri,mia mia zao zinazokusanywa kwenye mambo mbali mbali,ndo zinatunisha vitambi vya mafisadi na wengine waliojaa roho mbaya.
Hao hao,wangewapata wa kuwaelimisha na kuwaelekeza na kuwasaidia, pengine badae na wao wangeondokana na hiyo hali unayoisema.