Kiwanja changu kimekaa kama sambusa, ninapanga kumega eneo la jirani kiwe square. Sheria inasemaje kuhusu hili?

Kiwanja changu kimekaa kama sambusa, ninapanga kumega eneo la jirani kiwe square. Sheria inasemaje kuhusu hili?

Ninachofurahi ni kwamba unaonekana hutaki kabisa kuishi hapo maisha yako yote, mega hicho kiwanja utakapoondoka kurudi nyumbani itakuwa jumla kurudi kwenye eneo lako! Utabaki kusikia tu kwenye bomba kwamba umewahi kuwa na kiwanja eneo hilo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengine tuna vya mduara kama chapati


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Si vyema kwani utajenga chuki na huyo jirani hata kama unamuweza kwa kila kitu
Mf nina ndugu yangu alikuwa amepakana na jirani yake ila sasa huyu ndugu yangu eneo lilikuwa halitoshi kujenga jiko .Kistaarabu akamuomba mwnyeji wafanue mazungumzo na kama kuna kiasi cha pesa ili amuuzie hizo hatua kadhaa. Cha ajabu yule mwenyeji akamwambia hizi hatua mbili si kitu waweza ongeza bure.

Nakuambia ukawa ndio mwanzo wa undugu mzuri kati ya watu hawa wawili hadi pale mwenyeji alipotangulia mbele za haki.

NB; watu wengine bhn anakuja humu anaandika ujinga ilhali anaujua kabisa na fika kuwa kwa akili za ma intelectual Wa humu JF lazima watampinga kwa kitu anachotaka fanya lakini ye hajali ana type tu.
 
Sijui wananini Hawa majirani
Mie nauza nyumba yangu sababu ya maumivu ya jirani na watu was ardhi na wqjumbe wa serekali ya mtaa kukata eneo langu na kuumpa barabara jirani nikawa sijui siku inaletwa mchoro wa ardhi nakuta hivyo karibia nizimie na pia ardhi wamekubali kosa kupima eneo mie kutokuwepo kulekebisha hawataki na yule alipewa barabara ameenipeleka kwa afsa mtendaji kwanini nimeweka kifusi yaani roho inaniumaa mpaka kile kipande kinaniuma mpaka nauza hichi kilichobaki bado kikubwa yaani mkauzu anashirikiana na wenyekiti wa mtaa kunizurumu [emoji31][emoji31] ardhi inauma sikuwahi kujua watu wanauana kwa sababu gani daahaa nimekosa Raha kabisaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria inatafsiri hii kitu kama wizi wa waziwazi na ni kama kuhujumu uchumi wa mwenye mali. Na kosa lake halina dhamana
 
wewe ndio una mpango kama huu au wako ni mpango wa aina gani


82894119_2900468053348567_8534086480310774266_n.jpg
 
Angalia tu usije kuliwa hio sambusa yako.

Sent from my DUB-LX1 using Tapatalk
 
Ukifanya hivyo utakua hauna tofauti na serikali ya sasa

kushindwa ku design miundombinu ya jangwani kisa eti

ni eneo na mkondo wa maji,Achana na ugomvi na watu

Tumia akili ulizopewa ku design kiwanja chako kionekane

vile macho yako yanataka,acha kukariri Square tu ndio inatoa

picha nzuri ya muonekano wa kiwanja chako.
 
Same senerio..!
Kwa kweli siridhiki kuona kiwanja changu kimekaa kama sambusa.. Natamani kiwe square kama kiwanja cha mpira.

Sasa ili 'kuboresha mipango miji' ninapanga kumega kama mita moja kutoka kwa jirani ili kikae sawa.

Hapa ninakusanya nguvu ya tofali elfu mbili.. Nikija kuibuka naibuka na ukuta mmoja mrefu wa maana.

Mpaka jirani aje kushtuka atakuta kuna ukuta mzito kama ule wa kuzuia bahari wa Ocean road.
Je, kuna mwenye wazo tofauti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
'USiku kaenda na gari zake mbili alikuwa na dala dala na ya kutembelea akapaki.

usiku sehemu ya barabara ya kuingilia majirani wakafunga kwa kujenga ukuta wakiunganisha nyumba zao ili asiwe na pa kutokea.Asubuhi anatoka getini akajikuta kazungukwa na kuta kama yuko magereza.Watoto hawawezi kwenda shule wala yeye kutoka.'

Story nzima ya uongo mtupu,kawadanganye watoto ndio watakaoamini ukuta ulijengwa kwa usiku mmoja na asubuhi ukawa umekamilika.
huwa kuna majirani wanapendana kama ni uswahilini anahama.

kuna jirani mmoja alichukua kiwanja cha mwenzie maeneo yasiyopimwa .Yule aliyeporwa kiwanja akawaambia majirani .Majirani wakasema haina shida .USiku kaenda na gari zake mbili alikuwa na dala dala na ya kutembelea akapaki.

usiku sehemu ya barabara ya kuingilia majirani wakafunga kwa kujenga ukuta wakiunganisha nyumba zao ili asiwe na pa kutokea.Asubuhi anatoka getini akajikuta kazungukwa na kuta kama yuko magereza.Watoto hawawezi kwenda shule wala yeye kutoka.

IKabidi aruke ukuta aulize kulikoni.Wakasema ile barabara ni eneo lao waliachiana tu nafasi kama majirani sio barabara ya serikali wamekubaliana wameamua kujenga ukuta vibaka wanawasumbua.AENDE KOKOTE.kWENDA SERIKALI YA Mtaa kule akaambiwa hilo eneo ni lao wana haki kufanya nalo chochote.

Ilibidi aongee nao wamuuzie wakagoma wakasema hawahitaji pesa

Ilibidi ahame na aliuza eneo kwa hasara kwa msikiti ,msikiti wakaongea na majirani wale majirani wakavunja kuta kwa gharama zao akatoa magari yake na vitu vyake akahama moja kwa moja

mambo ya ukorofi wa ardhi sio mazuri

dodge
 
Kwa kweli siridhiki kuona kiwanja changu kimekaa kama sambusa.. Natamani kiwe square kama kiwanja cha mpira.

Sasa ili 'kuboresha mipango miji' ninapanga kumega kama mita moja kutoka kwa jirani ili kikae sawa.

Hapa ninakusanya nguvu ya tofali elfu mbili.. Nikija kuibuka naibuka na ukuta mmoja mrefu wa maana.

Mpaka jirani aje kushtuka atakuta kuna ukuta mzito kama ule wa kuzuia bahari wa Ocean road.
Je, kuna mwenye wazo tofauti?
Nadhani unachokitafuta utakipata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui wananini Hawa majirani
Mie nauza nyumba yangu sababu ya maumivu ya jirani na watu was ardhi na wqjumbe wa serekali ya mtaa kukata eneo langu na kuumpa barabara jirani nikawa sijui siku inaletwa mchoro wa ardhi nakuta hivyo karibia nizimie na pia ardhi wamekubali kosa kupima eneo mie kutokuwepo kulekebisha hawataki na yule alipewa barabara ameenipeleka kwa afsa mtendaji kwanini nimeweka kifusi yaani roho inaniumaa mpaka kile kipande kinaniuma mpaka nauza hichi kilichobaki bado kikubwa yaani mkauzu anashirikiana na wenyekiti wa mtaa kunizurumu [emoji31][emoji31] ardhi inauma sikuwahi kujua watu wanauana kwa sababu gani daahaa nimekosa Raha kabisaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Unauza bei gani? na wapi uko?
 
'USiku kaenda na gari zake mbili alikuwa na dala dala na ya kutembelea akapaki.

usiku sehemu ya barabara ya kuingilia majirani wakafunga kwa kujenga ukuta wakiunganisha nyumba zao ili asiwe na pa kutokea.Asubuhi anatoka getini akajikuta kazungukwa na kuta kama yuko magereza.Watoto hawawezi kwenda shule wala yeye kutoka.'

Story nzima ya uongo mtupu,kawadanganye watoto ndio watakaoamini ukuta ulijengwa kwa usiku mmoja na asubuhi ukawa umekamilika.

dodge
Kuna stori kama hii imetokea kiukweli, tena hapo Mbagala-Kongowe tu.
 
Back
Top Bottom