Hivi ni kweli Bunge hawajui kuwa Chadema kwa kushirikiana na Familia ya Lissu ndio wanaomuuguza Mh. Lissu hospita Nairobi.
Spika hana Ruhusa ya Mh. Mbowe (KUB) ya kumuuguza Lissu Nairobi.
Iweje malipo ya michango ya Wabunge yafanyike hospital bila kuwapa taarifa Wanaomuuguza Mgonjwa?Chadema na Familia ya Lissu.
Tena kutoa taarifa ya malipo muda mfupi baada ya kushutumiwa kuweka mfukoni Fedha za michango.
Mbona hii Serikali inazidi kujiweka uchi mbele ya hadhara kwenye hili suala la Lissu,Wanajichanganya mno,kila siku wanazidi kuharibu badala ya kujenga,Je hatukuamini kuwa Lissu angepona?
Pesa zichangwe tarehe 8 sijui zije kulipwa tarehe 20 kweli inaingia akilini tena kwa kificho?
Huyu mama naye wa wizara ya afya,utafikiri sio mwanamke?hana uchungu wa kimwanamke?Mgonjwa ameanza kutibiwa tarehe 7 baada ya siku 14 Wizara inatangaza kutaka kumtibu popote duniani kweli?hapana Dada angu Ummy muongope Allah,kuwa na hofu na Mungu,duniani hamna Mungu Mtu na ndio mana Lissu ameweza kunusurika,Ummy wewe ni Muislam,unajuwa maana ya Jina lako katika Uislam,kumbuka heshima ya Jina lako!!
Yule aliyeapishwa Juzi,anajitokeza kufafanua mambo yasiyomuhusu,eti Jaji Mkuu,kiongozi wa Mhimili wa Mahakama anafanya Press na waandishi wa habari,tena anachagua upande,sasa ikija kesi mahakamani na huo upande ukiwa ndio mshtakiwa?itoshe kusema na aone kuwa heshima aliyopewa na Mbowe ni busara na Hekima kwa Mhimili wa mahakama,aone maendeleo ya mahakama zetu kabla yake licha ya changamoto chungu mzima,asikubali kutufanya tukose imani na mahakama katika uongozi wake.