Hapo nyuma kidogo niliwahi kuuliza, je yawezekana wakuu wa vyombo mbali mbali nchini walijua kilichokuwa kinaendelea kuhusu hatma ya Mh. Tundu Antiphas Lissu? Je yawezekana waratibu na watekelezaji walikuwa na uhakika Mh. Tundu Lissu hangeendelea kuwa hai saa 24 baada ya kumiminiwa idadi kubwa ya risasi mwilini?
Ukweli kwamba Mwenyezi Mungu kasikiliza maombi ya wengi na hivyo kumuepusha na kifo Mh. Tundu Antiphas Lissu, kumewachanganya wahusika hadi kila moja anaibuka na tamko lake! Je kuibuka kwa kauli na vitendo kutoka kwa viongozi mbalimbali huku hali ya Mh. Tundu Antiphas Lissu ikiendelea kuimarika, kunatupa picha gani?
Hali hii bila shaka imesababishwa na kiwewe kizito kilichowakumba washauri, waratibu, na watekelezaji wa jaribio la kigaidi la kumuua Mh. Tundu Antiphas Lissu! Tusubiri kuona mengi, kusikia mengi na kushuhudia mengi kwani walichopanga kutenda hawa waovu Mwenyezi Mungu kawakatalia na sasa wanahaha nafsi zao zikiwasuta!