Elections 2010 Kiyabo "arejea" CCM

Elections 2010 Kiyabo "arejea" CCM

Mi naanza kuamini yale yaliyokuwa yanasemwa kuwa ccj kilikuwa ni changa la macho lililoandaliwa na ccm ili kuua nguvu ya upinzani hususani Chadema.Ila walipoona Mpendazoe amehamia huko,jambo ambalo halikutarajiwa basi wakabadili nia na kukimaliza kwa kutokukipa usajili wa kudumu.Maana kama wangekipa usajili basi mambo yangekuwa tofauti na walivyotarajia.Labda Mpendazoe alishtukia dili akahamia Chadema au ni bahati tu...Huwezi amini hawa ndo jamaa walioangusha kilio kule Butiama,jamaa wengine kwa kuact hawajambo.
 
Pamoja na kuwa mzazi, ila kuna mitoto siyo riziki. Yaani kama mtu hajui yuko wapi na anakotaka kwanda basi ni jitu la hatari hilo.

Pamoja na kuwa mzazi ila kuna mitoto hata likifa, rohoni unafanya sherehe ya kujipogeza kwa kuondokewa na zigo!:mad2::mad2:
 
Kisha mkuu wangu Mwanakijiji alikuja waamini watu hawa!....Na yuko wapi..

Mimi toka mwanzo niliamini kabisa kwamba CCJ ni chama kilichoanzishwa kuivunja nguvu Chadema kabla ya kampeni. Kuondoa hoja kubwa ya Ufisadi ambayo ndio ilitawala magazeti yote nchini na kwa kufanya hivyo walifanikiwa sana.
Huyu Richard Kiyabo kamaliza kazi yake na anarudi kambini. Hakuwa ametoka CCM hata siku moja na wajinga wengi waliamini kuwa CCJ ni chama kipya chenye mwelekeo.

Lakini pamoja na yote haya mimi na mashaka sana na Uwezo wa kufikiri wa Watanzania. Ni jana tu asilimia kubwa walikuwa wakilaani CCM na kutoa matusi yote ya mapungufu ya JK, leo hii wameshasahau au kusamehe, hao hao ndio wanaunga mkono chama hicho tena kwa nguvu zote...Kesho kilio tena!
Sijui ndio asili ya athari za Utumwa au Miafrika ndivyo Tulivyo!

Mie binafsi kila siku nasema tatizo la Tanzania sio CCM na dawa yake si CHADEMA wala CUF. Tatizo la TZ ni tanzania wenyewe.
 
Huyo alikuwa ni mamluki tu wa ccm kuja kuvuruga kura za wapinzani, hana lolote ni uchizi na njaa ndio yamsumbua. Yaani hata mtoto mdogo asiyejua siasa ni nini atajua huyo mtu hana akili timamu, yaani ndani ya mwaka mmoja kuanzisha chama, then kuhama vyama kadhaa ni zaidi ya uchizi.
 
2852134.jpg

Mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh!
 
Kweli siasa ni ajira, hakuna cha sera wala nini? na wala sitashangaa nyepesi akijiunga huko. Maisha maslahi bwana!!
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ) - almanusura niandike CCM! - Richard Kiyabo, leo "amerejea" na kukabidhiwa kadi rasmi na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.

Habari zilizotangazwa sasa hivi na Taarifa ya Habari kwa Ufupi ya saa 10 jioni ya TBC1 zimetangaza.

Taarifa zitaendelea kuwafikia.

Buriani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
kiukweli hapo ndmmm unagundua kuwa chama chetu kinawavutia walafi wa madaraka na mali and kiyabo R ni mmoja wapo anataman kuchukua chake mapema najua wapo wengi kama yy ndan ya sisiem ila mwisho wote ni fedheha na wadanganyika washaanza elimika taatbu watajua pumba na mchele.!
 
Sasa ili maandiko yatimie tunasubiria siku moja MZEE MWANAKIJIJI akienda Lumumba Street Kumwona Makamba... Patanoga hapo?:glasses-nerdy:
 
Wanabodi naomba kuuliza...

Kuna Mtanzania asiyejua kwamba SHIBUDA atarudi CCM baada ya Uchaguzi?
 
Kiyabo Kiyubu whatever the name is una akili kama ya mlevi, yes i said akili yako kama ya mlevi.. huwezi kuyumbisha akili za watu kwa manufaa yako binafsi. Nani anaonekana mpumbavu hapa ni wewe au sisi watanzania wenye uchungu na nchi yetu. Umefulia kwa ufupi huu ndio mwisho wa umaarufu wako kama ulitumwa na ccm basi wamekudanganya kama mtoto mdogo ambaye anaambiwa usilie nitakupa peremende. Shame on you na wale wote walikuweka kwenye hili including ccm chama cha mapum@#@#@# kila la heri katika mwanzo na mwisho wa safari yako.
 
Wanabodi naomba kuuliza...

Kuna Mtanzania asiyejua kwamba SHIBUDA atarudi CCM baada ya Uchaguzi?
Mkuu wangu nakuhakikishia kwamba Shibuda baada ya Uchaguzi huu atakuwa mwiba wa siasa nchini. Jina lake litavuma ana atakuwa na mvuto usiokuwa na kifani, huu ni mwanzo wake mpya.
Amini maneno yangu na utakuja nambia...
 
Ni kitendo cha kushangaza na kusikitisha. Hawa ndio watu wenye njaa na hawajali utu wao na familia zao. Huyu kiyabo naamini ana mke na watoto ambao wanamwangalia kama mfano wa familia. Hajali impact watakayopata watoto shuleni au mke ofisini kama anafanya kazi. Analeta picha gani katika jamii. Haingii akilini chini ya miezi 6 umezunguka vyama 4 kati ya hivyo, moja umeanzisha chama chako lakini nyingine umejaribu kabisa kugombea urais kupitia chama hicho. Hajali ni wafuasi wangapi, (hata kama ni wachache) lakini wapo waliomfuata na lazima tujue kuna watu wengine wanafuata watu na sio vyama. Hii ina maana mfuasi vile anamfuata Kiyabo atakuwa CCJ, halafu CHADEMA, baadae NRA, ghafla CCM tena. Hata kama mtu ana uhuru wa kuwa chama fulani inaonyesha hana maono wala mpango mkakati wa kuendeleza maendeleo ya sehemu inayomzunguka. Ni aibu hata kumwita kiongozi na hafai kabisa kuwa mfano hata kwa familia yake mwenyewe
 
Cheko lake tu limekaa kitaahira taahira - ananikumbusha mgonjwa mmoja taahira pale hospital ya MILEMBE!

:becky::smile-big:hahaha ndugu umefurahisha sana yule bwana kweli anaonekana alichelewa kulia (cry) wakati anazaliwa huenda akawa low score kabisa....
Kuna mzungu mmoja alimtusi mwenzake kwa kusema "there r some people walking with finger in the their A**" huenda huyu bwana ni mmoja wao.
 
Back
Top Bottom