Kizazi cha 1978-1985 hatuzeeki. Je, unajua sababu?

Kizazi cha 1978-1985 hatuzeeki. Je, unajua sababu?

Tuliozaliwa 1978- 1985 tunarange kuanzia miaka 39-46, tumegoma kuzeeka, sijui kama mnafahamu sababu.

Iko hivi, kipindi hicho nchi ilipitia changamoto za kiuchumi, tulikuwa na vita ya iddi Amin hata baada ya vita hali haikuwa shwari, tuliendelea kufunga mikanda, uzalishaji wa chakula haukua vizuri, kama nchi tuliagiza chakula nje ya nchi, mnaukumbuka ugali wa Yanga??

Ni mpaka Mwinyi alipochukua nchi tukaanza kula vizuri, asikwambie mtu afya ya mtoto hutegemea genes za wazazi na chakula, hayo mambo mawili ndio huamua muonekano wa mtu ukubwani.

Tuliozaliwa miaka hiyo kuna virutubishi tulikosa matokeo yake tukatengeneza highbreed ya watu fulani, sio magiant sio wafupi, ni kuanzia futi 5 na inchi 4 mpaka futi 5 na inchi 8 wengi tuko humo.

Kukuta kijana wa 1980 ananyimwa shikamoo anapewa wa 1990 ni kawaida sana.
Orodha ya watu mashuhuri wanaoangukia humo ni kama hii
Dully Sykes, 45
Ridhwan Kikwete, 45
Mwana FA, 45
Queen Daren, 44
Single Mtambalike, 47
Ben Kinyaiya, 46
Maulid Kitenge, 48
Haji Manara, 50
Mange Kimambi, 46

Hawa ni watu ambao either nimesoma nao au nawafahamu kiundani tangu utotoni miaka ya rary 80's

Uzi huu hauwausu walioharibu afya zao kwa pombe kali na starehe zingine
ila hata hivyo wazee wa 1990 ni masela sana na mvi zao zilizojaa jaa sana kidevuni 🐒

kabinti kakisalimia shikamoo... kanaitikiwa vizuri tu markhabah na Mzee wa 1990, lakini Lazima katapigwa na ile salamu ya mambo vip uko poa....
ili kutengeneza mazingira ya uflat na kumuondoa mtoto hofu 🐒

Vizee vya 1990 ni visela nuksi sana aise dah 🐒
 
Tuliozaliwa 1978- 1985 tunarange kuanzia miaka 39-46, tumegoma kuzeeka, sijui kama mnafahamu sababu.

Iko hivi, kipindi hicho nchi ilipitia changamoto za kiuchumi, tulikuwa na vita ya iddi Amin hata baada ya vita hali haikuwa shwari, tuliendelea kufunga mikanda, uzalishaji wa chakula haukua vizuri, kama nchi tuliagiza chakula nje ya nchi, mnaukumbuka ugali wa Yanga??

Ni mpaka Mwinyi alipochukua nchi tukaanza kula vizuri, asikwambie mtu afya ya mtoto hutegemea genes za wazazi na chakula, hayo mambo mawili ndio huamua muonekano wa mtu ukubwani.

Tuliozaliwa miaka hiyo kuna virutubishi tulikosa matokeo yake tukatengeneza highbreed ya watu fulani, sio magiant sio wafupi, ni kuanzia futi 5 na inchi 4 mpaka futi 5 na inchi 8 wengi tuko humo.

Kukuta kijana wa 1980 ananyimwa shikamoo anapewa wa 1990 ni kawaida sana.
Orodha ya watu mashuhuri wanaoangukia humo ni kama hii
Dully Sykes, 45
Ridhwan Kikwete, 45
Mwana FA, 45
Queen Daren, 44
Single Mtambalike, 47
Ben Kinyaiya, 46
Maulid Kitenge, 48
Haji Manara, 50
Mange Kimambi, 46

Hawa ni watu ambao either nimesoma nao au nawafahamu kiundani tangu utotoni miaka ya rary 80's

Uzi huu hauwausu walioharibu afya zao kwa pombe kali na starehe zingine
Kwaio mh. Ridhwan alikosa virutubushi utotoni sio ??
 
Na ndio maana tunaweza kuoa watoto wa 2000s tukawa sawa nao tu. Vijana wa siku hizi wanazeeka kuliko baba zao hadi mtu unaona noma kutembea na kijana wako ana mvi nyingi, kitambi na upara wakati dingi yake hana hivyo vitu. Kama ni binti unakuta ni mkubwa kuliko mama yake hadi aibu. Hawa madogo ndio wanaosalimiwa shikamoo sie wakongwe tunaachwa hatusalimiwi, huwa nacheka sana
 
Kwaio mh. Ridhwan alikosa virutubushi utotoni sio ??
Enzi za Nyerere wanasiasa nao waliishi maisha duni tu,kipindi rizwan anazaliwa baba yake alikuwa nadhani katibu wa CCM wilaya,sina uhakika,au alikuwa vitani uganda sijui,ila hali ilikuwa ngumu sana,nyerere mwenyewe aliishi maisha magumu,sasa wrwe kiongozi hata ungekuwa na hela dukani hakuna mayai,hakuna maziwa,hakuna sausage wala blue band,si ajabu rizwan aliishi maisha ya kawaida,maana JK hakuwa mtu wa kujitutumua
 
Mke wangu nimemzidi umri ana umri nusu yangu na namuona ni mtu mzima kuliko mimi. Naona kama ananizeekea haraka wakati mi ni mkubwa mbali sana. Ningekuwa mhuni ningekuwa na mchepuko mdogo kuliko mke wangu ninayemuona sasa kazeeka wakati mi bado kijana mbichi na nahitaji mabinti wabichi wenzangu. Sie watoto wa zamani tulilishwa vyakula vya ajabu ukilinganisha na hawa watoto wanaokula mapochopocho mazuri. Njaa kali ya mwaka 1984 nchi ilikumbwa na uhaba mkubwa wa chakula, watu tulikula mpaka nyasi, mihogo michungu yenye sumu ya cyanide, pumba na vitu vingine vya ajabu ili tu kujaza tumbo usife njaa. Vyakula vya afya vingetoka wapi? Potelea mbali huenda tulidumaa miili mpaka akili, hizi tulizo nazo ni kidogo hazitustahili. Hawa watoto wa siku hizi wanakua haraka kwa kuwa wanakula vyakula bora na vipo wakati wote, muda wote ni kula tu njaa hawaijui
 
Back
Top Bottom