Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
KIZAZI CHA SASA TAMBUENI KUWA; HAYA NDIO MAMBO AMBAYO YANAWEZA KUKUSABABISHIA KUUAWA BILA KUJALI SERIKALI IPO AU HAIPO!
Anaandika, Robert Heriel.
Kuna mausia ambayo kizazi cha sasa hakijapewa ndio maana kinachukulia mambo kiholela, yaani mambo rahisi rahisi. Wazazi wanalojukumu la kuwaachia watoto wao Mafunzo, na wosia wa maisha ili watoto wasipate madhara.
Kuna mtazamo wa watu hakuna sababu za mtu kuua, mtu yeyote awazaye Kwa namna hiyo ujue hajafikiri vizuri, na mara nyingi watu wa namna hiyo ni Masikini WA kifikra na Mali.
Watu wote wenye akili wanajua Zipo sababu za mtu kuuawa ikiwa atafanya Jambo fulani kubwa na la kuumiza.
Andiko hili sijaliandika kuhamasisha watu wauane isipokuwa kuwakinga Watu wasijiingize kwenye Mkondo WA kuuawa Kwa Makusudi Kabisa.
Zifuatazo ni Sababu za msingi ambazo zinaweza kukufanya Ukauawa na muuaji akajiona anahaki ya kufanya hivyo na roho yake ikawa na Amani;
1. KUIBA MKE AU MUME WA MTU
Wahenga walisema Mke WA Mtu sumu hawakuwa wajinga, na Mungu akasema usitamani mke WA jirani yako, hiyo sheria ipo Kwa karibu dini zote kubwa Duniani.
Kama mzazi hujamuusia mtoto wako kuhusu hili basi fanya hivyo mapema. Moja ya sababu zitakazosababisha Uhai WA Mtu uwe hatarini ni kuiba Wake za watu au waume za watu. UTAUAWA! Tena watakuuawa kifo kibaya, usije ukadhani Kwa vile wewe huwezi kuua kisa Mke au mume ukadhani watu wote wapo Kama wewe,
Kutoka na Mke WA Mtu au mume WA mtu ni sababu tosha ya mwenye Mali kukuua bila kujali Nani atasema nini.
Vijana wa siku wanafikiri kirahisi, wanadhani kila kitu ni mchezo tuu usio na matokeo, ndio maana kijana anaweza kukuchukulia Mkeo na akakuongelesha Kwa Dharau.
Taikon msimamo wangu, mtu akiuawa kisa kaiba mke au mume WA mtu huwaga sioni tatizo, najua vile mtu huyo anavyojisikia, na Kwa vile Mimi ni mfuasi wa Torati naona Yuko Right kufanya hivyo.
Niliwahi ambiwa na Babu yangu Kama ninataka kuishi umri mfupi zaidi basi niwe na tabia za kuiba Wake za Watu.
2. KUCHEZEA FAMILIA ZA WATU
Wapo watu linapokuja suala la Familia yake, yaani watoto wake hataki mchezo, huwezi haribu maisha ya mtoto wake alafu akakuacha salama. Watu wenye tabia hii ni zile familia kubwa za kifalme au watawala au matajiri, au jamii za Kitabu, kiyahudi, n.k.
Vijana wa siku hizi eleweni kuwa sio kila familia unaweza kuchezea watoto wake, kuna familia ukiingia ujue utakaa Kwa adabu zote na ukileta mchezo wa kijinga kutoka kwenu umekwisha, wapo wanaoua Kwa njia zifuatazo;
I. Uchawi na ushirikina
2. Ajali ya kupanga
3. Kuwekewa sumu Kwa hila
4. Mauaji ya moja Kwa moja na kutengeneza scenario ya Majambazi au vibaka ndio walikuua n.k.
Sipendi Wauaji Ila Kwa kweli sipendi zaidi watu wanaoharibu watoto wa wengine.
3. MALI NA PESA
Vijana hasa wasichana eleweni kuwa sio kwamba Mama zenu hawakuwaona wenye Mali wakati huo, eleweni kuwa Mali Kwa Baadhi ya watu ni mungu kwao, Mali na pesa ndio kila kitu. Msichukulie mambo kirahisi rahisi,
Yaani umetolewa kwenu fukara, ukasomeshwa na ukakuta familia ya mwanaume inautajiri wa kutosha tuu, ukaanza kuleta mambo ya kipuuzi alafu ukata mgawanyo Sawa Kwa kitu sijui kinaitwa HAKI SAWA Kwa kufuata sheria zilizotungwa, kuna familia hazina mchezo na mambo hayo, utauawa Binti yangu, watakuua kivyovyote iwe Kwa kuacha ushahidi au kutoacha kabisa.
Ikiwa ndugu wa tumbo moja wanauana kisa Urithi WA Baba Yao sembuse wewe Mali ulizozikuta ambazo hata hujui zilivyopatikana. Huko ni kutafutana ubaya.
Taikon sipendi wauaji, Ila sipendi zaidi watu wanaodhulumu wengine Kwa VISINGIZIO vya kijinga jinga na watetezi WA kisasa wasiojua hata nature inavyofanya kazi.
Mtu amuasi Mungu mpaka akawa Fisadi, akaenda Kwa waganga kutafuta Mali, au akaingia kwenye kazi hatari za haramu Kama kuuza madawa ya kulevya alafu awe na Mali alafu from nowhere uje uchukue mali zake mgawane Pasi Kwa pasu ati kisa Sijui ni Mke wake sijui kisa sheria zinasema nini Huko, au Mungu anasheria zake, uliona wapi mambo Kama hayo ndugu yangu, embu nawe fikiria hata Kwa akili tuu ya mtoto anayetambaa.
4. MADARAKA NA SIASA
Katika mambo ya kuyaendea Kwa umakini ni Madaraka. Wengi wamekufa kisa vyeo na mambo ya Kisiasa, Huko kwenye MAKAMPUNI binafsi, taasisi za kiserikali na mambo ya Siasa wengi wameuana na kutoana macho.
Alafu mambo haya hatakuanza Jana na wala hatataisha kesho.
Ukitaka kufa mapema kuwa na uroho wa Madaraka, pendapenda Madaraka, nakuhakikishia Utauawa bila kujali zipo sheria au hazipo.
Ukijifanya unajua kufuatilia Haki kupitiliza utauawa, kila kitu fanya Kwa kiasi, Kama ni kusema sema Kwa kiasi, Kama ni kutetea tetea Kwa kiasi, ukipitiliza watakupitiliza kituo wenye roho zipendazo Madaraka.
Usije ukadhani Kwa vile wewe huwezi kuua ukafikiri watu wote wapo Kama wewe, hiyo ni Akili ya kitoto kabisa ambayo hata mnyama wa porini hawezi kuwa nayo. Usije ukadhani Kwa vile sheria na polisi au mahakama au serikali au Mungu yupo ukadhani watu wote wanaogopa hayo 😀😀 utauawa nakuhakikishia.
Sikutii uoga Ila nakuelezea Hali halisi, si unajua Taikon anaongea Ukweli watu wasiopenda kuuweka Hadharani.
Wewe mwenyewe ndio uamue kusuka au kunyoa.
5. KUIBA ARDHI AU MIPAKA YA WATU
Ukitaka kuuawa basi penda kudhulumu watu Ardhi zao, hata kwenye ngazi ya nchi tuu. Embu fikiria Uganda itake kuchukua Mkoa WA Kagera unafikiri nini kitatokea, unafikiri serikali itasema haina haija ya kupigana na kuuana kisa Ardhi, au itasema tuwaachie tuu. Uliona wapi mambo Kama hayo wewe. Vita nyingi kama sio zote Duniani ni matokeo ya kugombania Ardhi.
Migogoro ya Ardhi sio lelemama, wengi wamekufa Kwa kuuawa iwe Kwa wazi au Kwa Siri.
Usije ukadhani Kwa vile wewe umezoea kumuachia Mungu ukadhani watu wote wanatumia kanuni hiyo, mfanyie hivyo mtu aliyepata Mali Kwa Mungu anaweza kumuachia Mungu, lakini unachukua Ardhi ya mtu ambaye hata hamjui huyo mungu wako unafikiri atakuacha hivihivi, tumieni akili kizazi cha Sasa.
Watu dhaifu ndio huweza kukuachia hata ukiwafanyia mabaya na kuwadharau, embu jaribu kumfanyia hivyo Mwanasiasa mwenye Mamlaka au matajiri au wafanyabiashara wakubwa uone Kama watatumia kanuni hiyo ya kukuachia tuu.
Utauawa!
Kuna watu watasema kwani ukiua unapata nini, hao ni watu wajinga WA mwisho na wanyonge, ni Sawa na Mtu aulize Kwani Mungu akichoma watu Moto Jehanam atapata nini, ni swali la kijinga linaloulizwa na mtu Mpumbavu.
Vijana eleweni kuwa sio kila kitu ni rahisi, na matokeo yake ni rahisi. Yapo mambo na watu wasio rahisi Kama akili zenu zilivyo, wapo watu very complicated na hawataki kufanyiwa michezo na wapuuzi.
Wito, watu wafanye mambo Kwa haki, watende Mema Kwa kufuata Sheria za Dini zao na sheria za nchi. Tabia ya kufanya Uovu kisa sheria za nchi zitawalinda wasije wakadhani watu wote wanawaza masuala ya sheria za Mungu au za nchi pale mtu anapowafanyia ubaya.
Zingatia; Serikali ipo Kwa ajili ya Kupunguza sio kuondoa kabisa, haina uwezo huo na haitakuja kuwa na uwezo wa kuondoa kabisa Uhalifu. Kwa sababu ya baadhi ya watu hutumia sheria Kama kichaka kujificha katika matendo Yao maovu wayatendayo.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam