Kizazi cha sasa tambueni haya ndio mambo yanayoweza kukusababisha ukaua bila kujali Sheria

Kizazi cha sasa tambueni haya ndio mambo yanayoweza kukusababisha ukaua bila kujali Sheria

Lakini mwanadam ameumbwa Ana sahau

Ova
 
Haya mambo tokea zamani yanaua

Na yataendelea kuua

Ova
 
Jack aliyefiwa na anayedai kua mumewe awe makini, ule utajiri ulipatikana kwa jitiada za pamoja kati ya marehemu na watoto wa mke mkubwa asitegemee sheria tu kumlinda /kutafuta haki atambue kua there is different between actual right and legal right, naomba kuwasilisha
 
Alafu sio kila mtu anayekufanyia ubaya atateseka Hilo weka kichwani [emoji3][emoji3]
Na sio kila utakaposamehe utakuwa na Amani. Inategemea na moyo wako unapenda nini.
Hakuna kitu kibaya Kama kujisaliti, kisha kusalitiwa
Hepu nieleze kwa upana hapa mkuu
 
Kuua mtu ni kiwango cha juu Sana cha ujinga ikiwemo ukosefu Mkubwa wa uhimilivu
 
Hichi ulichokisema hapa bwana Taikon nakumbuka nimekisoma kwenye darasa la Falsafa kwa mtu anaitwa Alf Ross, ambaye alisema kwamba sheria inambana tu mtuhumiwa na mshitakiwa. Nje ya hapo akasema watu wengi hawabanwi kabisa na sheria kama tunavyoamini, ila tu wanafuata miiko ya uungwana japo wanaweza wakaua.

Mimi nina mifano mingi nimeishuhudia kwenye hili ulilolisema hapa, ambapo watu waliuwawa kikatili kisa mali, mke au siasa. Nakumbuka wakati nakua kuna rafiki zetu walikuwa matajiri sana kwao, lakini mama yao aliuwawa kwa kupigwa risasi na mali zao zikaanza kupotea. Nikiwa mdogo nilisikia mama yangu akiongea na wenzake kwamba mama fulani aliuwawa kama kisasi kwasababu mume wake aliingilia maslahi ya watu fulani hivi wazito akitaka kuwatapeli fedha zao.

Siku ingine, nakumbuka kuna tajiri mkubwa alijiunga na NCCR-MAGEUZI na akaanza kuwapa fedha kwenye uchaguzi mkuu. Nachokumbuka tu ni kwamba aliambiwa nyumba yake yenye gharama ya zaidi ya milioni 100 imepita kwenye chanzo cha maji na inabidi ibomolewe. Wakati huohuo akafuatwa kwa tuhuma za rushwa na ukwepaji wa kodi. Mzee wa watu alikuwa ni mbabe sana lakini alipata tatizo la moyo huku familia yake nzima ikiandamwa.

Ushuhuda mwingine, wakati tumehamia mkoa X na wazazi wangu, kuna familia tajiri ya watu wenye asili ya kiasia waliuawa wote kwa kuchinjwa bila huruma. Kinachosikitisha ni kwamba waliuwawa wakubwa hadi watoto. Ilibidi pale mtaani waasia wengi waondoe watoto wao na kuwapeleka mikoa mingine. Ilikuja kufahamika baadae kwamba ni masuala ya kibiashara, baada ya baadhi ya wauji kuuwawa baada ya kuvamia nyumba ya jamaa moja usiku kumbe jamaa alikuwa amejiandaa siku hiyo.

Matukio ya mwisho kabisa yanayosikitisha, moja nilishuhudia mrembo moja mzuri akimwagiwa mafuta ya kupigia yaliyochemka baada ya kutembea na mke wa kigogo. Bahati mbaya mke wa kigogo alikuwa ni mtu katili asiye na huruma. Nasikia mrembo alikuwa anakula pesa huku akiletea kashfa kwa yule mke wa kigogo. It was a sad story...

Kuna jingine nakumbuka lilikuwa kwenye vyombo vya habari baada ya binti moja kutaka kumfanyia Black-Mail kigogo mzito sana ambaye alikuwa anatembea naye. Bahati mbaya sana yule kigogo ni mtu ambaye hata watu wazito ndani ya dola wanamuogopa mno kwa tabia zake za kimafia. Lakini mabinti wa kizazi chetu wanapenda kushaurina mambo mengi ambayo hayanaga uhalisia. Yule binti alikufa vibaya sana masikini.

Mwingine alikuwa ni Mkuu wa Mkoa, alitembea na mke Bi Mdogo wa mzee fulani hivi. Sasa siku ameenda bila taarifa ili akafanye yake na Bi Mdogo bahati mbaya akakuta mme yupo na familia nzima. Jamaa akashikwa na hasira akaanza kumshambulia na kumdhalilisha yule mwanamume kwamba ni bepari. Yule jamaa akaenda ndani akachukua gobole akamtandika Mkuu wa Mkoa vibaya sana, na kumtanguliza ahera.

NB: Kiufupi, kuna matukio huwa yanafanyika ambapo kama wengi tungekuwa na ufahamu nayo basi tunaweza kuwa wapole na waungwana. Kiukweli vijana wengi siku hizi hawana adabu wala uwoga, lakini ukweli ni kwamba unaweza kukutana na watu wa ajabu mno ambao wanaweza kukufanya kitu cha ajabu na wasifanywe chochote kile. Hivyo tujitahidi sana kuepukana na matatizo kisa tamaa au ujuaji. Aheri tatizo likufate lenyewe, lakini siyo kujitakia......
Mkuu heshima kwako..
 
Empathy is in my side... I'll not either kill or killed
 
Kuua mtu ni kiwango cha juu Sana cha ujinga ikiwemo ukosefu Mkubwa wa uhimilivu
Hakuna nchi yenye watu wenye maneno mengi kama watanzania. Kiufupi sisi Mungu ametupa NEEMA ya kushuhudia kiwango kikubwa cha amani ndiyo maana unaweza kuzungumza hivi. Watanzania tumelewa amani kiasi kwamba tumeanza hadi kuichezea, tukidhani ni haki yetu ya kuzaliwa. Kama ukifanikiwa kufika nchi kama Congo DR, Sudan, Somalia au walau ukae na wale Watusi na Wahutu waliokuwepo watu wazima miaka ya 1990-1994 utafahamu kwanini binadamu wanauwana.

Human Beings are capable of incomprehensible diabolical exploits that can make you sick to the stomach. Tupende kutafuta amani na watu wote, tujishushe, tuthamini haki na utu wa wengine na tuache tamaa.....
 
Hakuna nchi yenye watu wenye maneno mengi kama watanzania. Kiufupi sisi Mungu ametupa NEEMA ya kushuhudia kiwango kikubwa cha amani ndiyo maana unaweza kuzungumza hivi. Watanzania tumelewa amani kiasi kwamba tumeanza hadi kuichezea, tukidhani ni haki yetu ya kuzaliwa. Kama ukifanikiwa kufika nchi kama Congo DR, Sudan, Somalia au walau ukae na wale Watusi na Wahutu waliokuwepo watu wazima miaka ya 1990-1994 utafahamu kwanini binadamu wanauwana.

Human Beings are capable of incomprehensible diabolical exploits that can make you sick to the stomach. Tupende kutafuta amani na watu wote, tujishushe, tuthamini haki na utu wa wengine na tuache tamaa.....
Hizo Jamii ulizozitaja still zina kiwango cha juu Sana cha ujinga,thus utenda hayo.
 
Back
Top Bottom