Kizimbani kwa kujifanya yeye ni Rais Samia na kujipatia Tsh 40,000/-

Kizimbani kwa kujifanya yeye ni Rais Samia na kujipatia Tsh 40,000/-

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Mfoi alikiri hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Richard Kabate wakati Wakili wa Serikali, Ashura Mzava, akimsomea mshtakiwa maelezo ya awali, baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Mshtakiwa, anadaiwa kujiwasilisha kuwa yeye ni Rais Samia na kutumia laini ambayo haijasajiliwa.

Pia mshtakiwa huyo alikiri kwamba kati ya Septemba, 2021 ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa nia ya kulaghai umma alijiwasilisha kama Rais Samia Suluhu Hassan kupitia akaunti yake Facebook.

Alidai kupitia mtandao huo alijipatia Sh. 40,000 na pia Oktoba 2 alikutwa akitumia laini ya simu ambayo awali ilikuwa inamilikiwa na Getness Jackson kwa madai kwamba alipewa na mtu anayesajili laini.

"Ni kweli hii akaunti ya Facebook nilikuwa naitumia mimi, niliuziwa, lakini yaliyokuwa yakiendelea humo mimi siyajui na ni kweli nilikuwa natumia simu ambayo haijasajiliwa kwa kidole changu," alidai Mfoi.

Alikiri kwamba Septemba, 2021 alikamatwa na askari katika hoteli ya Malaika mkoani Mwanza na alipopekuliwa alikutwa anamiliki simu moja na laini iliyosajiliwa kwa jina la Jackson bila kutoa taarifa kwa mtoa huduma na kukamatwa.

Alidai wakati anahojiwa na askari, alikiri kutenda makosa yote na Agosti 4, 2021 alipelekwa mahakamani kujibu mashtaka yake.

Mshtakiwa huyo baada ya kukiri makosa hayo, alipewa jalada la mahakama kwa ajili ya kusaini na Hakimu Kabate aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 7, 2022 kwa ajili ya kupokea vielelezo vilivyotajwa kutokana na kukubali kukutwa navyo na kuvitumia.

Mshtakiwa alirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu na mwenye kazi ambayo inaaminika akiwa na Kitambulisho cha Taifa.

Chanzo: Nipashe
 
Aliyemshtaki ni nani ?aliyetapeliwa au Jamuhuri?

Ila mwamba katisha sana wampe miezi 6 tu inamtosha arudi na ubunifu mwingine😎😎
 
Back
Top Bottom