Yawezekama sijui, sasa kwa nyie wenye kujua, hebu tupeni basi cost benefit analysis na au business case inayo justify kujenga international airport hapo chato ili hali wanyama ndio kwanza wanasombwa kupelekwa huko... sipingi kuendeleza infrastructure, nachosema ni kwamba huko viwanja vya lami vinapotakiwa, vingepelekwa huko kwanza - mfano mikumi- watalii ni wengi, pembezoni mwa seregenti kama Mugumu, Selous, na sehemu nyingine ambazo zitaleta benefit kubwa muda mfupi...
Kwa hiyo Airport kuwepo chato: gharama za uendeshaji wake ni kubwa kuliko benefit, hasara itakuwa kubwa kuliko gharama za ujenzi... kumbuka mitambo ya kuongezea ndege, maafisa uhamiaji, waongoza ndege, grounds controller, usalama na mambo mengi yanayotakiwa kwenye 24/7 international airport.. je haya yote kweli Chato tunayaweza, je kuna volume ya watu/ watumiaji inayohitajika kukidhi huyo ujenzi au umejengwa tu ili mradi uonekane kwamba upo ? mbona viwanja vingi hasa vya mikoani hakuna lami kama mpango ni kuendeleza miundo mbinu?
Iweje Chato ipewe kipaumbele zaidi kuliko mikoa mingine ambayo ni ya zamani sana kuliko chato ? hapo ndio utaona ni kwa nini watu wananyoosha vidole vyao huo chato... hata kama JPM anatokea hapo, upendeleo si wa lazima... Ingependeza zaidi kuona kwamba viwanja vyote Tanzania vimewekewa Lami na baada ya hapo ndio vingine vifuatie kama hiyo chato...