Kizungumkuti hifadhi ya Burigi

Viwanja vya ndege vilivyopo vina hali mbaya na vinahitaji matengenezo makubwa kwanini kujenga uwanja wa kimataifa mahali ambapo hakuna shughuli za kimataifa zinaendelea?
Mbona viwanja vinakarabatiwa? Nafaham kuna ukarabati Mkubwa wa Kiwanja cha Ndege cha Songea unaendelea. Hebu wasiliana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania utapata taarifa sahihi na rasmi. Usisubirie taarifa sahihi Huku JF mana hizi sio taarifa rasmi.
 

Yawezekama sijui, sasa kwa nyie wenye kujua, hebu tupeni basi cost benefit analysis na au business case inayo justify kujenga international airport hapo chato ili hali wanyama ndio kwanza wanasombwa kupelekwa huko... sipingi kuendeleza infrastructure, nachosema ni kwamba huko viwanja vya lami vinapotakiwa, vingepelekwa huko kwanza - mfano mikumi- watalii ni wengi, pembezoni mwa seregenti kama Mugumu, Selous, na sehemu nyingine ambazo zitaleta benefit kubwa muda mfupi...

Kwa hiyo Airport kuwepo chato: gharama za uendeshaji wake ni kubwa kuliko benefit, hasara itakuwa kubwa kuliko gharama za ujenzi... kumbuka mitambo ya kuongezea ndege, maafisa uhamiaji, waongoza ndege, grounds controller, usalama na mambo mengi yanayotakiwa kwenye 24/7 international airport.. je haya yote kweli Chato tunayaweza, je kuna volume ya watu/ watumiaji inayohitajika kukidhi huyo ujenzi au umejengwa tu ili mradi uonekane kwamba upo ? mbona viwanja vingi hasa vya mikoani hakuna lami kama mpango ni kuendeleza miundo mbinu?

Iweje Chato ipewe kipaumbele zaidi kuliko mikoa mingine ambayo ni ya zamani sana kuliko chato ? hapo ndio utaona ni kwa nini watu wananyoosha vidole vyao huo chato... hata kama JPM anatokea hapo, upendeleo si wa lazima... Ingependeza zaidi kuona kwamba viwanja vyote Tanzania vimewekewa Lami na baada ya hapo ndio vingine vifuatie kama hiyo chato...
 
Hivi una taarifa za kutosha kusema hayo eddy? Acha uvivu tafuta taarifa sahihi. Neno kivutio Lina maana pana Sana. Inawezekana Burigi kuwa Chato ni kivutio pia mana ndo Nyumban Kwa Mhe. Rais. Kitu kuwa kivutio inategemea namna tunavyokipackage.
Hifadhi ya burigi inaunganisha mapori manne yaani biharamulo Burigi rumanyika na Kinesi, hifadhi hii iko katika wilaya za chato biharamulo muleba ngara na karagwe na ilianzishwa na chief Omukama Rumanyika kabla hata mjerumani hajaja, Sasa wewe unazungumza as if Ni shambapori la eka tano, huu upotoshaji mtaacha lini? Ndio maana Jana hamkwenda kanisani Mungu hapendi waongo
 
Mpango uliopo kufikia 2025 kila mkoa iunganishwe kwa lami, kila mkoa uwe na uwanja wa ndege, tatizo maeneo mengine wajuwaji badala ya kuweka mipango kazi wamekalia porojo
 
Ungeweka na idadi ya ndege za kibiashara au za kitalii zinazotua hapo tangu kumalizika kwa uwanja na uwepo wa hiyo hifadhi ya wanyama.

Kama hauna, alichosema TL kitabaki sahihi labda kama kinauma
I wonder. Ina maana watalii wanaoshuka Serengeti ama Arusha ni wengi kuli wa Chato. Pale Mwanza pana uwanja mkubwa wa kimataifa wa ndege, na ni mwendo karibia wa masaa mawili kufika chato. Kwa nini usitumike wa Mwanza?
 
Ukiangalia Kwa muda mfupi costs zinaweza outweigh benefits katika Ujenzi wa Chato Kwa sasa. Lakini uwanja ule huko mbeleni kama tutatimia vzr uwepo wake unaweza leta faida kuliko hata viwanja vingine tulivyonavyo. Kuleta faida au kutoleta faida inategemea na Sisi watanzania tumejipangaje kutumia uwanja huo.

Mathalan, sasa hivi wanao market Hifadhi ya Taifa ya Burigi, kwao uwepo wa uwanja huo ni a Plus. Kwasisi tunaokaa kusubiria kuona watalii wametua Chato bila kufanya jitihada zozote za kutumia fursa hiyo hatuwezi kuona faida za uwanja huo.

Ilipaswa sasa hivi watu waende Chato/Geita kufungua mashamba makubwa ya kibiashara Ili wakivuna mazao yatoke Chato direct to Walaji wa nchi zilizoendelea. Au tuanze kutumia uwepo wa Kiwanja hicho kumarket hifadhi za Magharibi mwa Tanzania Kwa nguvu zote. Badala yake tumekaa pemben tunarusha lawama. Kwa uzoefu wangu, uwanja huu hata ungejengwa Arusha bado tungelaumu. Sisi ni kama wana wa Israeli, hatuna jema.
 
Kama hayo mapori yote yaliyopandishwa hadhi yapo mkoa Kagera isipokuwa pori la Chato, na hata hiyo Chato ilikuwa Kagera kabla haijafanyiwa figisu na kuwekwa Geita, na kwankuwa zaidi ya 70% ya hifadhi hiyo ipo Kagera kwa nini hiyo hifadhi haikuitwa jina la Kagera? Na ili hizo huduma zote zikapelekwe Kagera huko kwenye hiyo hifadhi?? Maana hifadhi hiyo ime cover maeneo ya wilaya za Karagwe, Muleba na Biharamulo zote za mkoa wa Kagera.

Huu ubinafsi wa serekale ya V[emoji57][emoji57]
 
I wonder. Ina maana watalii wanaoshuka Serengeti ama Arusha ni wengi kuli wa Chato. Pale Mwanza pana uwanja mkubwa wa kimataifa wa ndege, na ni mwendo karibia wa masaa mawili kufika chato. Kwa nini usitumike wa Mwanza?
Mwanza Burigi Ni 360km mtalii gani utamtembeza umbali huo? Mbona mnatumia masaburi kufikuri?
 
Kwani Hifadhi inaitwa Chato!?

Mbona inaitwa Burigi. Na geti kuu liko Biharamulo.

Uwanja upo Chato ambayo ipo katikati ya Rubondo, Saa nane na Burigi national parks.

Ulitaka uwanja ujengwe Biharamulo!? Isingewezekana viwanja viwili vya kimataifa kuwa mkoa mmoja maana kwa Kagera Uwanja upo tayari.

Upendeleo uko wapi!?
 
Hifadhi ya Rwanda inaitwa Kagera tutawachanganya watalii, bukoba karagwe Ni milima, eneo tambarare la kujenga uwanja Ni Chato, eneo pekee kingine Ni murugwanza ngara lakini liko mpakani ndege unaweza dunguliwa na majirani kwa bahati mbaya
 
Hili eneo la uhifadhi ni eneo langu kitaaluma. Nimkulia na kuzeekea humo. Hivyo, jua ninauelewa mpana Sana kwenye uhifadhi ndo mana nkamwambia neno kivutio Lina maana pana inategemea namna mnavyojipackage.
 
Mpango uliopo kufikia 2025 kila mkoa iunganishwe kwa lami, kila mkoa uwe na uwanja wa ndege, tatizo maeneo mengine wajuwaji badala ya kuweka mipango kazi wamekalia porojo
Porojo kwa kweli ni nyingi..Miaka 59 ni mingi sana kuwepo madarakani- ingefaa hizi habari za lami nchini mwetu kila sehemu hadi kijijini ziwe historia...
 
Porojo kwa kweli ni nyingi..Miaka 59 ni mingi sana kuwepo madarakani- ingefaa hizi habari za lami nchini mwetu kila sehemu hadi kijijini ziwe historia...
Mipango ya maendeleo inahitaji muda mrefu, nchi zilizoendelea Zina mipango mirefu, malkia wa uingereza ana miaka 60 ikulu, nchi yetu sio maabara yakufanyia majaribio inahitaji watu wenye weledi sio porojo za majukwaani
 
UWANJA WA NDEGE WA CHATO
Kutokana na kupandishwa hadhi mapori hayo na kuwa hifadhi ya taifa kwa namna moja au nyingine ni lazima kuwepo kwa uwanja wa ndege ili uraisishe utali na kupanua wigo wa utali.
huo sio uwanja wa ndege tuu ila ni uwanja wa ndege wa kimataifa, sasa kati ya huko chato na iringa wapi kulipaswa kujengwa uwanja wa hadhi hiyo kama kigezo ni utalii?
 
huo sio uwanja wa ndege tuu ila ni uwanja wa ndege wa kimataifa, sasa kati ya huko chato na iringa wapi kulipaswa kujengwa uwanja wa hadhi hiyo kama kigezo ni utalii?
Wacha uongo, Kama Ni international airport tupatie codes zake, wa dar Ni JKIA wa Moshi Ni KIA huo wa chato codes zake zikoje?
 

..hakuna aliyemkosoa kwa kujenga hoteli.

..fedha alizotumia kujijengea uwanja wa ndege angezitumia kwenye miradi inayogusa wananchi wengi.

..hivi Mbowe au Sugu wangetumia fedha za mfuko wa jimbo kwa mradi unaowanufaisha wao tu na hoteli zao ungewaunga mkono?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…