Kizungumkuti hifadhi ya Burigi

Hifadhi ya burigi ilianzishwa na chifu rumanyika was falme za bunyoro alikuwa akifugia ngombe zake, wacheni kupotosha,
 
Hivi ni pori ama ni mbuga?

Sehemu ya ustawi wa wanyama kuweza kuonekana na kuwa kivutio cha utalii ni mbugani ama porini?

Nimeuliza jinsi jiografia ilivyokaa kaa huko, nipate mwanga kidogo niweze kuchangia hoja.
 
Hivi ni pori ama ni mbuga?

Sehemu ya ustawi wa wanyama kuweza kuonekana na kuwa kivutio cha utalii ni mbugani ama porini?

Nimeuliza jinsi jiografia ilivyokaa kaa huko, nipate mwanga kidogo niweze kuchangia hoja.
Pori Kubwa Sana
 
Mleta mada kahakikishe Kwanza ukweli wa mambo uliyoongea. Burigi haipo mkoani Geita isipokuwa kwa sehemu ndogo inaingia mkoani Geita.

Na mapori mengine yote uliyotaja hakuna hata moja liliko Geita labda la Kibanda kama lipo.

Kama ni suala la uwanja wa kuyafikia mapori yote hayo kwa Pamoja uwanja wa Ndege wa Bukoba ungekuwa centre ya kuyafikia kwa urahisi.
 
Serengeti National Park iko Mara, kwanini hawajajenga International Airport Mara?

Ruaha National Park iko Iringa, kwanini hawakujenga International Airport iringa?

Gombe National Park iko Kigoma, Je kuna International Airport Kigoma?

Katavi National Park iko Katavi, Je kuna International Airport Katavi?

Kuna hifadhi nyingi tu kama Ngorongoro, Selous, Mikumi, Manyara n.k lakini huko kote havikujengwa viwanja vya ndege vya kimataifa. Kwanini Chato??

Au hifadhi ya burigi inapokea watalii wengi kuliko hifadhi za Serengeti, Ngorongoro, Mikumi, Selous, Manyara, na nyinginezo ??
 
Hilo la uwanja wa ndege, nilidhani ungejengwa kwanza Mwanza International Airport ili iwe Katikati ya Mara na Kagera lakini cha kushangaza Mwanza hakuna uwanja wa Ndege!(watu watashangaa hakuna vipi) uliza nitakujibu
 
Umekuwa mwalimu wa lugha....!!!!
Hu ni udhaifu wa hoja ndugu,Mara nyingi watu Kama nyie mkisoma thread alafu mkaona zipo nondo mnatafuta Sasa makosa ya kiuwandishi.
Wewe Kama huna hoja pita kushoto..

Mtu kama huyo maskini kuandika kwenyewe hajui!! unanzaje kumjibu kwa hoja? Nyie endeleeni kula buku saba zenu kwa kuja kuandika upupu humu Ila mjue huu sio ushabiki wa simba na Yanga, mnachezea roho za watu kwa vijisent vidogo mnavyolipwa.
 
Hivi zile ngeu za juzi zimetikisa ubongo, tangu lini chato airstrip imekuwa international airport?

Serengeti Kuna KIA, ruaha Kuna uwanja wa nduli, gombe Kuna kigoma airport, katavi Kuna mpanda airport, mbeya hakuna kivutio chochote Kuna songwe airport, burigi ilikuwepo hata mjerumani aliikuta, kuwa na uwanja wake ishakuwa nongwa, mbona Mtei alijijengea Arusha airport Tena akiwa wazuri tu na hamsemi, ovyo
 
Hilo la uwanja wa ndege, nilidhani ungejengwa kwanza Mwanza International Airport ili iwe Katikati ya Mara na Kagera lakini cha kushangaza Mwanza hakuna uwanja wa Ndege!(watu watashangaa hakuna vipi) uliza nitakujibu
Fedha zilitolewa tangu enzi ya kikwete wajanja wakapiga juu kwa juu bil 200 zililambwa na hawasemi
 
Kwani unafikir hawajui
 

Duh we jamaa mzushii, umetembelea mbuga kweli wewee?? Mikumi, Tarangire, Selous, Manyara, Gombe??? Zote mapato wanategemea ngorongoro na serengeti???
 
Umekuwa mwalimu wa lugha....!!!!
Hu ni udhaifu wa hoja ndugu,Mara nyingi watu Kama nyie mkisoma thread alafu mkaona zipo nondo mnatafuta Sasa makosa ya kiuwandishi.
Wewe Kama huna hoja pita kushoto..
"Kiuwandishi", vijana wa slowslow wanatia aibu. Kosa siyo lenu ila kosa ni la aliyewapa ajira
 
Tunaomba Idadi ya Ndege zinazotua hapo Uwanjani Chato kuleta watalii wanaokuja kutembelea hio mbuga ya Burigi, Vinginevyo Lissu atabaki kuwa mkweli mpka mtakavyoleta ushahidi wa hayo mnayodai yanafanyika katika Uwanja wa ndege pamoja Mbuga ya Burigi.
 
Huyu ikiwa hatakatwa na NEC ni bora wasiojulikana wamalizie kazi yao ili sisi tulio wengi, watoto wetu na wajukuu wetu wabaki salama.

Hatuwezi kuwa na mtu muongo, mzushi na mfitini namna hii lengo lake akijua ni kuharibu amani ya nchi awafurahishe wenzie
 
Ukweli ni kwamba hizo hifadhi zimeanzishwa kisiasa kwa maslahi ya watu au mtu kwa mitazamo yao au yake. Nia haikua mbaya ila uanzishwaji wake kwangu nauona una mashaka. Hayo mapori yalikua machafu toka miaka na miaka na uanzishwaji wake umekua niwaharaka sana ukilinganisha na hali halisi. Hadi sasa Tanapa ina hifadhi nyingi tegemezi sasa kuwaongezea hizo mbuga tena kwa haraka nikuwaongezea mzigo usio wa lazima.

Nakuhakikishia ata ilazimishwe vip hizo hifadhi hadi zifikie daraja la kati lakuingiza ata wageni 200 kwa mwaka sio chini ya miaka 20.Nakama lengo lilikua nikuongeza idadi ya wageni suluhisho la kwanza lisingekua kuanzisha hifadhi mpya bali kuboresha kwanza zilizopo kwa maana ya zile zinazozalisha vizuri(serenget, tarangire, kilimanjaro, ngorongoro, manyara n.k) zizalishe zaidi kisha kugeukia zisizozalisha vizuri(ruaha, mkomaz, kitulo, rubondo, mahale, gombe, odzungwa, mikumi n.k) zifikie kuzalisha vizuri kisha ndo wazo lakuanzisha hizo nyingine lingekuja, tena ilitakiwa zipande moja baada ya nyingine.
 
Duh we jamaa mzushii, umetembelea mbuga kweli wewee?? Mikumi, Tarangire, Selous, Manyara, Gombe??? Zote mapato wanategemea ngorongoro na serengeti???
Unyumbu mbaya jamanii
Kasema kwa kuingiza mapato mengi.Japo kaeleza kwakifupi ila hifadhi chache ndizo zilikua zinaingiza mapato yakusaidia hifadhi nyingine.Kuna kilimanjaro,serenget,arusha,tarangire,manyara pamoja na mamlaka ya ngonrongoro.Hizo nyingine zinajazia tu ila ukilinganisha makusanyo yao na matumizi ni tofauti.Nahizi takwimu zipo tafuta utazipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…