Kamukhm
JF-Expert Member
- Aug 30, 2015
- 2,801
- 4,212
Unajua hapa ndipo tunapofail.. kupanga kwa ajili ya Leo na kesho. Mkuu strategic planning inangalia mbali Sana.. na lengo nikueven out spending ya serikali kuleta harmony katika ukuaji wa Miji yote.Sawa, Ngoja nikubaliane na wewe. Tunza post yako, Mungu akitujalia uhai, uje na takwimu ni watumiaji wangapi watakuwa wameutumia uwanja huo wa chato toka sasa hadi 2025. Hawatafika hata Milioni moja... mark my word.
Miundombinu inao mchango mkubwa katika kuvutia uwekezaji na fursa za kibiashara. Pori la Burigi limepandishwa hadhi litatunzwa zaidi matokeo yake kutakuwa sio na wanyama wengi tu ila pia kutunza mfumo wa kiikolojia ambao unaharibika kwa kasi.
Lakini pia misitu itakuwa na kusaidia kuoffest carbon kutokana na uzalishaji mkubwa unaoendelea katika Miji ya Kanda ya Ziwa ambayo pia ndio ukanda populous zaidi nchini. Na kuboresha upatikanaji wa mvua
Sasa kuvutia uwekezaji lazima uwe na trigger projects ... Na Uwanja wa Chato Ni moja tu ya hizo trigger projects . Lakini maboresho ya barabara nyingine Muhimu Kama tabora Kahama Geita-chato. Geita Sengerema Mwanza(Ujenzi wa daraja Busisi) nk.
Sasa Hawa watu (milion kumi wa kushuka) wataanza kushuka lini Chato Ni swala la muda. Lakini biashara nyingi zitasogea sababu ya Uwanja. Na lazima ukumbuke kule tunapokea mvua nyingi pia, na udongo sio mzuri kuwa na njia ya lami Ni advantage.
Zaidi kilichojengwa ni runway tu ya lami, uwezo wa kupokea abiria ni pamoja na miundombinu mingine wezeshi.. ikiwemo jengo la abiria, maeneo ya kutunzia/kupaki ndege nk..na hivi vyote kwa chato bado.