Kizungumkuti hifadhi ya Burigi

Kizungumkuti hifadhi ya Burigi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Tuwekane sawa kidogo kuhusu mambo ya uongo ambayo ameongea ndugu TUNDU LISU mgombea uraisi kwa nafasi kupitia chama Cha demokrasia na maendeleo.

HIFADHI YA TAIFA YA BURIGI
Mwanzo kabisa hi hifadhi ya taifa ya burigi kabla kupandisha hadhi kuwa hifadhi ya taifa ya wanyama pori, Lili kuwa ni pori moja wapo ya mapori ya hifadhi ya serekali ambalo linapatikana mkoa wa Geita, Hili pori lilianzishwa mwaka 1980 Kama pori la hifadhi la akiba.

Katika ukanda huo kwa maana ya mikoa ya Geita na Kagera yalikuwa yanapatikana mapori Kama vile:

Burigi
Kimisi
Biaramulo
Kibanda na
Rumanyika.

Mwaka 2018-2019 kwenye bunge la bajeti,wizara ya utali walipeleka hoja bungeni ya kuomba kupandishwa hadhi baadhi ya mapori ya akiba na kuwa hifadhi za taifa,mapori hayo ni Burigi,Biaramulo,kibanda na rumanyika.

Haya mapori yote yapo katika ukanda muhimu Sana wa ki ikorojia.

Lengo la wizara ya utali kupeleka hiyo hoja ni kwa sababu ya kupanua utali na kuongeza mapato ya taifa ndani ya miaka Saba ili yafikie bill.16 USD yani maana yake wastani wa watali kufikia mil.8 kwa miaka hiyo Saba.

Wa bunge wote wa bunge la Tanzania walipitisha na wakiwemo na wabunge wa Chadema na yule mtoa vimemo vya uongo kwa mgombea wao bwana Mnyika alikuwepo kwenye kupitisha maamuzi hayo.

Lakini wabunge walikubaliana hayo kwa hoja nyingine ya msingi.

Biharamulo,Burigi na Kimisi haya yote yaliunganishwa na kuwa hifadhi ya taifa kwa jina la BURIGI na mapori haya yote yamezungukwa na kata 18 na vijiji 48.

UWANJA WA NDEGE WA CHATO
Kutokana na kupandishwa hadhi mapori hayo na kuwa hifadhi ya taifa kwa namna moja au nyingine ni lazima kuwepo kwa uwanja wa ndege ili uraisishe utali na kupanua wigo wa utali.

Sasa ndio unaona uongo wa huyu mgombea wa CHADEMA bwana TUNDU LISU kwamba uwanja wa ndege raisi MAGUFULI kajenga kwa ajiri yake.

RAI YANGU KWA WATANZANIA
Tumpinge vikali Sana huyu muongo wa taifa na mchonganishi wa taifa letu kwa huu upotoshaji anaoufanya kipindi cha kuelekea kwenye kampeni za uchaguzi mkuu
 
Mwaka huu maji mpaka muyaite "mma!"

Ila mkumbuke asiyekubali kushindwa si mshindani. Kwa hilo tu inatosha sana kwa waungwana kuwatia adabu vilivyo. Tayari mnakera mno!

Yanini kuwabughudhi kina Sugu, Lissu, ACT, CDM etc, wagombea au mashabiki wao?

Msidhani kuwa watu hawawaoni.
 
Ungeweka na idadi ya ndege za kibiashara au za kitalii zinazotua hapo tangu kumalizika kwa uwanja na uwepo wa hiyo hifadhi ya wanyama.

Kama hauna, alichosema TL kitabaki sahihi labda kama kinauma
Swadakta
 
Kajifunze kwanza kuandika hakuna "ajiri" kwenye Kiswahili.
Wahi kwa aliyekutuma akupe ujira wako japokuwa kazi ni mbovu.
Umekuwa mwalimu wa lugha....!!!!
Hu ni udhaifu wa hoja ndugu,Mara nyingi watu Kama nyie mkisoma thread alafu mkaona zipo nondo mnatafuta Sasa makosa ya kiuwandishi.
Wewe Kama huna hoja pita kushoto..
 
Nimepata Bahati Nzuri Ya Kupita Hilo Mbuga

Kutokea Karagwe Kwenda Ngara

Sikukutana Na Wanyama Zaidi Ya Mbweha Watatu Kwa Umbali Tofauti Tofauti.

Pori Ni Kubwa Sana, Lingekuwa Kama Mikumi, Tarangire, Hata Pori La Akiba Pale Lamadi Kwenye Mizani Ukipita Wanyama Unawaona Tu
 
Hakuna mapato yeyote huko. Ni kuongeza tu matumizi yasiyo na maana. Mbuga mbili tu ndo zinaingiza pesa nyingi zaidi ya mapato. Ngorongoro na Serengeti. Hizo nyingine pesa za kuendeshwa zinatokana na Serengeti na Ngorongoro. Fanya research uache upuuzi
 
Kajifunze kwanza kuandika hakuna "ajiri" kwenye Kiswahili.
Wahi kwa aliyekutuma akupe ujira wako japokuwa kazi ni mbovu.
Neno ajiri lipo kwenye kiswahili lakini halina maana aliyotumia mwandishi.
 
mimi npo huku hata leo nimepita hapo luna tumbiri tu basi na nyani,
Lingeendelea kuwa pori la akiba tu kwanza,
kwa sasa linatia hasara tu gharama za uendeshaji,
pia awali raia walikuw wanapata riziki kupitia hilo pori.
lkn sasa limewagharimu wengi sana.
 
Back
Top Bottom