Kocha wa JS Saoura ya Algeria awatolea povu waandishi wa michezo wa Bongo kwa Kuandika ndivyo sivyo. Aliyasema hayo baada ya kichapo cha mabao 3 toka kwa Simba SC ya Tanzania leo jioni
Kocha huyo wa JS Saoura amedai Simba imebebwa sana na maamuzi mabovu ya refarii na magazeti ya Tanzania jana kuandika habari zisizo sahihi kimechezo.
Kocha huyo wa JS Saoura ametoa angalizo Simba ijisahihishe na kutobweteka na ushindi wa leo maana JS Saoura ni timu changa na siyo timu kubwa kama za Al Ahly, AS Vita au Simba SC.