Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Katika kile kinachoonekana kama kukaribishwa kwenye michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya, timu ya Genk anayoichezea mtanzania Mbwana Samatta imezabwa mabao 6-2 na klabu ya Salzburg katika mchezo wa kwanza wa kundi linalojumuisha pia mabingwa watetezi Liverpool na Napoli.
Samatta alifanikiwa kufunga bao la pili kwa timu yake kabla ya kulambwa kadi ya njano(baada ya kadi nyekundu kufutwa) kwa mchezo mbaya. Samatta angekosa michezo ya kwanza dhidi ya Liverpool na Napoli. Genk wakiwa ugenini wamenyanyasika vya kutosha na Salzburg ambayo husifika kwa kufunga.
Pole Samatta, pole Genk. Mwanzo daima huwa mgumu.
NB: Liverpool imezabwa mabao 2-0 na Napoli ya Italia